Mkutano maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa na wadau wa Demokrasia tarehe 04 Januari 2024

Bwana Buruani: Mtoa mada Taasisi ya twaweze.
Maoni na uchambuzi walioufanya kutokana na mswada huu. Hatujafanya sisi tu tumeungana na taasisi zingine. TLS, nk

Tumekuwa na muda wa kuuchambua na kuweza kutoa maoni yetu. Kuanzia kesho taasisi zetu tutaelekea Dodoma kupeleka maonia yetu.
Sitaweza kupitia mambo yote nitaongea machache tu.
 
Anaongelea mada zilizopita. Kwahiyo sitarudia kwa kina sana.
Mswada wa Sheria ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ni muhimu sana kwa miswada iliyoletwa.
Hii inaendana kabisa na 4R. Maridhiano ni muhimu sana kwenye chaguzi zetu.

Kumekuwa na migongano kwenye chaguzi zetu.
Anaendelea kuongelea 4R kuhusuana na chaguzi
 
Katika maoni tuliyonayo ni maoni ya jumla na maoni mahususi
Maoni ya jumla yapo 6 na maoni mahususi yapo 6

Inaweza kurahisisha kwa kuunganishwa. Uchaguzi wa wabunge na madiwani kuweza kuyaunganisha. Maudhui yanayofanana yaweze kuungwanishwa.

Tunapongeza kwa kuziunganisha sheria hizi mbili. Kuwa na sheria moja inayohusu uchaguzi Tanzania.

Tunapendekeza wasimamizi wa uchaguzi wawe ni watumishi wa tume
Wananchi waweze kupiga kura kwa kutumia vitambulisho vya taifa
Sheria hii iweze kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa harakaI(wagombea na wananchi) Mgeni wetu wa jana alisema msingi mkuu ni haki.
Matumizi ya teknolojia. Kipengele cha mwisho kimesema matumizi ya teknolojia. Matumiz ya teknolojia hayajitosherezi.
 
Ukisoma huu mswada wa sheria, hata kama tukiupitisha na ukawa ni bora sana. Kama hatuna tume huru ya uchaguzi.
Nini maana ya tume huru - Tume huru ni ile ambayo haifati amri ambayo inakiuka aktiba yetu. Tume huru ni ile inayofuata haki na uwajibikaji.

Kama tume yetu haina sifa ya uwajibikaji, vifungu kadha wa sheria vitaachwa
 
Mahususi
Kifungu 10. Nani anaruhusiwa kupiga kura. Mtu aliyetiwa hatiani aisiweze kupiga kura. Mtu aliyetiwa hatiani kuwa asipate haki ya kupiga kura.
Kifungu kinachoongelea kugombea urais. Mtu asizuiliwe kugombea urais kwa sababu ambazo zinawezakurekebishika. Vigezo pekee vya kumzuia mtu asigombee ziwe sababu za kikatiba pekee.

kifungu 50. Kuhusu sifa za wagombea. Tuongeze formu za kugombe kupiti mitandao. Inawezekana wahusika katika ofsi ile hawakuwepo kwenye ofsi ile. Mtu aweze kuwasilisha kupitia mtandao

Kifungu 112. Wabunge wa viti maalum. Izungumze namna ya wabunge wa vit maalu wanapatikana kwenye vyama vya siasa.
Kifungu 140: Dhamana, gharama za walalamikaji ni kubwa sana. Hakuna haja ya kuweka dhama na gharama kubwa sana.
Utaratibu mzima wa kufungua kesi na kuwasilisha malalamiko na kukata rufaa. Shauri kuweza kufunguliwa miezi 12. Shauri lfunguliwe ndani ya siku 60.
 
Deus Kibamba:
Kwakuwa ni mekuwa mwenyekiti wa jukwaa la katiba Tanzania.
Yapo mambo ambayo ambayo yanaelekea kukinzana na katiba. Kwenye katiba kumekatanzwa vizuri sana. Lakini kwenye sheri hayajakatazwa.
Mfano: Mswada huu unasema wasimamizi wa uchaguzi wapo makundi matatu
Kifungu cha Wakurugenzi (Tume inaweza kuteua)
6(2) Tume inaweza kuteua watumishi wa umma. Inawezekana tume ikateua watumishi wengine wa umma. Ikitokea ameteuliwa mwingine mkurugenzi atakoma.
Tume inaweza kumteua mtu mwingine ambaye siyo mtumishi wa umma.

Suala la TEHAMA ambalo limezungumzwa kwa kupita pita tu. Mswada huu ungesistiza kwenye kifungu 166. Uchaguzi ni mchakato. Kwa maoni yangu mswada huu useme kila patakapo wezekana TEHAMA itumike. Vijana hawataki aache bodaboda yake aende akajiandikishe. Tume iaandae App ili watu wajiandikishe. Tume utaisubiri masaa kadha.
Utapunguza idadi ya watu. Watu wengi hawajiandikishi kwa sababu wana watoto wengi.

Mambo yale ya wagombea kusema wameenguliwa. Je, si tunaweza kutuma kwa mtandao tu. Hard copy inatumwa hata nje ya muda.
Kuhusu sheria hii imabadilisha jina la sheria. Itakuwa ndio sheria itakuwa inashughulikia uchaguzi. Hii inatakiwa iitwe Sheria ya Uchaguzi Tanzania.
Sheria hii haitashughulikia haitaweza kushughulikia uchaguzi wa srikali za mitaa.
Huu ni mwanzo mzuri.
Huko mtaani watu wanahamu.
Watu mtaani wanasema dafatari la wapiga kura lipelekwe TAMISEMI
 
Mrisho:
Kuna mambo mawili ya haraka ningependa kuyazungumzia. Dhana na madhumuni ya mswada uliowasilishwa. Kama alivyosema Baruani. Sheria hii ni ndefu sana. Maeneo yanayofanana yaunganishwe.

Suala nililoliona ni kupunguza wagombea wanaopita bila kupingwa. Lazima wananchi wapige kura kwa kukubali au kukataa.

Eneo ambalo Baruani kazingumza jinsi ya kushirikisha wadau mbalimbali kupata haki zao kwa wakati na gharama himilivu.
 
Idda:
NItazungumza kwa kifupi mambo matatu.
Suala ya uchaguzi wa serikali za mitaa kusimamiwa na tume ya uchaguzi. Kwa Tanzania chaguzi hizi zimetofautishwa. Shida ya kuunganiswa. Hatuta wapa haki wananchi kusikiliza sera.

Napendekeza ziainishwe changamoto za serikali za mtaa ili zifanyiwe kazi. Kisha yatolewe maoni namna tume itkavyofanya kazi.

Mpiga kura aweze kupiga kura sehemu yoyote. Tuweze kutumia TEHAMA. Mtu anaweza kupiga kura kokote alipo. Litasaidia sana.

Kipengere kinachozungumiza makosa na adhabu. Kifungu hiki nimekipenda.
 
Said Sudi Mwenyekiti FP
Mambo yote yote tunayoyajadili hapa Roho yake ni Katiba.
Bila kuwa na katiba hakuna cha sheria. Kwa mfano si vibaya mtu kwa kujiandikisha kwa kupiga simu. Ki msingi ni kuheshimu katiba. Ikifika wakati wa UChaguzi, Tume inazidiwa nguvu na polisi. Mimi naunga mkono tume ya uchaguzi iweze kuajiri watumishi wa kudumu.
 
Zitto Kabwe:
Kifungu 6
Ukisikia maelezo ya Deus unaweza ukalainika. Kifungu kimewataja wakurugenzi kama kwa lazima.
Kimelazimisha kuwa mkurugenzi shall.
Napendekeza kifungu kisomeke ..... Tume itatetua ................
6(2) Kwa kuzingatiwa kifungu cha kwanza tume inaweza ......

kiongeze kifungu cha 6(4) Kitakachotaja sifa za wasimamizi wa uchaguzi
 
Mwenyekti UWT
Sheria itamke mgombea kuwa kiti cha rais mgombea urais akiwa jinsia nyingine makamu awe jinsia nyingine.
Ilikuipa meno tume ya uchaguzi sheria iseme anagalau 20% ya watakaoteuliwa kwenye uchaguzi wa wabunge wawe wanawake.
Kosa kuhusu ukatili wa kijinsia. Katika makosa yanayoelekea kupoteza kuwa na haki ya kugombea ni unyanyasaji wa kijinsia.
Sheria iweke utaratibu wa kupata wabunge wa viti maalum
 
Adv Paskal Mayalla
Hoja zangu ni nne:
Sheria yetu ya uchaguzi naomba ifuate katiba ya Tanzania. Katiba ya Tanzana imetoa haki kwa kila raia wa tanzania kuchagua kiongozi.
Katiba imetoa haki kwa mtanzania yoyote kugombea. Hapo katikati ibara ya 21 ikachokwa kitu kingine. Eti ikiwa mtu anataka kuchaguliwa lazima awe kwenye chama cha siasa.

Tume inatakiwa iitwe Tume huru na shirikishi.
Zanzibar wanafanya chaguzi tano kwa siku moja. Na sisi tunaweza kuungani chaguzi zote kwa pamoja kwa siku moja.
Utumishi wa vyama ni kujitolea. Kwanini tuvipe ruzuku vyama vya siasa. Ukifika kama Zaire kuna vyama zaidi 500.
Fedha za nchi sio za kugharamia vyama.
 
Majjid Mjengwa:
Jana nilikuwepo hapa nilimsikiliza sana makamu wa kwanza wa rais Zanzibar.
Keyword aliongelea kuhusu reforms. Hii ndiyo key kwenye 4R.
Nimewaona waandishi hapa Paskal Mayala na Manyerere.

Machakato wa kidemokrasia na ni wakuendelea. Tumewaona hapa Lipumba, Cheyo. Hawa walikuwa waasisi wa demokrasia ya vyama vingi na wengine walitangulia mbele ya haki.

Watu wa vyama vyote wanakaa pamoja. Hii ni kumpongeza rais.
Hii ni fursa adhimu kwa nchi yetu.
Kumbe point ni kumpongeza Rais na siyo kujadili contents?
 
Dr, Lilian Badi Mwenyekiti NGO taifa

Mchango uende kwa kamati itakayokuwa inafanya majumuisho. Kuhusu wakurugenzi wa halmashauri wasiwe wasimamizi wa uchaguzi.
Wakurugenzi kuwa wasimamizi wanauelewa wa maeneo ya utawala wa maeneo husika.
Kuteuliwa na rais hakutawafanya wasitekeleze majukumu yao. Kujitoa uanachama.
Athari ya watu ambao wapo nje ya Serikali ikiwemo ghrama.
 
Adv Paskal Mayalla
Hoja zangu ni nne:
Sheria yetu ya uchaguzi naomba ifuate katiba ya Tanzania. Katiba ya Tanzana imetoa haki kwa kila raia wa tanzania kuchagua kiongozi.
Katiba imetoa haki kwa mtanzania yoyote kugombea. Hapo katikati ibara ya 21 ikachokwa kitu kingine. Eti ikiwa mtu anataka kuchaguliwa lazima awe kwenye chama cha siasa.

Tume inatakiwa iitwe Tume huru na shirikishi.
Zanzibar wanafanya chaguzi tano kwa siku moja. Na sisi tunaweza kuungani chaguzi zote kwa pamoja kwa siku moja.
Utumishi wa vyama ni kujitolea. Kwanini tuvipe ruzuku vyama vya siasa. Ukifika kama Zaire kuna vyama zaidi 500.
Fedha za nchi sio za kugharamia vyama.
Hapa Paschal nakubali
 
Dr, Lilian Badi Mwenyekiti NGO taifa

Mchango uende kwa kamati itakayokuwa inafanya majumuisho. Kuhusu wakurugenzi wa halmashauri wasiwe wasimamizi wa uchaguzi.
Wakurugenzi kuwa wasimamizi wanauelewa wa maeneo ya utawala wa maeneo husika.
Kuteuliwa na rais hakutawafanya wasitekeleze majukumu yao. Kujitoa uanachama.
Athari ya watu ambao wapo nje ya Serikali ikiwemo ghrama.
Dr mjinga kama huyu ni hasara kwa taifa
 
Stella:
Kwa ufupi. Kifungu cha 30 sheria inatakiwa iseme kwa uwazi kuwa wenye ulemavu watakuwa asilimia ngapi(Wabunge na Madiwa). Na inatakiwa ieleze mchakato gani utumike kuwapata.
 
Mwasilishaji Majumuisho
Matumizi ya TEHAMA kuhusu uhifadhi wa nyaraka. Kuhakikisha Nyaraka zinahifadhiwa kwaajili ya kihitoria. Kama zitahifadhiwa kwa kutumia digital teknolojia itakuwa vizuri.

Zitto amezungumzia kifungu cha 6. Sisi tunapendekeza kuwa kifutwe kabisa.
 
Back
Top Bottom