Mkuu Mzee Mwanakijiji, Rais Magufuli Sio Alfa na Omega. Rais Sio Mungu! Na Kwenye Utawala ni Katiba!

The big problem with that so called @Mwanakijiji is inflated ego.

Hadi anatupangia vitu vya kuongelea kama jamii... Kwamba tuongelee mambo ya maji vijini... Who gave him that right in the first place?

Dunia ya mahaba na hadaa....
Hata wewe Paschal ulishadadia sana haya mambo.
Chicken have come home to roost, keep quite.

KAMA ABBAKE MAGOGONI, ATAKJI TUNGALIE SHILAWADU ILA YEYE ANAIPENDA SANA!
 
Hii nguvu tunayoitumia kwenye hili swala la Makonda tungeiwekeza kwenye Kilimo leo hii tungekuwa na foodbasket wa Dunia, au hata tu kwenye kupigania Rasilimali zetu zinazopokwa kila uchawao na wageni!

Sisi Waafrika ni watu wavivu sana!
Hizo rasimali tukapiganie sisi wakati wao wanawapa kiurahisi kwa kusaini mikataba yao. Mnataka watu waende huko kwenye rasimali waonekane wahalifu wamevamia eneo la muwekezaji?

Tunaanzia hapa kwenye jino bovu tulkiling'oa tu kinywa kitabaki salama.Hivyo hata hamu ya kulima inakosekana kwa sababu utawala bora hakuna wala sheria hazifuatwi inavyotakiwa.

Wateule tu ndio wanaoishi kama malaika ila sisi wengine ndio tunaoishi kama mashetani kwa kauli ya hilo jino bovu tena ni lile gego la mwisho.

Time will tell.

AMANI YA UOGA HII INATUPONZA MPAKA TUNAPIGA MAKOFI PANOTUUMIZA.
 
Umeandika huku tunajua unataka Mh. Makonda aondolewe

Umeobyesha kuwa jana ulipigwa mshtuko mkubwa kama wenzako

Humu unajitia ujanja kuandika kijanja, ila wengine sisi tunayaona kupita maneno yako hata ukoroge vipi.

Mtanyooka tu, umevizia kutumia mada ya mtu ili mfunze watu wavunje amani nchini. Hii imeanza masaa yaliyopita, na wewe naona umo.

Mmmmmh

Mnatumwa wote wakati moja au mnapewaje tasks za kufanya mitandaoni?

JPM oyeeeeeee
Makonda oyeeeeee
Ajabu ya Mussa, woooote mnaopingana humu, Paskali, Bashite, Mwanaamerica , JPM, Coco . . , wooote wa kanda hiyo hiyo . .

Inasikitisha sana kumbe mlipokua mnamtetea JPM na Bashite mlikuwa mkifikiri kiukabila kabila . . , sasa Babeli ni dhahiri . .
 
Hizo rasimali tukapiganie sisi wakati wao wanawapa kiurahisi kwa kusaini mikataba yao. Mnataka watu waende huko kwenye rasimali waonekane wahalifu wamevamia eneo la muwekezaji?

Tunaanzia hapa kwenye jino bovu tulkiling'oa tu kinywa kitabaki salama.Hivyo hata hamu ya kulima inakosekana kwa sababu utawala bora hakuna wala sheria hazifuatwi inavyotakiwa.

Wateule tu ndio wanaoishi kama malaika ila sisi wengine ndio tunaoishi kama mashetani kwa kauli ya hilo jino bovu tena ni lile gego la mwisho.

Time will tell.

AMANI YA UOGA HII INATUPONZA MPAKA TUNAPIGA MAKOFI PANOTUUMIZA.

Nimetumia neno sisi, hivyo ni kila Mtanzania, kwamba sisi ni watu wavivu sana, na hii ni wote kuanzia Viongozi mpaka Wananchi, na ndiyo maana Miezi miwili tunapoteza kujadili Mkuu wa Mkoa mmoja tu ambaye hata kama akiondolewa hakuna chochote kitakachobadilika!
 
Hii nguvu tunayoitumia kwenye hili swala la Makonda tungeiwekeza kwenye Kilimo leo hii tungekuwa na foodbasket wa Dunia, au hata tu kwenye kupigania Rasilimali zetu zinazopokwa kila uchawao na wageni!

Sisi Waafrika ni watu wavivu sana!
Kwanini usishauri kua tushughulikie hilo swala la Makonda na hapo hapo tushughulikie kua foodbasket wa dunia?
 
Hakuna jipya, hata Wazungu na Waarabu waliotawala Afrika yetu ndiyo maana waliondoka, tena kwa hiari!

Ndiyo hao wanarudi kwa mwendokasi,maana watawala hawajui kama WAKOLONI wanarudi wakijifanya sisi WACHINA marafiki zenu.

Stupid watawala wa Afrika hakuna hata wenye akili
 
Ndiyo hao wanarudi kwa mwendokasi,maana watawala hawajui kama WAKOLONI wanarudi wakijifanya sisi WACHINA marafiki zenu.

Stupid watawala wa Afrika hakuna hata wenye akili

Hakuna kitu kama Watawala wa Kiafrika Dunia hii, bali kuna Waafrika ambao huja kuwa Watawala, hivyo kwa kifupi hakuna tofauti kati ya Mtawala na Mtawaliwa kwani wote wawili ni wamoja tofauti tu mmoja ana cheo mwingine hana, laiti yule asiye na Cheo ukimpa Cheo atafanya yale yale ambayo yule mwenye Cheo anafanya!
Na ndiyo maana tunapoteza muda kujadili mambo ambayo hayatusadii, hivyo hata sisi tukiwa Watawala tutendelea na yale yale ya akina Nape, Zito &Co. mipasho, unafiki na Majungu tu na hakuna jipya!
 
Hii nguvu tunayoitumia kwenye hili swala la Makonda tungeiwekeza kwenye Kilimo leo hii tungekuwa na foodbasket wa Dunia, au hata tu kwenye kupigania Rasilimali zetu zinazopokwa kila uchawao na wageni!

Sisi Waafrika ni watu wavivu sana!
Mkuu maisha ya binadamu siyo kushiba tu. Wakati mwingine watu wako radhi hata kufa kwa njaa ili mradi haki itendeke
 
Ndiyo maana wenye maono wanataka tuwe na katiba ya kujenga institutions imara na siyo mtu imara. Katiba nyingi za nchi za africa ni za kujenga mtu imara, akiamua kufanya atakavyo matokeo yake tunayashuhudia kila siku.
 
Wanabodi,
Hili ni bandiko la kumjibu mwana JF mwenzetu, Mkuu Mzee Mwanakijiji, aliyesema rais Magufuli ni Alfa na Omega, hapa mimi natofautiana naye kuwa rais Magufuli sio Alfa na Omega, Alfa na Omega ni Mungu tuu pekee, rais Magufuli sio Mungu, ni mkuu wa nchi yetu, lakini yeye sio kila kitu, hivyo hawezi kuwa Alfa na Omega.

Tukiacha yaliyo ya Kimungu, tukija kwa yaliyo ya Kaisari na kwenye utawala wa nchi, pia rais sio Alfa na Omega, bali katiba ya nchi ndio kila kitu, rais yuko chini ya katiba. Kitendo chá rais Magufuli kuikanyaga katiba na kuachwa tuu hivi hivi akiangaliwa, ndiko kumepelekea baadhi yetu kumuona yeye ndio kila kitu hadi kumfananisha na Alfa na Omega.
Hata mimi jana nilimsikia rais Magufuli alipozungumza kuwa kwenye mambo ya uteuzi, yeye ndio kila kitu, hakuna yoyote anayeweza kumpangia kitu, hii sii kweli, kiukweli rais sio kila kitu, bali katiba ndio kila kitu hivyo kuna vitu hata rais anapangiwa na kulazimishwa avifanye atake asitake, apende asipende.

Hii maana yake kuna vitu ambavyo rais anavifanya at his discretion kwa mapenzi yake na kuna vitu anatakiwa kuvifanya not at his discretion bali kwa lazima kwa mujibu wa katiba.

Kwanza sote tunakubaliana kuwa Magufuli ndiye rais wetu, ndio mamlaka kuu kupita zote za kiutawala nchini mwetu mwenye nguvu kubwa hivyo anapaswa kuheshimiwa, lakini sio kuogopewa au kuabudiwa as if yeye ni Mungu!. Hili nimelizungumza hapa Nilivyomdhania Magufuli kumbe sivyo...

Rais ana powers, ila sio absolute powers, yuko chini ya katiba, katiba ndio kila kitu, hata rais akimess, anaondoshwa!. Kuhusu mamlaka ya rais kumteua yoyote, nimeieleza hapa. Je, wajua Rais aweza kuteua yeyote hata darasa la saba?. Teuzi hizi hazihojiwi popote na yeyote!

Magufuli japo ni rais wetu na yeye ni binadamu kama sisi na sio malaika, hivyo ana mapungufu yake, na moja ya mapungufu yake makubwa ni hili kwa vile yeye ndio rais wetu, hivyo anajidhania yeye ndio kila kitu. Lakini kwa bahati mbaya sana, japo ameapa kuilinda katiba, lakini imetokea kuwa kumbe Magufuli haijui hata hiyo katiba yenyewe aliyoapa kulinda ndio maana baadhi ya maamuzi yake yanakwenda kinyume cha katiba, kwake it's OK kwa vile hajui atendalo ni kinyume cha katiba, na anatenda kwa nia njema, na hili hata mimi simlaumu kwa sababu yeye sio mwanasheria ila ni ajabu kwa wanasheria wanaojua rais anavunja katiba lakini wanamnyamazia Gwiji wa Sheria na Katiba, Prof. Issa Shivji, Agoma Kuzungumzia Dhana ya Udikiteta/Uvunjifu Katiba!

Kwa vile ni yeye ndiye aliyemteua Makonda, anaamini hakuna yoyote mwenye uwezo wa kumtoa huyo Makonda, kiukweli sio tuu Watanzania wakiamua wanaweza kumtoa huyo Makonda, bali hata yeye ampende vipi Makonda, bali Watanzania tukiamua kwa kauli moja kuwa hatumtaki Makonda kwa sababu za msingi ambazo ni justifiable, sio tuu tunamtoa huyo Makonda wake, bali tunauwezo wa kumtoa hata yeye Magufuli na Makonda wake kwa mujibu wa katiba mradi tuu ziwepo sababu za msingi.

Sababu ya msingi ya kumtoa Makonda, ni iwapo ikithibitika kuwa ni kweli jina halisi la Makonda ni Daudi Bashite, ni kweli alifoji vyeti na akafanya udanganyifu kwa kutumia vyeti vya Paul Chistian kujipatia elimu, ajira hadi uteuzi, then kwa kutumia vipengele fulani vya kisheria, kwa kupeleka shauri mahakamani, then Mahakama inamlazimisha rais Magufuli kutengua uteuzi wa Makonda kwa lazima kwa kutumia nguvu za kisheia, hata Magufuli ampende vipi Makonda ni lazima amtengue!.

Kitu ambapo Magufuli anaweza kukifanya kumuokoa Makonda wake, kwa vile anampenda sana kwa uchapa kazi wake, na rais anayo kinga ya kutokushitakiwa, anaweza kummegea kidogo Makonda hiyo kinga yake ya kutokushitakiwa, hivyo kumkingia kushitakiwa kwa jinai ya kufoji na kufanya udanganyifu, lakini jina la wizi lazima livuliwe hivyo lazima atengue uteuzi wa Paul Makonda kama RC wa Da es Salaam na papo hapo kumteua Daudi Albet Bashite kuwa mkuu mpya wa mkoa wa Da es Salaam na kuendelea kuchapa kazi.

Nawaomba mnipe muda niwatafutie vifungu vya katiba na sheria vinavyoonyesha kuwa rais sio kila kitu bali katiba ndio kila kitu, na rais anaweza kufanya maamuzi fulani na mahakama ikayatengua maamuzi hayo kwa kutumia vipengele vinavyoitwa writs or prerogative ordes kama prohibition, certiorari, mandamus, harbea copus na quo warranto ambapo rais analazimishwa kufanya kitu fulani kwa lazima, apende au asipende na akigoma, Bunge linaitishwa na kumfukuza kazi!. Hili lipo, sheria hizi zipo, ila sisi hapa Tanzania hatujawahi kuitumia, lakini anamuondoa madarakani mteule yoyote wa rais hata rais ampende vipi. Kwa vile sheria zetu tumezirithi kutoka India Para materiale, kuna sheria nyingi tunazo lakini hatujazitumia, kwa vile mimi sio practicing lawyer, kuna sheria zipo tuu kama just persuasive tuu, with time tutawathibitishia kuwa rais Magufuli sio kila kitu, bali katiba ndio kila kitu!.
Kuna mtu alifukuzwa kazi na rais, mahakama ikaamuru arudi kazini.
Kuna mtu alitiwa kizuizini kwa amri ya rais, mahakama ikamtoa.
Kuna ile kesi ya Bawata etc.

NB. Katiba yetu imempa rais wetu mamlaka ya kuwa kila kitu endapo tuu atatangaza hali ya hatari, hili likifanyika, hapo ni kweli rais ndio anakuwa kila kitu maana katiba huwekwa pembeni!.

Kuna vitu kibao rais wetu Magufuli alitangaza kuwa atafanya, wakati akitangaza, yeye alitangaza kwa mamlaka kabisa akijidhania anao uwezo huo, au mamlaka hayo lakini kiukweli kabisa, kuna vitu rais anatangaza kuwa anao uwezo lakini hana uwezo huo na mifano
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote

Rais amefanya mambo mengi tuu kinyume cha katiba lakini kwa vile amefanya kwa nia njema, hakuna aliyelalamika.

Udikiteta ni Dhana Tuu or ni Real?. "Lets Call A Spade A Spade!"Dikiteta ni Mtu Mwenye Tabia Hizi!".

Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria, ongoza kwa 'presidential decrees'!
Paskali

Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki 'Separation of Powers'?

Watetezi Wa Kweli wa Haki za Binaadamu Tanzania ni Kina Nani?!, Jee JF Tumo?!.

Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The Right Time, And Doing It Right, Or ?!

Udikiteta: Uongo Ukisemwa Sana na Kuachwa Bila Kukanushwa Hugeuka Ukweli!. Dawa ya Uongo ni Ukweli.

Je, Rais wetu, Magufuli anasoma JF? Rais, Please msikilize Binti huyu, ana hoja ya Msingi!

Kutoonyesha Hisia/Huruma wala pole za sauti si Udikteta bali ni Ushujaa wa Kijeshi!

Mawaziri Watakaolalamikia OC Ndogo!, Waache Kazi!. Ni Kauli ya Kujenga Nidhamu au Udikiteta Tuu?!.

Nimetishwa, Kushitushwa na Kuogopeshwa na Kauli Hii ya Rais Magufuli!, Alimaanisha Nini?!.

Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?

Paskali
Mkuu hao unaosema wanaelewa lakini hawazungumzi wamerudi kwenye ule utamaduni wetu, "the culture of silence and fear." Ni ule wakati wa kuwaita wale wenye mawazo tofauti na wewe kuwa wana mawazo ya kufugwa. Tunaambiwa tuongee tu mambo yanayoleta sembe kwenye sahani. Lakini hao wanaosema hivyo sidhani kama wana tatizo na kuongea mambo ya simba na yanga au manchester na arsenal ila ni yale yasiyowapendeza watawala tu. Kuvunja sheria na katiba? Julius Ceasar alisema hivi; "If you must break the law do it to seize power; in all other cases observe it." Hapo mtu unaweza kujiongeza na kuondoa neno "seize" na badala yake ukaweka "consolidate"
 
Mkuu maisha ya binadamu siyo kushiba tu. Wakati mwingine watu wako radhi hata kufa kwa njaa ili mradi haki itendeke

Haki huanzia kwenye Familia, maisha yetu yenyewe hakuna haki kwenye familia zetu sasa kusema unatafuta haki kwenye nchi ni kujidanganya, kwani huyo anayekwambia anakutafutia haki yeye mwenyewe anakuibia, rejea Tundu Lisu aligoma kuondolewa kwa posho za Ubunge alitaka Wabunge walipwe Milioni 300 kwa kuwa kwa maneno yake Tundu Lisu kwamba ana madeni na hivyo anahitaji hizo fedha kulipia madeni, kwa maana nyingine anataka fedha za walipa kodi zimlipie madeni yake binafsi, hivyo mwisho wa siku ni kudanganyana na kupeana ulaji tu, haki huanzia nyumbani kwenye familia, haiwezekani watoto wanakula ugali Maharage kila siku lkn wewe Baba/Mama unakula Nyama choma ukirudi unalala tu, hiyo siyo haki na karibia Watanzania wote hufanya hivyo!!
 
Hakuna kitu kama Watawala wa Kiafrika Dunia hii, bali kuna Waafrika ambao huja kuwa Watawala, hivyo kwa kifupi hakuna tofauti kati ya Mtawala na Mtawaliwa kwani wote wawili ni wamoja tofauti tu mmoja ana cheo mwingine hana, laiti yule asiye na Cheo ukimpa Cheo atafanya yale yale ambayo yule mwenye Cheo anafanya!
Na ndiyo maana tunapoteza muda kujadili mambo ambayo hayatusadii, hivyo hata sisi tukiwa Watawala tutendelea na yale yale ya akina Nape, Zito &Co. mipasho, unafiki na Majungu tu na hakuna jipya!

Labda wewe kwa kuwa unazo akili kama za Mwenyekiti wako wa Chama Cha Majipu.Wengine tunatambau wajibu wa RAIS.Pole sana Mzuka wa Dompo
 
Nchi hii tuna kila kitu isipokuwa watu tu wa kuishi hapana kutumia rasilimali tulizobarikiwa nazo ndiyo hatuna!
Nchi hii ina watu wachache lakini vitu vingi maana kuna mwimbaji wa kibongo alisema kuna watu na miti hasa humu JF kumejaa miti zaidi ya watu. kama unataka kuwakosoa wanasiasa wao wawe wa upinzani ama wa CCM andika kidhungu kama hutaki matusi na watu hao hao vidomo domo kumsema rais wao hajui kiingereza wao hawawezi hata kujibu hoja moja ndogo ya kiingereza. Maana udaku mwigi hauna ladha ama ufinyu wa vocabulary kwa kiingereza. Ndiyo Tanzania hii.. Me say
 
Hii nguvu tunayoitumia kwenye hili swala la Makonda tungeiwekeza kwenye Kilimo leo hii tungekuwa na foodbasket wa Dunia, au hata tu kwenye kupigania Rasilimali zetu zinazopokwa kila uchawao na wageni!

Sisi Waafrika ni watu wavivu sana!
Nani kakwambia tunatumia nguvu wakati vitu viko wazi namna hii! Kama unafikiri tunatumia nguvu basi wewe utakuwa na ubongo wa panzi!!
 
Labda wewe kwa kuwa unazo akili kama za Mwenyekiti wako wa Chama Cha Majipu.Wengine tunatambau wajibu wa RAIS.Pole sana Mzuka wa Dompo

Ni vizuri kujifurahisha na kujipa Moyo lkn mwisho wa siku hakuna Jipya, ni majungu tu ya akina Zito Kabwe, Tundu Lisu &Co. Dunia inajua hivyo kwamba Afrika yetu hakuna jipya na ndiyo maana hakuna African community diaspora iliyofanikiwa na kuwa mfano wa kuigwa, kama jamii nyingine kama vile Wachina, au hata Wahindi Dunia nzima kuna China town na kila mtu hupenda kwenda lkn kama Waafrika tukijenga Afrika town New York hakuna mtu atakuja pamoja na sisi Waafrika wenyewe!
 
Back
Top Bottom