Mkimgusa Edward Lowassa mtasahaulika katika siasa za Tanzania!

wewe sasa hivi ni wakutiliwa shaka, huaminiki,vyanzo vyako vya habari ni vya kukurupuka!
 
Chondechonde Kikwete achana na agenda hiyo ya UPOLE, inakiua chama chako na serikali yako,

Ni karibu miezi 28 sasa, Edward Lowassa amekuwa agenda kuu ndani ya CCM na wanaccm wenyewe, si mwenyekiti wala mjumbe wote mioyo yao ni Lowasa tu, wengi wakitaka ajipambanue nakuwa nyota huru ya chama na wachache walio juu ya chama wakitaka kumpoteza gwiji huyu wa siasa za ukwasi na fitina msonge!

Ikumbukwe kuwa doa kuu linalotajwa kuwa Lowasa ni fisadi ni Richmond, lakini nani asiyejua richmond ni nani na ilikuwaje? Pale dodoma Lowasa ameweka wazi mbele ya Mwenyekiti kuwa hakuna kilichotendeka ambacho mwenyekiti hakukijua ama kumtuma! Narudia tena UCHAFU wa LOWASSA ni RICHMOND tu!

Nauliza tena RICHMOND ni nani? Mwenyekiti alijibu nini siku ile pale Dodoma wakati Lowassa anamhoji zaidi ya kuinamisha kichwa chini hali iliyopelekea BWM kumtuliza Lowasa?

Sasa Lowassa anakitaka Chama na anatakka agombee urais 2015 na ameshashinda ndani ya Chama na nusu uwanja nje ya chama, shime ccm, ili muendelee kuitwa chama cha siasa japo mtakuwa wapinzani zuieni jaribio la mwenyekiti wenu la kujaribu kumzika Lowassa angali amekibeba chama!

Kuna juhudi za kitoto ndani ya ccm eti wapo kwenye harakati za kumuuandaa January Makamba kugombea Urais 2015, wanatumia raslimali za nchi kujijenga kisiasa kwa upinde wa mvua ya siasa!

Chondechonde mwenyekiti wa ccm ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, Amini Lowassa ndie chaguo la wanaccm wote hata hao wanaojifanya wapo na wewe mioyo yao ipo kwa Lowassa! Wanakula na kunywa kwa mgongo wa Lowassa!

Mwenye USHAHIDI wa wazi juu ya UFISADI wa Lowassa aulete hapa, sio stori za kulishwa vijiweni kisha mnakuja hapa kupiga ngonjera ooho Lowasa fisadi, oooho sijui nini! Leteni utetezi hapa au mfikisheni mahakamani!

Mimi nitampa kura yangu ikiwa atagombe japo hata shinda, lakini atakinusuru chama kufutika kabisa duniani!

Rejao, zomba, Malaria Sugu msianze kuugua matumbo ya ghafla!

EL2015
Yericko,
Walimgusa Lowassa. Bado wako wanadunda.
Huko chadema alikohamia hali yao ni mbaya. Imebaki sauti ya Tundu Lissu tu.
Ulikuwa sahihi kusema akigombea utampa kura yako na hatashinda.
 
Yericko,
Walimgusa Lowassa. Bado wako wanadunda.
Huko chadema alikohamia hali yao ni mbaya. Imebaki sauti ya Tundu Lissu tu.
Ulikuwa sahihi kusema akigombea utampa kura yako na hatashinda.
Hujauona ulemavu ambao chama "twawala" kimeupata na kuanza sarakasi na ndoto za kufikirika?
Hujaona hoja zinavyozimwa kwa kutumia mabavu?
Hujaona kadri siku zinavyozidi ndivyo hali inavyoendelea kuwa taabani?
Hujaona inavyobidi kununua watu ili ionekane yale mabavu ni upendwa?
Hujaona wanaokosoa wakitiwa misukosuko ili uvundo na uozo ufichike?
Bado tu hamuoni mmebaki kumuimba kila uchao na sera zake mliziiga zimewatokea puani bado tu hamuoni?
Yericko hakukosea
 
Yericko alisema Lowassa akiguswa ccm inafutika....haijafutika.
Hayo unayoyasema yanaonyesha jinsi Lowassa na timu yake wanavyodhibitiwa bila kufurukuta.
Na kwa usawa huu watafutika kabisa.
 
Nyie JPM kawamaliza, mmebaki kutapatapa kama mfa maji
 
Kilasiku wanazunguka Mbuyu lakini hamna anayejaribu kuugusa na pia anauwezo wa kuzungumzia mahali popote na kuwakemea viongozi wote wa CCM mpaka Mkuu na wasimfanye chochote huyo ni mwamba Ndani ya CCM. jamaa akichukua form ya Urais ndani ya CCM lazima wafyate mkia wote

Vipi ndugu, Lowassa yuko wapi leo
 
Yericko alisema Lowassa akiguswa ccm inafutika....haijafutika.
Hayo unayoyasema yanaonyesha jinsi Lowassa na timu yake wanavyodhibitiwa bila kufurukuta.
Na kwa usawa huu watafutika kabisa.
Ni kweli kabisa usemavyo, bila msaada wa dola ayasemayo Yericko yangeisha timia mapema tu. Kusingekuwa na kitu kinaitwa CCM, hata masalia yake yasingekuwepo!
 
Yericko alisema Lowassa akiguswa ccm inafutika....haijafutika.
Hayo unayoyasema yanaonyesha jinsi Lowassa na timu yake wanavyodhibitiwa bila kufurukuta.
Na kwa usawa huu watafutika kabisa.
Inayumba kwa kasi ya kimwondo ndio maana vyombo dola vinajitahidi kuiwekea vigingi na miti isiporomoke.
Hujiulizi kwanini watu wanatishwa kila uchao? Usijiulize kina Lissu, Jiulize ilikuwaje Nape akatishiwa? Ilikuwaje Roma... ilikuwaje.... Utapata majibu kwamba lichama limechokwa ndio maana hata magazeti yanatishwa na waandishi wanaishi kwa hofu. Waheshimiwa Wanasheria, Mahakimu na Majaji wapo katika mashaka. Watumishi hawaijui saa wala siku... bado haitoshi kada tulioahidiwa neema tunapambana na hali zetu huku matajiri wakijikusanyia mapesa yao kwenye manunuzi yasiyofuata sheria za manunuzi. Hadi hapo wakosa haya wanasimama na kutangaza utumbo kuwa lichama linazidi kung'ara!!!
Kweli kama hivyo ndio kung'ara hongereni
 
Nyie JPM kawamaliza, mmebaki kutapatapa kama mfa maji
Mkipata majibu ya MAKINIKIA na Bombardier Q400, Milioni 50 kila kijiji, Sukari 1800 tutajua nani anatapatapa kwa kutumia vyombo dola ili hofu itawale na watu wanaoumia wanyamaze kama si kunyamazishwa

Serikali yamwaga ajira 52,000 waombaji wakionyesha udhaifu
Soma hiyo habari uone ilivyo na nyufa na inavyoacha maswali kisha uje tuendelee na mjadala husika.
 
Mkuu wakati mwingine uwe unakubali tu kwamba Yeriko kwenye thread hiyo alichemka! Alisema CCM wakimgusa Lowassa CCM itapotea swali ni je CCM imepotea? Jibu ni hapana bado ni chama tawala. Labda sehemu alipopatia ni kwamba atampigia kura Lowassa lakini hata shinda! Ni kweli Yeriko alimpigia kura alipohamia Chadema lakini hakushinda. Huu ndio ukweli wala hautabadilika!
 
kuna maswali hujanijibu mkuu
 
Back
Top Bottom