Mtego wa Noti
JF-Expert Member
- Nov 27, 2010
- 2,591
- 1,599
Wahenga wanasema ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni....!!!
Rafiki yangu wa karibu sana jana kidogo agongwe na magari baada ya kumfuatilia mke wake kwa umakini zaidi na kugundua kuwa mkewe anahusudu sana na anashiriki katika mambo ya kishirikina. Kwa sababu mke wake huyo anafahamu kuwa mumewe hapendi haya mambo ya kishirikina, basi ilibidi ayafanye kwa tahadhari sana ili kuhakikisha kuwa mume wake hafahamu kinachoendelea.
Mumewe alikuwa anahisi kuwa mkewe anashiriki ktk mambo hayo. Mambo yalikuja kuharibika pale mumewe alipomtegea vitu vya kunasa sauti katika maeneo ya nyumbani na maeneo ambayo mkewe anafanyia kazi zake na kushitushwa na mawasiliano ya kulipana pesa baina yake na mganga wake huyo.
Baada ya mumewe kugundua hivyo na kupata ushahidi wa sauti, mkewe alijitetea kuwa anajilinda mwenyewe na anashughulikia afya yake na kuwa eti hana mpango wa kumdhuru yeye.
Anasema mkewe baada ya kuona ishu imevuja kaomba msamaha na kuahidi kuwa hatafanya tena upuuzi huo. Mume anasema haamini maneno hayo, anadai labda mkewe anasema hivyo ili kujipanga zaidi na kuhakikisha kuwa nyendo zake hazivuji tena.
Sasa jana rafiki yangu huyo kaja povu likiwa linamtoka akisema kesha mzaba mkewe vibao kadhaa na anafikiria kuachana naye. Kaniomba ushauri afanye nini maana keshachanganyikiwa baada ya kugundua kuwa mkewe amekuwa akifanya mambo hayo behind the door!
Kaja kuniomba ushauri na mimi nikaona sio vibaya nikaliweka hapa jamvini ili watu waweze kunisaidia kumshauri rafiki yangu katika kipindi hiki kigumu!