Mkurugenzi MSD asimamishwa kwa ARV bandia

Kimbori

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
5,458
3,209
Nimesikia ya kwamba Serikali
imemsimamisha kazi Mkurugenzi mkuu wa bohari ya dawa Joseph Mgaya kutokana na kuidhinisha dawa bandia za
ARV. Pia mkaguzi wa bohari amesimamishwa; na kiwanda cha Arusha kimefungwa.
Wenye habari kamili tunaomba mtujuze.
 
kiwanda kilichotengeneza ni TPI LTD kinamilikiwa na ramadhan madabida na washikaji zake na zile ARV'S zilikuwa kwenye maboksi yao ya arv wanazozitengeneza. huyo ujamaa anagombe uenyekiti wa ccm-dsm anapambana na guninita
source: mimi mwenyewe
 
Haya ni matokeo ya tenda zenye utata,inawezekanaje asifunguliwe mashtaka na pia kwa nini MSD pekee?nani TFDA amewajibika kwa hili!Failed state inaendelea kujidhihirisha.Tatizo walilosababisha ni kubwa zaidi ya mnavyoweza kufikiri maana hizo dawa huwa ni mchanganyiko wa dawa tatu ila nasikia baadhi zimekutwa na dawa aina moja tu kitu ambacho kitaleta usugu wa dawa kwa wagonjwa wengi sana.TANOPHA mko wapi? fungueni kesi.Watanzania tujifunze kuchukia na kureact tunapofanyiwa mambo ya hovyo!!!
 
kiwanda kilichotengeneza ni TPI LTD kinamilikiwa na ramadhan madabida na washikaji zake na zile ARV'S zilikuwa kwenye maboksi yao ya arv wanazozitengeneza. huyo ujamaa anagombe uenyekiti wa ccm-dsm anapambana na guninita
source: mimi mwenyewe

Ukisikia tu mtu anagombea CCM lazima ujue kuwa anatafuta pa kuficha biashara zake chafu.
 
Bado na wengine wasakwe na kutupwa nje sio kuwasimamisha kazi halafu watu wanaendelea kula mshahara wa bure eti kupisha uchunguzi; uchunguzi upi kitu kinaeleweka wazi..?
 
Hii skendo inawagusa wengi sana wakiwemo TPI LTD. Waziri wa Afya
amefanya hivyo ili kuwafunga Watanzania modomo, kwa kuwa watasema "hili jambo lipo kwenye uchunguzi, hakuna haja ya kulijadili, kulijadili kutavuruga uchunguzi". Nchi hii kuna harakati za hatari kabisa, zote zina mshambulia mlala hou.
 
Hakuna kitu apo.
wapi Ikerege wa TBS?

we jambazi angalia hizi EPISODES:

1: aRV fake
2: Uchakachuaji wa mafuta
3: mkataba mbovu wa kukodi ndege ATCL
4: ujenzi wa barabara ya kilwa chini ya kiwango
5: ujenzi wa national stadium chini ya kiwango.
6: kuuza wanyama hai nje. Et cetera.

Hivi hapa kuna aliyewahi wajibika/wajibishwa?
 
Back
Top Bottom