Mkimgusa Edward Lowassa mtasahaulika katika siasa za Tanzania!

Nadhani umetumwa na kama ni ushahidi hapa si mahali pake. Tunahitaji mtu safi na mwenye uzalendo na nchi hii.Wengi wanajua huyu bwana si safi ikiwa ni pamoja na walio kaburini (Nyerere, etal.). Kama anataka kujisafisha kwa sasa atatumia nguvu nyingi sana, tena sana.Ni sawa na kumwosha mtu aliyetumbukia chooni akaokolewa kwa kutumia sabuni yambuni. Ukiona mtu anafuta uongozi kwa kuhonga watu na makundi, ni hatarisana.

Wote tuna makosa. Nitajie ndani ya ccm asiye fisadi. Haitoshi kusema "ndani ya ccm kuna watu wengi wasafi."
 
Nchi hii tunahitaji kiongozi imara mwenye uwezo wa kuisemea serikali na kuisimamia,sio sasa hivi kila mtu analialia tu,na mwenye uwezo huo ni EL pekee,hakuna mwingine ndani ya CCM,mpende,msipende.
 
Tatizo la msingi ni kuwa CCM karibia wote wanabei na Lowasa anazijua bei zao na yupo tayari kuwanunua mmoja baada ya mwingine. watu ambao hawana bei katika CCM ni wachache na hawana ushawishi kwenye sekretariet. Ile sekretarieti, mie namuona Mangula tu ndoo hana bei. The rest wanalipika kwani ni watu wa fedha
 
Tatizo la msingi ni kuwa CCM karibia wote wanabei na Lowasa anazijua bei zao na yupo tayari kuwanunua mmoja baada ya mwingine. watu ambao hawana bei katika CCM ni wachache na hawana ushawishi kwenye sekretariet. Ile sekretarieti, mie namuona Mangula tu ndoo hana bei. The rest wanalipika kwani ni watu wa fedha

Lowasa akipitishwa ndio mwisho wa ccm
 
ktk maelezo yako unajichanganya,mala unasema Lowasa anakubalika ndani ya chama na nje ya chama,ingawaje ccm itakuwa chama pinzani,hapo ndipo nimeshindwa kukuelewa.
Ni kwamba,mgogolo huu ni wa mpito tu na mambo yatakapokuwa sawa na wanaccm kukubaliana nani apeperushe bendera ya ccm ktk uchaguzi mkuu wa urais ndipo utakapo elewa vyema kuwa ccm haiwezi kuwa chama pinzani hususani ktk nafasi ya urais na hili linawezekana tu kama hakutakuwa na sintofahamu ndani ya cc.
CCM ni wepesi sana wa kucheza karata,kumbuka ya zanzibar mwaka 2010,ilikuwa ni mshike mshike kati ya rais wa sasa na makamu wa rais muungano,lakini mwenyekiti aliwaeleza kama ni madaraka basi msiwe na shaka,ili chama kiendelee kuwa imala ni vyema tukaweka pembeni tofauti yetu na kweli mambo yakawa kama ilivyokusudiwa na sasa 2015 inakuja.
Lowasa akisimamishwa kugombea nafasi ya urais kwa bendera ya ccm kutakuwa na ushindi wa kimbuga ama sunami kama ilivyotokea kule zimbabwe.
Huu ni mtazamo wangu
mtazamo finyu!
 
Mtu anawezaje kuamka kutoka atokako na kudai wanaccm wote wameshaamua kuwa Lowassa ni chaguo lao? Matusi gani haya? Kama kwako ameshafika bei, shauri lako. Lowassa akiwa Rais wa Tanzania itakuwa janga la kitaifa kwa miaka 10. Usisemee wengine. Jisemee mwenyewe. No research, no right to speak.
 
Kipindi kile, nikiwa mvulana, wakati dada alikuwa anatuogesha nilikuwa mtundu na nilitaka kujaribu kila kitu especial yale ambayo wazazi walikuwa wanakataza...na kweli niliyajaribu, na nikagundua hidden potential kwenye mengi niliyokuwa naambiwa acha...

Edward Lowasa ni fisadi, yes...wenzake wa CCM wanamwita hivyo, Lowasa hafai kuwa kiongozi, yes makada waandamizi wa chama chake wanatuaminisha hivyo? Ni mtu hatari, wameenda mbali kwa kumwita silent killer , yes kwa kuwa hata abebeshwe tuhuma gani huwa hakubali wala kukataa...

Hatari nayoiona hapa ni kama kizazi tukutu kitaamua kuanza kumpekua,na kumsikiliza huyu CCM wanayemwita mwanampotevu na kugundua hidden potential, hakika CCM hata wake za hao wanaompiga vita wanaweza kuwasaliti bwana zao kwa kumshabiki! Hebu CCM onesheni uthubutu mumfukuze Lowasa CCM isipokuwa NGO....jaribuni muone!
 
- Kaka heshima yako sana, kama ninavyosema kama kweli haya ndio maneno ya kumtetea Lowassa na Richmond basi mna safari ndefu sana hiyo kambi mpaka kushika Urais, hivi ni ushahidi upi huo mnaoutaka kuhusiana na Richmond? Ni kwa nini Lowassa alijuuzulu Uwaziri Mkuu? eti ni kwa sababu hakukuwa na ushahidi wa Richmond yeye na mawaziri watatu wakajiuzulu badala ya kusimama mbele ya bunge na kutoa huu utetezi wenu mnaouleta huku sasa hivi when it is too late!!

- Nimeamua kuandika hapa kwa sababu hata wewe ukiangalia hakuna mtu anayewapa majibu seriious na hizi nyepesi nyepesi, yaani unaongelea "The Benefit of the doubt" kwenye kasi ya kisiasa ya Waziri Mkuu aliyejiuzuulu na mawaziri watatu kwa pamoja na the very same skendo, unasema ushahidi hakuna au mwenye nao auelete hapa JF, ha! ha! ha!,

- Kaka kwa haya maneno sio siri kwamba mnaamini wasomaji wa JF wengi ni wajinga maana mngejua kuwa tupo wenye akili hamuwezi kuja hapa na hizi nyepesi nyepesi, I mean mnaandika ujinga ujinga halafu mkiul;izwa mnaanza kuingiza mambo ya personal badala ya kusimamia hoja zenu, Lowassa alitakiwa kusimama bungeni ile siku na kujibu tuhuma sio kukimbia na kuanza kulia lia huku JF kwamba eti hakuna ushahidi, yale yalikuwa makosa makubwa sana kisiasa kwa mtu mwenye ambitions kama zake za Urais, alitakiwa kusimama pale pale kidete bungeni na kujibu mapigo, poleni sana kaka

- Mimi sina chuki zozote na Lowassa ahajanikoea anything ila nafuata lines za siasa na Taifa na kutoa maoni yangu ambayo huwa watu wake hamuyapendi sana, ninarudia tena kama wewe ni mmoja wa washauri wake Lowassa au wanaompigia debe basi ndio maana hatapata urais, kama kweli Lowassa anataka urais anahitaji kuwafukuza washauri wote alionao sasa maana hamumsaidi kabisa na maneno kama haya,

- Mngetumia muda mwingi sasa hivi kuwashawishi Wa-Tanzania uhalali wa mapesa mengi aliyonayo ambayo tunawaona waliowaiwa wakitanua nayo hapa mjini je aliyapata wapi?

Le Mutuz

CCM wanatakiwa kunshukuru EL ..angejibu mapigo kama unavyotaka Rais angekuwa ndio wa kujiudhuru.He took one for the team, everybody know that!!

Kwa nini hajavuliwa gamba basi?

CCM vipande vipande haa haa haha ..kwi kwi kwi tehe tehe tehw lol
 
Watetezi wa Lowassa ni Chadema funny!

Lowassa nenda chadema baba kwa mafisadi wenzako

Lowassa CCM door is closed for you..
 
Back
Top Bottom