Mkoa wa DSM Kugawanywa na Kuunda Mkoa wa (Ilala +Kisarawe -HQ) na Dar Es Salaam

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,695
1,696
Nimesikia Tetesi kuwa Mkoa wa Dar Es Salaam utagawanywa sehemu mbili ili kurahisisha utawala na kuleta ufanisi.

  • Kutakuwa na Mkoa wa Dar Es Salaam bila Wilaya ya Ilala.

  • Kutakuwa na Mkoa wa Ilala ambao utakuwa na Wilaya ya Ilala na Kisarawe huku Kisarawe ikiwa makao makuu ya Mkoa.

Mwenye taarifa zaidi tunaomba atupatie.

Sasa hivi kuna viwanja vingi sana vya serikali vimepimwa na vinaendelea kutolewa huko KISARAWE na wadau wanavichukua kwa kasi ya ajabu. Taarifa za Uhakika ni kuwa kuna Viwanja vya LOW DENSITY - TZS 1.0 Million; MEDIUM DENSITY - TZS 800,000 na LOW DENSITY - TZS 500,000.

Habari Ndo Hiyo!

Mkoa wa Njombe, Mkoa wa Ilala, watu wanabunifu wa njia za kupata ulaji. Langu jicho.
 
Mkuu, jitahidi walau upate kiwanja. Vya low density vimetulia. Kisarawe kumetulia na Road Traffic Flow yake ni nzuri kuliko ya Mbezi/Tegeta Road.

Ya utawala, hayo ngoja tuwaachie wenyewe maana bado ni tetesi tu.
 
Sasa hivi kuna viwanja vingi sana vya serikali vimepimwa na vinaendelea kutolewa huko KISARAWE na wadau wanavichukua kwa kasi ya ajabu. Taarifa za Uhakika ni kuwa kuna Viwanja vya LOW DENSITY - TZS 1.0 Million; MEDIUM DENSITY - TZS 800,000 na LOW DENSITY - TZS 500,000.

MKuu hii ni habari njema sana,tafadhali unaweza kutumatia maelezo zaidi namna ya kuvipata hivyo viwanja? unajua sio sio lazima tubanane katikati ya mji,kama sisi vijana huko Kisarawe kuna tufaa zana. More details
 
Mkuu maybe ni Temeke + Kisarawe na makao makuu yawe Kisarawe but not Ilala. Unajua kuwa City Centre ipo Wilaya ya Ilala? Haiwezi kuja akilini kwamba wakazi au wafanyabiashara wa city centre wawe wanawajibika Kisarawe. Hapana
 
Josm;

Nenda Kisarawe Ofisi ya Ardhi ya Wilaya siku yoyote ya Kazi. Kujaza Form ni TZS 5000 tu. Ukiwa na Pesa ya Kiwanja unalipia hapo hapo na unapewa Kiwanja.
 
Mkuu Mimi sina uhakika kwani bado ni tetesi. Ila kama ni kweli Kijiografia bado ni sawa. Angalia ramani ni wilaya ya Ilala tu inapakana na Kisarawe:
attachment.php
 
Attachments

  • Dar Es Salaam Map.jpg
    Dar Es Salaam Map.jpg
    56.1 KB · Views: 433
Nafikiri kuna haja ya kuangalia jinsi mikoa ilivyotengwa. Trend hii kama ni kweli basi hali ni mbaya. Kama kuna nia ya dhati basi ni vyema kuangalia upya baadhi ya mikoa mfano Mwanza, Mbeya, Iringa, Morogoro na Pwani ikaangaliwa upya!
 
Josm;

Nenda Kisarawe Ofisi ya Ardhi ya Wilaya siku yoyote ya Kazi. Kujaza Form ni TZS 5000 tu. Ukiwa na Pesa ya Kiwanja unalipia hapo hapo na unapewa Kiwanja.

Mkuu ubarikiwe sana,habari kama hizi ni nzuri sana zina tufaa wapenda maendeleo.
 
Mkuu Mimi sina uhakika kwani bado ni tetesi. Ila kama ni kweli Kijiografia bado ni sawa. Angalia ramani ni wilaya ya Ilala tu inapakana na Kisarawe:
attachment.php

sawa Mkuu lakini kama hizi tetesi ni za kweli, naona watakuwa wanachemsha. Yaani Mtu akitoka Kinondoni atakuwa anaingia Mkoa mwingine ndo aende Temeke. Pia kutakuwa na mkorogano mkubwa sana hasa maeneo ya posta, ferry na Ikulu. Katika hali hiyo Ikulu itakuwa Mkoa wa Kisarawe/Ilala na Mkuu wa Mkoa ataishi Kisarawe.

Kama watakuwa wanaamua hivyo, lengo lao ni Dar kuto loose Bandari, Uwanja wa ndege, National stadium na Kigamboni. Otherwise location ya Temeke ndiyo ipo strategic kwa kuungana na Kisarawe.
 
Mmh haya! tusubiri mkoa wa Bagamoyo naona mikoa ina ota kama uyoga sasa....
 
Mzee mkoa wa bagamoyo tayari,angalia, nyumba za watumishi kajenga magufuli na akaziita za nhc zipo Chalinze njia ya kwenda moro, ni ghorofa,hamna wakaaji na sasa wanakaa popo, bandari ya bagamoyo inajengwa na kupanuliwa (wairan juzi wamesema watasaidia), uwanja mkubwa wa ndege unajengwa bagamoyo(je unakumbuka enzi za KIA na Arusha awamu ya tatu). hizo ndo dalili zenyewe.
 
sawa Mkuu lakini kama hizi tetesi ni za kweli, naona watakuwa wanachemsha. Yaani Mtu akitoka Kinondoni atakuwa anaingia Mkoa mwingine ndo aende Temeke. Pia kutakuwa na mkorogano mkubwa sana hasa maeneo ya posta, ferry na Ikulu. Katika hali hiyo Ikulu itakuwa Mkoa wa Kisarawe/Ilala na Mkuu wa Mkoa ataishi Kisarawe.

Kama watakuwa wanaamua hivyo, lengo lao ni Dar kuto loose Bandari, Uwanja wa ndege, National stadium na Kigamboni. Otherwise location ya Temeke ndiyo ipo strategic kwa kuungana na Kisarawe.

Nziku;

Nchi hii miundombinu yetu bado haijakaa vizuri kabisa.

Unajua Kisarawe pia iko Mkoa wa Pwani ambayo makao yake Makuu ni Kibaha. Cha ajabu huwezi kwenda Kibaha bila kupita DSM kwa kuwa njia ya kuunganisha Kisarawe na Kibaha ndo hivyo tena.

Kuna watu Wanafanya Kazi Kibaha wengi sana wanaishi DSM, hali kadhalika wengi wanaofanya kazi Kisarawe wanaishi DSM including Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe.

Kazi Kweli Kweli
 
Mzee mkoa wa bagamoyo tayari,angalia, nyumba za watumishi kajenga magufuli na akaziita za nhc zipo Chalinze njia ya kwenda moro, ni ghorofa,hamna wakaaji na sasa wanakaa popo, bandari ya bagamoyo inajengwa na kupanuliwa (wairan juzi wamesema watasaidia), uwanja mkubwa wa ndege unajengwa bagamoyo(je unakumbuka enzi za KIA na Arusha awamu ya tatu). hizo ndo dalili zenyewe.

Nasikia Pia ile barabara ya Kuunganisha Bagamoyo na Tanga nayo itajengwa soon.
 
JK anataka kuongeza ajira ,nafikiri hiyo ni mbinu nzuri ametumia
 
Bila ya kusahau wilaya mpya ya Mbezi ambayo makao yake makuu yatakuwa Luguruni... Wilaya hii mpya itajumuisha Kimara,Mbezi,Luguruni,Kiluvya,Goba,Wazo,Tegeta,Boko na Bunju
 
Nadhani Superman angeliweka hivi, "Tarafa ya Ukonga iliyopo Wilaya ya Ilala kuunganishwa na Kisarawe", badala ya kusema Wilaya ya Ilala. Hii itatatua mkanganyiko wa City centre kuhamishiwa Kisarawe.
 
He, huku Chalinze Segera hadi Tanga, double Roads na Bagamoyo Tanga barabara, Hee Wagosi wanasafiri sana eeh.
 
Back
Top Bottom