pumbatupu
JF-Expert Member
- Jul 20, 2011
- 256
- 82
Jamani JF hebu nisaidieni,kuna mke wa mtu ananipenda, yaani kanitamkia mwenyewe kwamba nafanana na mumewe aliye masomoni nje ya nchi. Nilipomuuliza zaidi anataka nini akaniambia kwamba nimpe kampani kwa sasa kwamba hata mumewe akifahamu hawezi kumlaumu kwa sababu nimefanana naye sana. Kiukweli naogopa make hata mie nina mke lakini siku zinavyokwenda nahisi nitashindwa kustahimili. Make twafanya kazi pamoja na ni mtu wa nyumbani ambaye kila mtu amezoea kutuona tukiwa pamoja. Hebu wanaume na wanawake wenye kuyajua mambo nishaurini niupukeje huu mtihani..walaaaah mgumu...