Chief Isike
JF-Expert Member
- Jan 17, 2010
- 445
- 462
Wakuu leo nilihudhuria katika mkutano wa CCM uliofanyika Mkoa wa Dar, Wilaya ya Kinondoni, Jimbo la Kawe, hapo Tegeta Sokoni. Mgeni rasmi mwanzoni baadhi yetu tuliambiwa ni W. Mkama (tulidanganywa? Ili kujaza watu?) kumbe alikuwa ni Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, Mwigulu Lameck Mwichemba. Huyu bwana pia ni mbunge wa Iramba Magharibi nafikiri kama sijakosea. Leo ndo nimesikia kumbe alikuwa mfanyakazi wa Benki Kuu (BoT) (???????), kabla hajaenda kugombea na kuukwaa ubunge na ukatibu huo wa NEC.
Nilikuwa na siku nyingi kidogo, du! Watoto bado wanatumikishwa, wamevalishwa maskini nguo haziwaenei. Kubwa si kubwa, ndogo si ndogo. Wamekalilishwa na kulishwa maneno! Walipomaliza kuimba, jamaa Mwigulu nikaona kampatia mmoja wao, kiongozi sijui, shilingi elfu kumi kadhaa hivi mkononi, akiwa amezifunga funga! Posho ya siku kwa kukaa juani masaa kadhaa! Maneno kama wakereketwa sijayasikia kitambo, leo nikayasikia. Nisiwachoshe, msinichoshe pia!
Katika upupu aliomwaga huyo jamaa, (maana yeye na Shigela walitumia sana nafasi hiyo kuwananga wapinzani, hasa CHADEMA, Mbunge Halima Mdee, Dkt. W.P Slaa na Freeman Mbowe) huu ulivuka mipaka ya vijembe vya kisiasa bali ulikuwa ni uongo uliokubuhu. Halafu jamaa hata aibu hana kabisa. Hoja za Jamaa na Shigela zinasema hivi;
1. Dkt. Slaa alifukuzwa upadri kwa sababu alimpatia mimba sister mmoja. Hana analojua, maana ni Dokta wa Sheria za Kanisa, akisisitiza neno Padri, kwa makusudi wanayoyajua wao Chama Cha Magamba. Hata kazi hiyo aliyoisomea na kupata udaktari wa sheria za kanisa bado hakuweza kufanya kazi muda mrefu, maana alifukuzwa punde tu alipoanza kufanya kazi! Wakuu du!
2.Juzi wakati akichangia bungeni Freeman Mbowe atakuwa alikuwa amepandwa na Malaria, maana alisema kuwa ukosefu wa maji uliosababisha ukosefu wa umeme si janga la asili. Kwa hiyo si kiongozi wa kuaminika wala kusikilizwa maana uelewa wke ni mdogo hata hajui kuwa kukosekana kwa mvua/ maji ni janga linalotokana na asili, nje ya uwezo wa binaamu.
(Jamani kwa wale tuliomsikiliza kwa makini juzi Mkuu wa Kambi yetu rasmi ya Upinzani bungeni alipiga nondo za uhakika. Mbowe alisema serikali isiseme wala kusingizia kuwa matatizo ya umeme ni janga (si maji, aki-refer kauli ya Ngeleja kuwa umeme ni janga la taifa sasa), kwa sababu majanga husababishwa na natural calamities, nje ya uwezo wa binadamu, lakini matatizo ya umeme nchini yamesababishwa na binadamu ambayo ni matokeo ya uongozi mbovu), jamaa bila aibu akabadili, du! Nikaona watu wenye mavazi ya kijani na weusi wakishangilia. Wakaitikia sema baba ukweli! Nikasikitika.
3. Halima Mdee hana muda na wananchi wake, kwa sababu muda wote yuko katika maandamano. Hawezi kuwaletea maendeleo, wala kuwanunulia hata pipi. Hana uwezo wa kujenga hata uchochoro kwa sababu inabidi akaombe msaada serikali ya CCM.
4. CDM hawafanyi maandamano 'kwao', ndiyo maana huwezi kusikia maandamano Karatu wala Kilimanjaro kwa akina Mbowe kwa sababu wenzenu hawataki hata kuona risasi zikigusa migomba na kahawa zao, wanaletea ninyi huku, mnapigwa tu risasi.
5. CDM wanafuja fedha za wananchi kufanya maandamano. Akina Lema na Mdee na wengine badala ya kupeleka maendeleo, kucha wanazungumza mambo yasiyokuwa na maana hata bungeni. 'Nimewauliza Arusha kama wameletewa hata pipi, hakuna, wakati kwangu mimi Iramba nimepeleka mifuko ya sementi, nimesomesha wanafunzi wote waliokwenda form five, nimelpia ada wanafunzi na nimepeleka madawati, ninyi hapa mmepata nini, huko sasa wananiiita Baba wa Taifa wa Iramba.'.
Zilikuwepo hoja nyingi za uongo wa wazi na vijembe vya hovyo kbs kufanywa na mwanasiasa wa level ya washikaji kama Shigela na Mwigulu. Nitazidi kuziweka kadri mjadala utakavyokwenda!