Uchaguzi 2020 Mkutano Mkuu wa CCM 2020 wamchagua John Magufuli kuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Amteua Samia Suluhu kuwa Mgombea Mwenza

Nilikosea ni Jim Brown hivi huyu. Ni ndugu yako,? Sisi tunamwita Truck turner? Tusalimie Bashite na Kardinali wako pengo

Tatizo lako hutaki mjadala wenye afya....nimeshafafanua mengi tena vya kutosha,lakini kwa kuwa "unapigana jihadi isiyoeleweka" inakufanya utamalaki na ARGUMENTUM AD HOMINEM....Umekuwa ukipotosha hata KUHUSU asili yangu......Basi endelea kufika "orgasm" kwa KUPWAGAPWAGA maneno......
 
Kuna mtu ambaye ni miongoni mwa walio hesabu kura, anasema matokeo yalikua mazuri lakini sio 100% .

Kilicho fanyika ni uungwana tuu na myangaza matokeo nadhani alikua na ujumbe toka juu kwamba kura zote zisomeke ndio.

Anasema matokeo kuwa mazuri japo siyo 100% yamechangiwa na mkakati ambao uliwekwa kuhesabu kura kwa mikoa ili kubaini mkoa upi upiga hapana.

Bahati mbaya moja ya mkoa ambao ulikua na hapana ni mkoa ulio karibu sana na muhusika.

Makubaliano hayo ya kutangaza 100% ambayo anasema hata nyerere hakuwahi kupata ni kuanza kwa kampeni za propaganda kwamba anakubalika na watanzania wote.

Na mtoa nyeti anasema, hata oct 25 anaweza jichukulia 100%, na hakuna waku uliza.

Moja ya jambo ambalo mtoa nyeti ameligusia ni mkakati wa kuto toa kopi ya matokeo, maana yake vituo vitakua na kopi moja tuu ya matokeo.

Mungu ibariki Tanzania, la msingi Barabara zinajengwa, na zahanati zinajengwa.

View attachment 1503805
Hii Ndiyo Raha ya kuwepo mawazo mbadara (upinzani)

Uzushi na uzandiki uko siasani, Kesho tukutane Church ama Masjid Ijumaa ili kutubia huu uwongo wa kizembe
 
Hana sifa ya kushinda kwa box la kura toka zamani. Na hilo la kuwa na fomu moja ya matokeo General Election ni agizo lake. Unaposikia atashinda kwa 90%+ ujue hayo ni maagizo yake. Na kuna misukumo mikubwa ya kutaka wapinzani wasishindane na yeye ili apite bila kupingwa. Na iwapo wapinzani watakaza kamba tutarajie damu kumwagika, na uchaguzi wa kishenzi kuwahi kutokea hapa nchini.
Mkuu, utaratibu huu WA hawa Jamaa CCM ndio umeanza mwaka huu wa kuwa na mchukua fomu ya Uraisi mmoja tu ambapo mgombea hajakamilisha vipindi vyake viwili, binafs sikumbuki kama kumewahi Kutokea kushindanishwa na mgombea mwingine Kwa anayeendelea hajakamilisha awamu zake 2
 
Mkuu, utaratibu huu WA hawa Jamaa CCM ndio umeanza mwaka huu wa kuwa na mchukua fomu ya Uraisi mmoja tu ambapo mgombea hajakamilisha vipindi vyake viwili, binafs sikumbuki kama kumewahi Kutokea kushindanishwa na mgombea mwingine Kwa anayeendelea hajakamilisha awamu zake 2

Kutokana na sifa za ccm ya awamu hii, ni kuwa ccm hii ni mpya na haifanyi mambo yake kwa mazoea. Na kama ulimsikia Bashiru leo akiongea, anasema walitarajia kuwe na wagombea watatu safari hii, lakini watu hawakujitokeza kuchukua fomu. Sasa ili na ww uwe unacheza vizuri na upepo, tafuta uje na hoja ipi ya utetezi kati ya hizo. Kinyume na hapo utachekesha hapa.
 
Kutokana na sifa za ccm ya awamu hii, ni kuwa ccm hii ni mpya na haifanyi mambo yake kwa mazoea. Na kama ulimsikia Bashiru leo akiongea, anasema walitarajia kuwe na wagombea watatu safari hii, lakini watu hawakujitokeza kuchukua fomu. Sasa ili na ww uwe unacheza vizuri na upepo, tafuta uje na hoja ipi ya utetezi kati ya hizo. Kinyume na hapo utachekesha hapa.
Sasa wewe unabisha nini mkuu? Je, kuna mtu alienda kucbukua form akanyimwa?

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
 
Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Jumamosi, Julai 11, 2020 jijini Dodoma, Wajumbe 1,846 wanatarajiwa kushiriki. Mkutano huo unongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli.

AJENDA:
1. Kufungua Mkutano

2. Marekebisho ya Katiba ya CCM ya Mwaka 1977, Toleo la 2017

3. Taarifa za Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015-2020 za SMZ, SMT na CCM

4. Uteuzi wa Mgombea wa CCM wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

5. Kufunga Mkutano.






UPDATES

Mkutano Mkuu wa CCM unafanyika leo tarehe 11 Julai 2020 ukiwa na lengo kuu la kumpitisha mgombea wa Urais wa JMT.

Mkutano umehudhuriwa na wanachama 1,822 huku wanachama waliokosekana wakiwa 23 sawa na 1% hivyo uko sahihi kikatiba na ajenda zinaweza kujadiliwa.

Katika hotuba yake, Rais Magufuli kama mwenyekiti wa mkutano huo, amewashukuru viongozi wa upinzani waliohudhuria katika mkutano huo

Amemshukuru Lyatonga Mrema, mwenyekiti wa TLP kwa kauli yake ya kusema TLP haina mgombea bali itamuunga mkono mgombea wa CCM

Rais Magufuli:

Mambo yaliyofanyika ni mengi, kila mmoja ni shahidi, hata Viongozi wa Vyama vya upinzani wanafahamu mazuri yaliyofanyika hata Nchi jirani wanafahamu, Ndege 11 kununuliwa kwa mpigo tena kwa cash, Elimu bure,Barabara,vituo vya Afya nyinyi wote ni mashahidi

Tumeipeleka Nchi kwenye uchumi wa kati, tumepambana vizuri na corona na mengine mengi, tumeitengeneza Tanzania, ni mafanikio yetu wote hata ambao hawako CCM na ndio maana Mzeee Mrema mapema kabisa akasema yeye hana mgombea Urais, mgombea wake CCM maendeleo hayana chama.

Nimefurahi kuwaona Marais Wastaafu, nimefurahi kumuona Mama Anna Abdallah huyu Mama alinifundisha Kazi lakini pia alimfundisha kazi Mwinyi akiwa Naibu Waziri wa Afya, nimefurahi kumuona Mzee Kinana, Lowassa, Mzee Sumaye, Maspika Wastaafu na wote.

Nimefurahi kumuona Mzee Mwinyi Mzee wa ruhusa, nimefurahi kumuona Mzee Mkapa Mzee wa uwazi ingawa sijajua ni uwazi upi?, nimefurahi kumuona Mzee Kikwete naona mvi zimeanza uzee unamuwinda, hii ndio Tanzania, nimefurahi kumuona Dr.Bashiru, Mzee Mangula n.k


Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Mhe. Augustino Mrema:

May 04, 2019 sisi TLP tulikaa tukajadili nani atuongoze, H/Kuu TLP ikasema hatuna mbadala wa Magufuli tukasema Magufuli anatosha, tukakutana tena May 08,2020 kura zote zikamuangukia Magufuli

TLP tumesema wewe Magufuli unatosha, tutafanya kampeni Nchi nzima kuhahakisha unachaguliwa tena, ombi langu kwenu CCM tujipange kuhakikisha kwenye Kata na Majimbo yote kuna mgombea wa TLP na CCM, tusing’ang’anie jimbo moja Watu wa CCM 30 ni matumizi mabaya ya rasilimali Watu

Baada ya May 08,2020 Halmashauri Kuu TLP kusema Magufuli anatosha kuwa mgombea wetu, May 09,2020 tukamuita Polepole aje, tukamualika na Msajili aje ashuhudie kuwa kikao cha TLP hakikuwa cha Magumashi na hapo tukapiga kura kisha wote wakasema tena wanamtaka rais Magufuli


Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF

Amesema chama chao katika uchaguzi wa 2020 kinakuja na agenda ya “Furaha kwa Watanzania inawezekana”

Pia Professa Lipumba amewaomba CCM kuwa na siasa za ustaarabu kitapoanza kipindi cha kampeni akisisitiza kupambana kwa hoja


Mzee Kinana

Amewaomba Wajumbe mkutano mkuu wampe mgombea kura zote bila kuharibika bila hapana ili apate nguvu kuliongoza taifa letu.

Amewasihi Wanaccm kufanya kazi kwa bidii kwa kujitolea kutafuta kura za Rais, Wabunge na madiwani. Hakuna uchaguzi rahisi.

Kuna Watia nia na ubunge wengi sana, kuna jimbo la Rorya watia nia wako 60, nawaomba hatimaye watamteua mgombea mmoja wa CCM hivyo wasigawane kura.


Mzee Mwinyi

Nawaomba wenzangu tumekutana hapa na wanatanzania nzima pamoja na wapinzani. Sote tumeshuhudia kuwa mgombea Rais wetu tuliye naye ameshika madaraka kasoro miaka mitatu kama mambo mengi, ya ajabu kama kununua ndege 11. Sijawahi kuona nchi inayosemwa haina pesa inanunua ndege 11 kwa pesa za ndani. Hakika Rais Magufuli amefanya mambo ya ajabu katika sekta zote ikiwemo Umeme na SGR.

Tumekaa miaka mingi na uwezekano wa kupata umeme lakini Rais wetu kalishugulikia suala la umeme kwa kujenga Stiegler's Gorge na karibu tunakuwa mabepari wa umeme.

Nchi yetu inaendeshwa kwa Katiba lazima tuienzi, , tusiingilie lakini tunaweza kuiahirisha kwa muda mfupi ili kumpa Rais wetu kipindi kingine kimoja cha asante. Hichi ni asante na kisha tuendelee vile vile mpaka dunia iishe. Hiki ni maalum kwasababu ana mengi nchi itayakosa.

Rais Magufuli akimjibu Mwinyi kuhusu kuongezewa kipindi kingine

Mbona wewe (Mzee Mwinyi) hukuongeza muda baada ya kumaliza? Au mzee Mkapa hakuongeza? au Mzee Kikwete hakuongeza? Ila nimekuelewa Mzee Mwinyi wewe ni mtani wangu.


Agenda: Uteuzi wa Mgombea Urais kupitia CCM

Rais Magufuli amejivua Uenyekiti ili aweze kupigiwa kura, Uenyekiti umekaimishwa kwa Mzee Sheini.


RAIS MAGUFULI APITISHWA KUWA MGOMBEA WA CCM KWA 100% YA KURA ZA WAJUMBE

Msimamizi wa Uchaguzi, Spika Ndugai anasoma...

Wajumbe walohudhuria ni 1822

Kura zilizopigwa ni 1822

Hakuna kura iliyoharibika kura halali ni 1822. Kura za ndiyo ni kura 1822 sawa na asilimia 100.

Rais John Pombe Magufuli ameteuliwa na CCM kuwa mgombea wa Urais kwa mwaka wa uchaguzi 2020

Kwa kura 1822 zilizopigwa na wajumbe wa kamati kuu, Rais Magufuli amepata kura 1822 ya kura za ndio

Awali katibu mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally alisema, ilibidi wawe na wagombea watatu lakini hakukuwa na mgombea aliyejitokeza kuchukua fomu ya kugombea urais

Hali hiyo ilimfanya Rais Magufuli awe mtu pekee aliyechukua fomu ya kugombea Urais kupitia CCM


Hussein Mwinyi

Nimefanya kazi na Marais watatu ambao ni Mkapa, Kikwete na Magufuli. Ninawashukuru wote kwa kunielekeza lakini kuna Rais ambaye Mstaafu ambaye sijafanya kazi nae ila ndio Mzazi wangu Mzee Mwinyi, amenilea, kama nina tabia njema basi ni malezi yake, namshukuru Mama yangu Mama Sitti tuko nae hapa, mchakato wa Urais umefanya nipungue uzito ila Mama yangu amepungua zaidi.

Namshukuru Mzee Mkapa nikiwa Kijana wa miaka 33 (Mbunge wa Mkuranga) aliniteua kuwa Naibu Waziri Afya,Mzee Mkapa ulinifungulia njia, namshukuru Mstaafu Kikwete katika utawala wake wa miaka 10 yote nilikuwa Waziri, namshukuru JPM pia kwa kuniamini na kunipa Uwaziri.

Katika miaka mitano ya kufanya kazi na wewe, nimejifunza mengi kwako Rais Magufuli . Wapo waliosema mimi ni mpole lakini nimejifunza kuna mambo yanataka uwe mkali, mfano rushwa, uzembe na ubadhirifu, nikichaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar nitakuja na style ya Rais Magufuli katika maeneo hayo.


Hotuba ya Dkt. Magufuli (Kwa ufupi)

Namuomba Mwenyenzi Mungu anisaidie kura nilizozipata leo zisinipe kiburi, zisinifanye nijione mimi nafaa sana, bali zikanifanye nikawahudumie Watanzania wote bila kubagua dini zao, makabila na vyama vyao. Ninafahamu kazi hii inahitaji msaada wa Mungu. Kura nilizopata leo zikawe salamu kwa wasaidizi wangu kuwa wana kazi ya kutimiza shauku ya wanachama na wananchi wote, hivyo tukashirikiane kuijenga nchi yetu hii tajiri

Niwaombe Watanzania mkazidi kuniombea ili nikafanye yale mnayoyataka. Wajumbe mmenipa kura kwa 100%, lakini kamwe msitoke hapa mkiamini kuwa tunakwenda kushinda kwa 100%.

Mara nyingi sisi CCM tunapoteza majimbo kwa sababu ya mfarakano ndani yetu. Anapitishwa mtu ambaye hamumtaki halafu mwisho mnashindwa. Wagombea Zanzibar wameonesha mfano mzuri wapo 31 ameshinda mmoja wengine wamekubali, wanamuunga mkono na nina uhakika watazunguka kwenye kampeni kuhakikisha Mwinyi anashinda

Hussein Mwinyi ni tofauti sana na watoto wa wakubwa. Mwinyi [Dkt. Hussein] hakuubeba Urais wa baba yake [Rais Ali Hassan Mwinyi]. Hussein Mwinyi amezaliwa mwaka 1966, mimi nimezaliwa mwaka 1955, mumchague yeye. Msinichagulie mtu ambaye kila siku nitakuwa nasema shikamoo, shikamoo. Mimi ni Rais wa Tanzania, nikija kule (Zanzibar) nianze kusema Shikamoo muheshimiwa Rais, inakera

Nilimteua kuwa Waziri wa Ulinzi. Waziri ambaye unamkabidhi majeshi yote ni lazima uwe unamuamini sana. Nitamshangaa mtu atakayesema Mwinyi hatoshi. Amesimamia mabomu yote na mizinga ashindwe kutawala Zanzibar?

Wanasema tumechagua Masultan. Mwinyi ndio amegombea kwa mara ya kwanza, sasa kati ya yeye na wale wengine kila mwaka ni wao tu nani Sultani? Hussein ni mnyenyekevu, hajaubeba Urais wa Baba yake na mmeona wakati anashukuru hapa hajaanza kumshukuru Baba yake, kamshukuru Mkapa, Kikwete kisha kanishukuru mimi ndio akamaliza na Baba yake.

Nilipomteua Mama Samia kuwa Makamu wa Rais mwaka 2015 sikuujua utendaji kazi wake vizuri lakini ni mchapakazi, anajituma pia ni mzuri, Wasukuma tunapenda weupe, ukiwa na Msaidizi mweupe hata ukiwa na stress zinaisha, nimeamua awe tena Mgombea mwenza wangu

Katika kipindi nilichofanya kazi na Samia nimejifunza mambo mengi sana na kupitia yeye nawahikikishia nitakuwa mtetezi mzuri wa wanawake. Nimekuwa nikimtuma popote hakatai kama na nyie kina Mama mkitumwa hamkatai.

Kwenye uongozi hakuna Urafiki unatanguliza maslahi mapana ya Taifa, Kikwete aliwatwanga Rafiki zake akaniteua, Mkapa aliwatwanga Rafiki zake akamteua Kikwete, Mwinyi na Nyerere hivyo hivyo, Wastaafu wakiona nimefukuza Rafiki zangu kwenye kazi ni kwasababu nimejifunza kwao

Niseme wazi hapa japo sikutakiwa kusema, lakini ukweli ni kwamba mwaka 2015 nilikuwa nimependekeza Hussein Mwinyi na Mama Samia mmoja wao awe Mgombea mwenza, Mama Samia akapita. Mwinyi namwamini sana.

Nitoe wito kwa Vyama vya siasa tusiwe na Wagombea haohao, tubadilishe Sample, sio kila siku Watu walewale, Mungu hajakuumba wewe tu kwamba uwe Kiongozi kila siku, tuwaachie wengine, Mzee Kikwete angeweza kuendelea kuwa Mwenyekiti ila aliniachia na waliotangulia hivyo hivyo,

1594492991880.png


Nafasi za WALIONUNULIWA zilikuwepo...Waliwatenga
 
Na Emmanuel J. Shilatu

Napenda niungane na Mamilioni ya Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Watanzania kwa ujumla kumpongeza Mwenyekiti CCM Taifa na Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuandika historia ya aina yake kwenye mkutano Mkuu wa CCM Taifa uliofanyika leo Julai 11, 2020 mjini Dodoma.

Kwanza, Dkt. Magufuli amethibitishwa kwa kupigwa kura ya ndio na Wajumbe 1822 wote sawa na asilimia 100 kupeperusha bendera ya CCM kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka huu utakaofanyika mwezi Oktoba, 2020.

Haijawahi kutokea katika historia ya miaka yote ndani ya CCM Mgombea kwa nafasi ya Urais kupitishwa kwa asilimia 100. Mwaka 2015 Dkt. Magufuli alipitishwa kwa asilimia 87. Ongezeko hili ni ishara ya kubaliko la uadilifu, uzalendo, ufuatiliaji, uchapa kazi, ukweli na ucha Mungu alionao Dk. Magufuli kiuongozi.

Pili, Dk. Magufuli akiwa Mwenyekiti wa Kikao amewadhihirishia Watanzania na Dunia kwa ujumla juu ya Demokrasia iliyokomaa, uwazi na Uhuru wa uchaguzi ndani ya CCM kwa kura kupigwa wazi wazi na kuhesabiwa wazi wazi tena ikionyeshwa mubashara (live) na vyombo vya habari. Hii rekodi ameivunja na haijawahi kutokea katika historia ya Miaka yote ya chaguzi za CCM kwenye nafasi ya kumpata Mgombea Urais.

Hakika, Dk. Magufuli alivyosema uchaguzi wa mwaka huu atahakikisha unakuwa wa huru na haki alimaanisha na anaonyesha kivitendo kuanzia ndani nyumbani kwake (CCM).

Narudia tena kusema historia aliyoiandika Dkt. Magufuli ni ya aina yake inayompambanua kivitendo kuwa Mwamba na mkufunzi wa Dunia juu ya siasa safi, Demokrasia ya kweli na Uhuru wa uchaguzi.

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki CCM
Mungu Mbariki Dk. Magufuli

*Shilatu E.J*
 
Mtapinga sana lakini -Chanda chema huvikwa pete. Rais amefanya mengi makubwa.Hii ni ishara tosha kwenye uchaguzi wa oktoba si chini ya asilimia 98. Mtaona.Viva JPM VIVA TZ VIVA CCM. God bless our country
 
Kungekuwa na wagombea wawili au zaidi alafu angepata aslimia 💯 hapo ndio ingekuwa historia sasa.
 
Hiyo ridhaa hatuwapi ng'oo, tushawashitukia, kwanza hamjui mnataka nini! Kila siku kudandia hoja, mnasubili CCM waseme ndo nanyie mapovu yawatoke! Mawakala wakubwa wa Beberu nyie, mtasubili sana kuwaachia hii nchi. Shubamiti
Cdm haishindani kukupita chama fulani, bali cdm inasaka ridhaa ya wananchi kukaa madarakani kwa ridhaa yao. Idadi ya wabunge wanashindania vyama vilivyoamua kuwa michepuko ya ccm.
 
Back
Top Bottom