bridalmask
JF-Expert Member
- Jan 14, 2015
- 2,195
- 1,168
Poor inheritence of DED....na huu ni ugonjwa uliyo kwa awamu hii itafika mahala wataji dehumanize wenyewe kwa wenyewe let keep on watching these series of movies from season one.
Hahaaaa!! Kumbe wana msimu mtani? Mbona huwa nawaona muda wote?mtani nipo sana....tunapishana..
wadudu na ukame huu watatoka wapi? mi nilidhani wewe ndiye uliyedeki mwanzo nilidhani ni geniveros Teh Teh Teh
huyu nae ni wazim mngineKama yeye ameshindwa kusimamia wanafunzi wadeki au wasafishe darasa, basi hacha asimamiwe yeye adeki
umeshaambiwa ni jioni darasa lina fanyiwa usafi saa ngapi.? unafikiri huyo mkurugenzi angewakuta walimu wa field angewaamrisha kipuuzi hivyo ? hajipendi ?Kama yeye ameshindwa kusimamia wanafunzi wadeki au wasafishe darasa, basi hacha asimamiwe yeye adeki
Does it matter?Mwalimu alikua wa kike au wa kiume?
Mkuu umenena hawa wakurugenzi waliotolewa UVCCM ni shida sana, yule wa Tanga kamtishia trafic kwa bastola, Arusha nako kuna mkurugenzi kamshusha cheo mratibu wa elimu kata na kumrudisha darasani kufundisha kisa wamezinguana na mbunge wa viti maalum wa ccm kwenye group la whatsapp, huku tena mkurugenzi kamdekisha mwalimu, nyoko kweli haya mambo yanafanyika ktk utawala unaofananishwa na mwalimu Nyerer, aisee haya ni matusi mwalimu aliheshimu sana walimu tena sana, ila sasa sijui hawa wakurugenzi walioteuliwa kwa uhakiki mkubwa wa mkuu ni kati ya wale mmoja ktika kila 4?! wanasikitisha na kuudhi kwa mabo yao ya hovyohovyo.Ninawasiwasi na Mkurugenzi pia
wana hifadhiwa ...kuna kipindi wanakuwa wachache kuna kipindi wanakuwa wengi hasa cha mvua...Hahaaaa!! Kumbe wana msimu mtani? Mbona huwa nawaona muda wote?
Aisee miee kudeki tena, tungekuwa tunaongelea mengine muda huu!
Akili mfu hiyoKwanza hodi maana kwa hili imebidi niombe tu uraia wa kudumu hapa JamiiForums na
any ways nisiwachoshe kwa ugeni wangu. naiweka kama nilivyo ikuta.
Mkurugenzi halmashauri ya wilaya Misungwi amemdhalilisha mwalimu wa shule ya sekondari Shilala iliyopo wilayani humo baada ya kumuamrisha kudeki darasa huku wanafunzi wake wakimshuhudia
Tukio hilo lilitokea pale ambapo mkurugenzi huyo akiwa ameambatana na baadhi ya mafisa walipo fika shuleni hapo mida ya jioni, muda ambao wanafunzi wa kidato cha nne walikuwa wakijisomea ili kujiandaa na mitihani.
Alipofika sekondari hiyo ya Shilala alitembelea madarasa baadhi na kukuta darasa moja likiwa chafu, ndipo akamuhitaji mwalimu aliye karibu kuja kujibu kwa nini darasa chafu na baada ya hapo mkurugenzi huyo akamwamrisha mwalimu huyo kudeki darasa hilo jambo ambalo mwalimu huyo hakuwa na pingamizi ingawa mwanzo alidhani huenda anaambiwa awaambie watoto wasafishe, hivyo akawa anafanya mpango wa kuwaambia wanafuzi ndipo mkurugenzi bila hata chembe ya busara akamwambia udeki wewe mwenyewe, mwalimu hakuwa na ajizi akatafuta ndoo na maji na kuanza kudeki huku wanafunzi wakimshuhudia.
MAONI YANGU SASA.
OMBI KWA SERIKALI NA WAHUSIKA WA MASWALA YA UTUMISHI
Ili mwalimu afundishe darasani na aeleweke kwanza lazima anaowafundisha waanze kumheshimu kwanza, sasa mazingira kama haya tena mbele ya wanafunzi na kuamrishwa kama naye ni mwanafunzi sijui hao wanafunzi watamuona vipi mwalimu wao baada ya tukio hili la fedheha alilotendewa na mkurugenzi huyu, na imekuwa desturi baadhi ya viongozi awamu hii hasa wakuu wa wilaya na wakurugenzi kudhalilisha watumishi wa umma kwa vile kwa sasa watumishi wa umma hawana mtetezi kabisa na wametelekezwa wakati wana mchango mkubwa sana kwa maendeleo ya taifa kutokana na mgawanyo wa majukumu waliyo pangiwa.
LAKINI PIA
Pamoja na dhana hii ya mwendo kasi na hapa kazi tu, watumishi wa umma waheshimike hasa wanao fanya kazi kwa karibu sana na jamii, maana wakijengewa mazingira ya kudharauliwa kiasi hiki nadhani na jamii nayo itawadharau zaidi.
Hawa wakurugenzi na baadhi ya wakuu wa wilaya na mikoa wa sasa walio wengi hawana kabisa skills za utawala bora na namna ya kupambana na changamoto na ninadhani hii yote inatokana na kuweka wanasiasa kwenye kazi zinazohitaji utaalamu na weledi wa hali ya juu sana.
Kama yeye ameshindwa kusimamia wanafunzi wadeki au wasafishe darasa, basi hacha asimamiwe yeye adeki