MBUZI MWENYE BUSARA
Senior Member
- Nov 24, 2019
- 143
- 151
Habari wadau wa jukwaa hili pendwa,
Naomba nienda moja kwa moja kwenye mada.
Mimi nimeoa na Mungu amenijalia watoto wawili. Nafanya kazi sekta binafsi na mke wangu sasa ni mama wa nyumbani. Mke wangu kabla sijamuoa alikuwa amenunua kiwanja chake makao makuu ya wilaya na mimi pia nilikuwa nimenunua kiwanja changu katika wilaya hiyo hiyo ila kwenye tarafa mojawapo.
Tulipooana tuliamua kuishi wilayani, kipindi hicho mimi nilikuwa sina kazi ila yeye alikuwa na kazi japo si mshahara mkubwa na alikuwa kwenye kata mojawapo katika wilaya hiyo nami nilikuwa nimepanga makao makuu ya wilaya, ambapo yeye ndiyo alinunua kiwanja.
Mwaka mmoja baada ya ndoa nikaajiriwa mkoa mwingine hivyo nikamuacha yeye na mtoto, yeye akiwa bado anafanya kazi.
Nikaanza kujenga msingi kwenye kiwanja changu na sikuendeleza nikaachia kwenye msingi. Baadaye nikapiga msingi kwenye kiwanja chake.
Mwaka moja baadaye yeye akaachishwa kazi pale alipokuwa anafanya kazi, ikabidi niwachukue nikae nao mjini. Lakini nikaona ni gharama sana kupanga mjini na mshahara ni mdogo, nikaamua kuchukua mkono nikaendeleza msingi katika kiwanja chake kwa maamuzi kwamba, niendeleze hata vyumba kadhaa halafu niirudishe familia wilaya wakakae huko, mimi nichukue chumba kimoja kupunguza gharama.
Hili pia lilichangia na mgogoro, nikaona siku moja nitapoteza kazi halafu sina pakukimbilia wakati natafuta kazi nyingine. Nikaanza ujenzi na taratibu zote halmashauri nilifanya kwa jina langu. Nikajenga vyumba viwili nikaweka na umeme nikahamisha familia. Kwa sasa wana miezi kadhaa nakuwa nawatembelea walau kila mwisho wa mwezi.
Kilichonifanya niandike uzi huu ni kwamba mke analeta jeuri kwenye hiyo nyumba, kwa kiasi fulani amebadilika, maana juzi kati tulitofautiana jambo fulani dogo nikagundua kiburi kimempanda sana.
Pili, sasa hivi anapambana hati iwe kwa jina lake. Kwa sasa tuna harakati za kuweka maji anajitahidi ajaze fomu yeye kwa jina lake na pia juzi nililipia hela B con na imewekwa sasa yeye anataka kujiandika kama mwenye nyumba.
Ebu naomba ushauri wenu nimuache ajiandike? Nia yangu mimi ni kulinda ndoa yetu, maana naona yeye kama akipata umiliki atanisumbua na tutasababisha mgogoro utakao wasumbua watoto wetu.
Ebu naombeni ushauri kulingana na uelewa na uzoefu, maana mimi kama baba mwenye nyumba ni wajibu wangu kulinda familia yangu, wakina mama wanadanganyika haraka sana. Natarajia kumpiga marufuku harakati zote kwa mamlaka niliyonayo ila nasubiri ushauri wenu.
Asanteni.
Soma mrejesho wa kisa hiki: Mrejesho: Mke wangu anataka kuandika jina lake nyumba niliyoijenga