Mke wangu atanifikisha pabaya

Gopsh

Member
Oct 11, 2012
15
4
Ivi km una mke wako,umegundua anatembea nje ya ndoa waziwazi bila vifisho na una vithibitisho,ukaamua kumfukuza,mkatengana kln akiwa na ujauzito wako na sio kutoka nje tu ila na matatizo mengine ikiwemo kutoshiriki vzr na ww tendo la ndoa na heshima ya km mume kwake haipo,baada ya kutengana,miezi mi nne akakuendea kwa mganga ukamrudisha baadae ukapata ushahidi alikuendea kwa mganga na wewe una mwanamke mwingine uliamua kuwa nae baada ya matatizo ila umeamua kumrudisha jifungue kwanza ila hujui cha kufanya na mtoto hujui km ni wako,sasa nimuoe huyo mwanamke mwingine atunze watoto au kumsamehe huyu huyu na yote alofanya?lkn kila ukimuona amani haipo?nisaidieni jamani
 
Kama mkeo ndio kwanza ana mimba (regardless ya miezi mingapi) huyu mwanamke mwingine ulianza kutoka nae lini mpaka ufikie uamuzi wa kumfanya replacement ya mkeo...?

Unajua wanaume wengi mmezoea kuchiti...mkichitiwa nyie pressure inapanda...pressure inashuka...mkeo hata kama alikuchiti kuna uwezekano mkubwa wewe ndio ulianza na yeye itakuwa alikuwa analipiza kisasi.

Hayo ya sijuhi namrudia mpaka ajifungue...akisha jifungua...utasema nasubiri mtoto akue...mmeshabomoa ndoa yenu.

Eti alienda kwa mganga who told you? Huyo replacement?

Nyie ndio mnafanya watu waogope ndoa kumbe mnakosa kujua kuwa ndoa ni kitu kitakatifu...inahitaji descipline ya hali ya juu kuweza kulinda ndoa yako...kuoa mwingine si solution.
 
vitu kama hivi hushauriwi, tumia ufahamu wako wa kupima machungu ya mkeo na raha ya huyo mwingine.
 
Hivi mtu ukirogwa unajisikiaje sikiaje? Humtaki mkeo afu unashindwa kumuacha? Kichwa kinauma?

Mtu akisema karogwa mi nacheka sana...afadhali asemewe na third part...lakini mwenyewe eti 'nimerogwa'.
 
Hivi mtu ukirogwa unajisikiaje sikiaje? Humtaki mkeo afu unashindwa kumuacha? Kichwa kinauma?

Mtu akisema karogwa mi nacheka sana...afadhali asemewe na third part...lakini mwenyewe eti 'nimerogwa'.
aliyerogwa hawez kujitambua, kama anasema kalogwa basi keshapata tiba.
 
Hivi mtu ukirogwa unajisikiaje sikiaje? Humtaki mkeo afu unashindwa kumuacha? Kichwa kinauma?

Mtu akisema karogwa mi nacheka sana...afadhali asemewe na third part...lakini mwenyewe eti 'nimerogwa'.

na ukisema wife 'kaniroga' ndio nikaudiana nae
na keshoo ukiambiwa huyo mwanamke mwingine alienda kwa mganga?
utasemaje?
kila anaekusogelea 'mchawi'?
 
|M|wisho na yeye atajiunga kwenda kwa waganga...mwe!

maana umeshakuwa mduara.

mtu unaweza kuwa kichaa kwa woga tu na imani kuwa 'mi nimerogwa' hofu juu ya hofu...unajiogopa mwenyewe.

Na hao watakao kupeleka kwa waganga hao ndo
watakwenda 'kukushughulikia vizuri sasa kiulaini '....lol
 
Huyo replecement ilikuwa mwaka jana mwezi wa 11 mwishoni na huyo mwanamke mimba alipata mwezi wa 11 mwanzoni na alinilazimisha tendo la ndoa..sikuwa na mpango wa kuzaa nae tena,pia matatizo yalianza muda nikamvumilia sijawah kucheat mimi ni baada ya matatizo kuzidi,pia aliemsindikiza huyo mwanamke kwa mganga ndo alietoa siri hiyo na mwanamke akakiri kweli kanifanyia dawa akadai nimsamehe
 
We fikiria tu kwa makini YUPI MTAMU SANAAAA, WHO MAKES YOU HAPPY, NANI TULIZO LA MOYO WAKO, NANI UKIISHI NAE UTAPATA AMANI!!!!! Baaaaaaaaaaaaaaaass! Mie nikikushauri nitakuwa muongo sababu ukweli moyo wako ndo waujua. Tafuta mahali furaha yako ilipo! Baaaaaaaass!
 
Na mbaya zaidi alikuwa anatembea na mume wa mtu na huyo mwanamke alimuonya hakuelewa akaniface mimi,ma sio mwanaume mmoja na zaodi nilikuwa sipati haki ya tendi la ndoa kumbe alikuwa na anaempa kwa mapenzi yake mimi mpaka nimlazimishe mpaka tukatengana vyumba ndani mwisho kutengana na nilimkabidhi kwa wazazi wake kuwa simtaki tena mpaka alipoamua kuniendea kwa waganga
 
Nina mawazo mpaka nakosa usingizi mimi sielewi huyo mwanamke mwingine nampenda sana na naamini nikiwa nae nitakuwa na furaha,amani,na maendeleo ila nawaza ataweza kulea watoto wangu??na kuendelea kuwa na huyu mwanamke mwenye mimba bado sitakuwa na amani kabisaa kila nikimuona napata hasira na je nitajuaje km huyu mpya ataweza kunitunzia watoto japo yeye anasema ataweza
 
Mmmh kazi unayo babu ila time nyingine kama hutak kuzaa play safe kuepusha shari
 
Kumbe mna watoto wengine.

Bado sioni ni kwa nini unaamini kuwa hiyo mimba ni yako kama mkeo ni mzizi ze wey unavyomzungumzia...kutembea na wewe siku mmoja ndio apate mimba aache kupata huko anakotembea siku zote?

Otherwise ulifanya haraka kutafuta replacement wakati wewe huko kwenye confusion...mara nyingi mtu huwezi kufanya maamuzi makini ukiwa frustrated...tulia na wanao utapata real replacement if necessary...si wa kukurupuka...

Hyu unamsifia sasa kuwa anakupenda sana...sijuhi nini ni kwa kuwa huko heart broken...don't rush into anything serious utarudia makosa au utajikuta na matatizo makubwa zaidi ya ya mwanzo.

Back
Top Bottom