MKE wangu ameridhia kununua Robot wa kike ili awe MKE Mwenza, nimkubalie au nikatae?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
Kwema Wakuu!

Hayawi hayawi sasa yamekuwa. Hakika ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni.
Baada ya tangazo LA ajabu la kubuniwa Kwa ma-Robot ya kike yenye mvuto WA kimapenzi, kumbe MKE wangu nayo aliyaona hayo madude.
Kwanza aliyasifia Sana ingawaje ni kiwivuwivu Mimi nikibaki kwenye msimamo Mkuu kuwa hayo ma-Robot kamwe hayawezi kumshinda yeye Kwa uzuri, kauli ambayo ilimfanya afurahi Sana. Ni kweli MKE wangu ni mzuri Sana hilo halina ubishi, lakini muundo wa Ile midoli kumbe mpaka yeye imempagawisha.

Nikamwambia, unajua Mimi ni kuhani, Mtibeli, na Sisi Watibeli hatuwezagi kufanya mambo ya namna hiyo. Hata kufikiri tuu uchafu wa Aina hiyo kwetu ni mwiko. Lakini yeye akasema Elon musk amekuwa Mkombozi Kwa kupunguza wanaoninyemelea, kwani tayari ameshaandaa bajeti ya Pesa kwaajili ya kununua Robot MKE kwaajili ya kujipa kama Zawadi.

Madai ya MKE wangu mpaka kufikia Kuninunulia MKE Robot ni haya;

1. Bora MKE Robot kuliko kuwa na michepuko binadamu, ambayo inaloga, na hataki familia yake(mumewe) nilogwe.
MKE Robot hataiangamiza familia yake Kwa Magonjwa ya zinaa kama Ukimwi, Gino, na UTI za kijinga. Ameshambulia zaidi kuwa michepuko ya kibinadamu inamagonjwa.

2. Robot wakike Hatakula Pesa ya mumewe.
Unajua MKE wangu ni MTU wa Kaskazini. Pesa Mbele kama mimba(kama inavyoripotiwa vijiwe nongwa). Anasema kuwa michepuko itaitia familia hasara. Inanjaa Sana. Anamtaja Mke Robot kama kipenzi chake Kwa kuja katika Wakati Sahihi. ATI Taikon sitahonga nje zaidi ya kuli-charge tuu kwenye umeme.

3. MKE Robot hataleta vitoto vya nje ya Ndoa.
Akili za MKE wangu anazijua mwenyewe. Anasema yeye kama MKE wa Ndoa anajua maumivu ya kuletewa Watoto wa nje. Anaungana na Wanawake wengine Duniani kununulia Waume zao midoli kwaajili ya kusaidiaishu ya mahusiano.

4. Hakuna mambo ya kugombania mirathi Kwa MKE Robot.
MKE wangu anasema MKE Robot ndio mpango mzima. Anasema hata nikitangulia Mbele za Haki yeye atabaki salama, tena anaweza Kupata faida ya kumuuza MKE Robot Kwa MTU mwingine na kujipatia kipato. Kuliko kupambana na MKE Mwenza binadamu katika mgawanyo wa mirathi.

5 MKE Robot Hana mawazo mabaya kama michepuko ya kibinadamu.
Namnukuu" unajua MKE Robot hana Wivu, na wala chuki kama walivyo hawa kina nchokonole. Tena nitamsuka, nitamuogesha na kumpamba ili Mume akija ajimalize mwenyewe" Tobaa! Hivi hizi ni Akili au matope. Hivi kweli MKE wangu wewe ndio unaongea hayo?.

Licha ya kumkatalia mpaka basi huku akinitaka nimpe facts za kumkatalia, nikasema dini hairuhusu, akanambia nimpe kifungu au nukuu Kutoka kitabu chochote kikuu cha kidini. Kwa kweli sikupata. Nilimwambia hiyo ni zinaa, akaniambia zinaa Kwa namna ipi? Nikamwambia Robot sio Binadamu, akaniambia licha ya ubishi wangu ataniagizia moja ya pisikali za kirobot zilizonyooka aziweke ndani.

Anajua Ipo siku isiyo na jina nitainyemelea Mimi Mwenyewe akiwa hayupo. Nimemkatalia.
Nimemuambia siku akileta huyo MKE mwenzake ndoa itavunjika, akasema Sawa tutaona. Nimemuambia anipe hizo hela nifanyie mambo mengine akasema hanipi.

Sasa tumenuniana kisa ma-Robot ya Ellon, ngoja nitafukuza Mimi. Sitakubali kuletewa chakula na chakula kingine. Huo kwangu nitauhesabu kama mtego.

Hii ni Karne ya 21, fikra za Zama hizi Kwa kweli zinastaajabisha.
Acha nipumzike SASA.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Chai
 
Kwa mazingira yetu mke roboti ni gharama kubwa sana kumnunua na kummiliki kuliko mwanamke binadamu.

Wanawake ni cheap sana mazingira yetu.

Huyo mke roboti anauzwa hela nyingi zinazotosha kujenga nyumba kabisa ya kisasa.. huku mademu mitaani unawapata kwa bei mbuzi tu
 
Hiyo sio sababu kwangu.
Pesa zipo na Kwa wasiokuwa nazo zinatafutwa.
Ishu ni maadili hayaniruhusu kulala na midoli. Hapo ndipo hoja ilipo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom