JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,462
Hayo yameelezwa na Mtaalamu wa Masuala ya Lishe, Maria Samlongo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kufuatia kambi ya siku mbili ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Dar Group iliyopo TAZARA, inanayotoa Huduma za Tiba Mkoba (Outreach Service) kwa kufanya kambi maalumu ya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mikoa jirani.
Ambapo mtaalamu huyo wa masuala ya lishe ameeleza kuwa yapo madhara ambayo watu wenye uzito wa kupitiliza yanaweza kuwakumba, ambapo ametaja baadhi kuwa ni pamoja na magonjwa ya kisukari, presha na mogonjwa ya moyo.
Aidha kwa upande wa Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto, ambaye ni Kaimu Mkuu wa Huduma za Tiba za Hospitali ya Dar Group, Dr. Eva Wakuganda ameeleza mwitikio wa watu katika kunufaika na huduma hiyo ambapo amesema wananchi wamejitokeza na baadhi yao wanaogundulika na matatizo ya moyo wanawahudumia kulinga na majibu ya vipimo.
Pia Kaimu Mkurugenzi wa JKCI- Dar Group Hospital, Iddi Lemmah ameendelea kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kunufaika na huduma hiyo inayotolewa bure. Ambapo huduma hiyo inatarajiwa kuhitimishwa kesho March 3, 2024 ikiwa ni siku ya pili.
Itakumbukuwa Dr. Eva alitaja dalili mbalimbali za magonjwa ya moyo kwa watoto wadogo kuwa ni pamoja na mtoto kuanza kuwa na mwonekano wa rangi ya bluu kwenye sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo kwenye midomo na kucha, changamoto ya upumuaji, kushindwa kuongezeka uzito, mapigo ya moyo kwenda mbio, mtoto kushindwa kula au akila anachoka na kutoka sana jasho.