MVUMBUZI
JF-Expert Member
- Jan 8, 2011
- 5,182
- 2,304
Rafiki wangu wa karibu sana amenieleza tatizo lake nikaona si vyema kulileta hapa kwa wahenga kwani palipo na wengi hapaharibiki jambo.
Anasema ameona na mkewe ndoa ya Kikristo miaka 10 iliyopita na kipindi chote cha uchumba aliamua kuto onja chochote hadi ile siku ya ndoa yao ili heshima, uaminifu na adabu iwepo. Baada ya kuona kila mmoja alimweleza mwenzake tabia ambazo hazipendi kama kufokeana hadharani, kupigana n.k. na wakakubaliana kwamba kila mmoja atajitahidi asimwudhi mwenziwe. Miaka 5 ya ndoa ilikuwa mizuri na waliishi kwa kuzingatia misingi waliyoiweka. Baada ya miaka mitano mkewe akaanza zile tabia ambazo ni kero kwa mumewe huku mume akimkumbusha kuwa anakiuka maagano lakini mkewe anaziacha wiki then anarudia tena.
Mbaya zaidi kuna kipindi mume alisafiri na katika kumpigia mkewe simu kumtakia hali na kumweleza habari za safari mkewe akashindwa kuwa seriuos kuhusu ule ujumbe kwani inaonyesha alikuwa ametingwa labda na TV au na kitu kingine. Hii hali ikawa imemuudhi mumewe na wakawa wanajibizana ki ugomvi ugomvi na hata aliporudi akawa amerudi na uso wa chuki.
Ilipofika usiku kitandani kana kwamba haelewi kilichomuudhi mumewe mkewe akaamuuliza mbona huongei na mimi kwa furaha? nini kimekuudhi?
Maswali haya yalimuudhi sana yule mume kwani hakujua mkewe haelewi nini wakati wamegombana jana kwenye simu na hawajasuluhisha.
Naomba mawazo yenu wana JF je mwanamke kama huyu utamwelewaje? amekupuuza? ameku ignore? au ana matatizo gani?. Na nini cha kumfanya ili awe na approach sahihi?
Hii ndio maana huyu rafiki yangu amesema hamuelewi mkewe hata baada ya kuwa kwenye ndoa kwa miaka 10 sasa. Naomba msaada wenu,