Katavi: Wanafunzi wazibua choo kwa mikono, Wazazi wamjia juu Mwalimu

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,346
5,570

Wazazi wenye Wanafunzi wanaosoma katika Shule ya Sekondari Kaliwaoa iliyoko Kata ya Ilembo, Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamechukizwa na kitendo cha mwalimu ajulikanaye kwa jina la Ndikulio Matenga shuleni hapo kutoa adhabu kwa Wanafunzi wakiume wa Kidato cha Kwanza kuzibua choo kwa kutumia mikono bila kuwa na vifaa.

Wazazi hao wamesema kitendo hicho hakipaswi kufumbiwa macho na Mwalimu huyo anapaswa kuadhibiwa au kufukuzwa kazi kwani amekuwa Mwalimu ambaye anawanyima amani wanafunzi katika shule hiyo.

Gabril Kitundu ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Mapinduzi amesema mwalimu huyo amekuwa na matukio endelevu ambayo mara kadhaa anakanywa pasipo mabadiliko huku Joseph Kang' ombe ambaye ni diwani wa kata ya Ilembo ameiomba serikali kuhakikishwa mwalimu Ndikulio Matenga anaindolewa katika shule hiyo.

Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Mpanda, Deodatus Kangu amekiri kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema tayari Mwalimu huyo amechukuliwa hatua za awali ikiwemo kumsimamisha kazi.
 
Back
Top Bottom