Mkuu Wa Mkoa wa Pwani, Avunja Shule Ya Msingi Tondoroni na Kumilikisha Eneo la Kijiji kwa Jeshi:

mzawa1

New Member
Jan 4, 2012
1
0
Wadau , Nilikuwa na pita njia ya Kwenda kisarawe kutokea Kilvya pwani, nikakuta shule ya Msing ya Tondoroni ikiwa imesambaratishwa na Tinga Tinga chini ya ulinzi mkali wa polisi. Barabara nayo ilikuwa imechimbwa kiasi cha kusababisha usumbufu kwa sisi tuliokuwa tukitumia nyia hiyo muda huo. Tarifa nilioipata ni kwamba, Mkuu wa mkoa ameagiza shule ivunjwe na ameaamuru wa wananchi kuondoka katika eneo hilo akishinikiza ni eneo la jeshi. Kuna kesi mahakama ya ardhi iliodumu kwa miaka isiopungua 20 na bado haijatoa hukumu kuwa mmiliki wa eneo hilo ni jeshi or ni wananchi. Kijiji kimesajilliwa na Jeshi lilipelekwa kule likaikuta shule hiyo na shuguli za kilimo zikiendelea katika eneo hilo lenye Rutuba sana, nampaka sasa kijiji bado kinatambulika na hati ya kijiji haijafutwa.
Vidole vinanyooshewa vigogo wastaafu akiwemo waziri mkuu mstaafu, Jamani mbona viongozi wastaafu hawaridhiki hata baada ya kunyonya wakiwa madarakani?????

Mkuu wa mkoa wa pwani, ameonyesha kutokuwa makini na kukosa ushirikiano kwa kamati yake nzima ya mkoa kwa kusahau kuwa mgogoro wa eneo hilo upo mahakamani na bado shauri lake la msingi halijatolewa hukumu.

Chakushanga kesi inahusisha vijiji 3, na kijiji cha tondoroni kipo mbali sana na Jeshi lakini ndo kinatolewa macho na katika vijiji viingine kuna shule na pia hawachukui eneo lote .

Tondoroni kunaniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii......
 
Mimi nilipoona thread yako kwenye list *mkuu wa mkoa wa pwani avunja....* nikajua kavunja ungo, enhe!

Sasa kavunja shule je watoto wa hao wanajeshi watasoma wapi? Kama yupo hapo karibu yako mnase makofi tu, katiba inaruhusu na statement yako itaandikwa amenaswa makofi na mwananchi mwenye hasira
 
Mkuu wa mkoa wa Pwani si yule mama anayependa kuongea sana! Bi Mwantumu Mahiza! Kama ni kweli hilo eneo ni la jeshi basi sheria ichukue mkono siyo kuendelea kujenga mazoea ya kunyemelea maeneo yasiyotakiwa.
 
Anajua wakwere hawahitaji elimu ndio maana. Labda kawatengenezea sehemu ya kucheza ngoma. Si unaona hata Mkuu wa kaya kasoma lakini wapi, kila kitu kinamshinda. Sasa watoto wao wapate elimu ya nini? Wakadumishe mila?
 
Back
Top Bottom