Babu wa miaka 110 amuua mke wake kwa kisa cha kumnyima unyumba

Utawala2025

JF-Expert Member
Oct 20, 2023
329
1,058
#HABARI Polisi huko katika wilaya ya Ntungamo nchini Uganda, wanamshikilia mzee mmoja mwenye umri wa miaka 110 kwa tuhuma za kumuua mkewe mwenye umri wa miaka 109 kwa kosa la kumnyima unyumba.

Kwa mujibu wa msemaji wa polisi wa mkoa wa Rwizi Samson Kasasira, Mzee Dominic Babiiha anatuhumiwa kumuua mkewe Costansio Bakasisa akitumia mundu majira ya saa 1 asubuhi jumamosi huko nyumbani kwao eneo la Kahunga.

Taarifa Zaidi zinatanabaisha kwamba wazee hao ambao ni wakulima wamekua wakiishi vyuumba tofauti tangu walipooana.

Polisi wamesema mkewe alikataa kumpa tendo la ndoa sababu alikua akijisikia vibaya, ambapo licha ya hayo bibi huyo aliendelea kulazimishwa tendo hilo ambapo aliamu kwenda kulala chumba cha wajukuu zake.

Mzee huyo aliamua kuchukua mundu na kumuamuru atoke nje ya chumba, ambapo aliingia kwenye chumba hicho na kumshambulia na mundu mfululizo huku wajukuu wakikimbia nje kuomba msaada. #EastAfricaTV
 

Mwanaume akinyimwa tendo la ndoa anakuwa mkali kama Simba..
 
Wazee wa zamani wana nguvu sio wa chipsi yai...

Wazee wanapenda utamu kuliko vijana..
Ndio maana wanapenda dogodogo...
Yaani kuhani musa unanipa wasiwasi sana hizi mada unazochangia.

Kimtokacho mtu ndicho kilichoujaza moyo wake.

Kesho upo kuhani musa
 

Mwanaume akinyimwa tendo la ndoa anakuwa mkali kama Simba..
Unajiona umeongea pointi kweli
 
Back
Top Bottom