Mke wa JK akumbana na mauzauza

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
22nd October 2009

SalmaJK%281%29.jpg

Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete

Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, amejikuta akikumbana na mauzauza ya aina yake katika ziara yake ndani ya wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro baada ya wananchi kibao kuzomea mfululizo, kisa kikiwa ni kumpinga mbunge wa jimbo lao la Ulanga Magharibi, Dk. Juma Ngasongwa.

Mauzauza hayo ya zomeazomea kwa mbunge (Ngasongwa), mbele ya mke wa Rais, yalitokea jana wilayani humo, ikiwa ni mara tu baada ya wananchi kutajiwa jina la Dk. Ngasongwa.

Kwa ujumla, sakata lenyewe ambalo aibu yake ilizidi maradufu baada ya wanafunzi kibao wa shule za sekondari kuungana na watu wazima katika kuzomea lilikuwa hivi:

Kwanza, Mama Salma na msafara wake waliwasili katika Tarafa ya Malinyi kwa ajili ya kuendelea na ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli mbalimbali za maendeleo ya wanawake wilayani Ulanga.

Kama kawaida yake, Mama Salma alipokewa kwa furaha, chereko na na watu kibao waliofurika kumshuhudia wakati akiendelea na shughuli zake, ikiwa ni pamoja na kugawa misaada ya vifaa vya afya katika kituo cha Afya cha Mtimbira ambacho hutoa huduma kwa wajawazito.

Wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo vya afya kwa kituo cha Mtimbira, ndipo mauzauza yalipotokea, mara tu baada ya Mkuu wa Wilaya ya Ulanga,
Dk. Rajabu Rutengwe kumtambulisha Ngasongwa.

Mkuu wa Wilaya alipolitaja tu jina la Ngasongwa, umati wa watu uliokuwepo ukalipuka ghafla kwa kelele za kuzomea bila kukoma, huku wengine wakipiga miluzi ya kebehi.

Hata hivyo, mbunge huyo hakuwepo kwenye hafla hiyo huku taarifa nyingine zikidai kuwa machale yalishamcheza kitambo, kwani awali alionekana akishiriki mapokezi ya Mama Salma na kuongozana naye hadi katika tarafa hiyo.

Baadaye tena, wakati Mkuu wa Wilaya akisoma taarifa ya maendeleo wilayani humo na kumtaja Ngasongwa, wananchi walilipuka tena na kuzomea kwa jazba, huku wakipinga hatua ya kutajwa tajwa kwa mbunge huyo waliyedai hana msaada wowote kwao.

Hali hiyo ilielekea kuvuruga utaratibu na kumfanya Mama Salma aingilie kati na kumfanya Mkuu wa Wilaya aseme 'Mtimbila oyeee...!'.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya, pia alishangazwa na wananchi hao ambao walizomea kwa nguvu pale naye alipolitaja jina la Ngasongwa.

"Hana msaada kwetu... hayupo pamoja nasi na siku zote hujitokeza pale viongozi mbalimbali wanapofanya ziara zao huku, wakiondoka naye haonekani... nadhani ndio maana watu wanazomea kila wanaposikia jina lake," akasema mmoja wa wananchi waliokuwepo kwenye hafla hiyo.

Kama hiyo haitoshi, tukio kama hilo pia lilijitokeza tena katika Shule ya Sekondari Kipingo wakati Mama Salma alipotembela na kugawa zawadi ya jezi kwa moja kati ya shule nane ambazo wanafunzi wake walikusanyika hapo (Sekondari ya Kipingu) kwa ajili yake.

Mama Salma alikutana na mauzauza hayo pale alipowaambia wanafunzi wa shule zote nane ambao walikusanyika kwa ajili yake kuwa hakutegemea kama angekutana na shule zote, hivyo akaahidi kukabidhi jezi nyingine kwa mbunge wao.

Dk. Ngasongwa au Mkuu wa Wilaya ili waliokosa nao wapate jezi hizo.
Wanafunzi hao ambao idadi yao ilizidi 500, bila kuchelewa, nao wakazomea kwa nguvu pindi alipotajwa Ngasongwa ambaye kwa wakati huo alikuwepo jukwaani.

Wanafunzi hao walizomea baada ya Mama Salma kusema zawadi nyingine za shule saba, atamkabidhi yeye (Ngasongwa).

Hata hivyo wanafunzi hao walikataa zawadi zao asipewe mbunge na badala yake ampatie Mkuu wa Wilaya (Dk. Lutengwe) ili awafikishie.

Ili kuua soo, Mama Salma aliingilia kati na kutumia busara, akisema kuwa atampatia seti mbili za jezi Dk. Ngasongwa ili azigawe kwa baadhi ya shule na nyingine atampa Mkuu wa Wilaya kama walivyotaka wanafunzi hao.


CHANZO: ALASIRI
 
huko ulanga kazi wanayo mwaka huu..PREZIDA alikuwa huko august,Mizengo Pinda Peter Kayanza alikuwa huko last week ,now mama mwenye kaya..hahaaaaaa
 
Yup...ni kawaidamtu kuvuna anachokipanda!
Huyu bwana anaonyesha kwamba kwanza hawatembelei wananchi wake, na anaahidi ahadi za uwongo.

Lakini pia huyu mtu ni wa siku nyingi, bila shaka umakini wake umeshapungua kwa kasi kubwa , kiasikwamba wanaona wazi kwamba hawafai tena!
Asome ishara za nyakati huyu!
 
tatizo huyu ni mwizi sana wa kura hata kama iweje lazima atatangazwa mshindi..it is true kuwa wananchi hawamtaki kabisaaaaaa
 
Changia basi kidogo JF wewe wasiliana na Maxence Melo, Mkono mtupu haulambwi...

Mkuu tangu upande ngazi na kuwa premium member habari zako zimekuwa nyingi humu ndani!

Nilishawahi pitia mfumo mzima wa kulipa ila nikaona mambo ya matumizi ya visa card na mambo mengine kidogo sikupenda maana sasa ni kuanza kuji-expose wakati my privacy is of paramount importance!
 
Mkuu tangu upande ngazi na kuwa premium member habari zako zimekuwa nyingi humu ndani!Nilishawahi pitia mfumo mzima wa kulipa ila nikaona mambo ya matumizi ya visa card na mambo mengine kidogo sikupenda maana sasa ni kuanza kuji-expose wakati my privacy is of paramount importance!

Si hivyo mazee kuna njia mbadala wewe mwandikie tu invisible PM, hakuna anayetaka kudisclose ID yake....kama uko bongo unanunua sim card nakutuma vocha ukimaliza unaiweka kwenye dustibin...unakuwa umeisha changia JF badala ya kusema oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Si hivyo mazee kuna njia mbadala wewe mwandikie tu invisible PM, hakuna anayetaka kudisclose ID yake....kama uko bongo unanunua sim card nakutuma vocha ukimaliza unaiweka kwenye dustibin...unakuwa umeisha changia JF badala ya kusema oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

Hahaha!

Well said!Wii follow your advise!
 
"What you want is what you see" aliyataka mwenye wewe unaomba kura uwatumikie wananchi halafu huwajibiki, wanafikili wananchi watakua wanawangalia tu lazima wananchi waonyeshe hasira zao wamechoka sasa.
 
mambo ya wabunge kuishi Dar, kusahau majimbo yao...na kwenda majimboni mwao kutafuta kula tuu, tena wengine hata uwaziri ambao ndio unakuwa kisingizio hawana...basi tu
 
Wote wanapima upepo mwaka 2010 ni maeneo mengi watashangaa hakika .Chadema wazidi kujiweka sawa tu .CCM wanapima upepo ndiyo maana unaona harakati zote . Au kuna madini huko nini maana inawezekana wanatafuta namna ya kuwahamisha wana Ulanga ?Maana bwana wawekezanji ndiyo wenyewe
 
ilikuwa raha tupu....kwa kweli...huko mtimbira ngasongwa ahesabu maumivu 2010
haikuanza leo hiyo hali huko mtimbira, 1995-2000-2005 ni mtimbira na baadhi ya watoto wanaoota utukufu, mwandishi afanye home work yake vizuri ili jamii ifahamu kwanini mtimbira na wanafunzi na ni kwanini kila unapokaribia uchaguzi!!!??

Ahadi wakuu ni za ccm, na ni wajibu wa ccm kutetea mafanikio yao na kukiri makosa yao kwa pamoja.

Big up mama salma, jk, pinda.

Todate they need ngasongwa kwani waliojitokeza kama yassin njayagha, ngonyani na wengine hawana majibu ya haraka na yenye maono juu ya matatizo ya ulanga west ukilinganisha na huyu alhaj ngasongwa.

Kazi ipo 2010 lakini si ngumu kama mnavyodhani sasa.

Mwandishi arudi kule na kuifanya home work yake vizuri wakati hawa wakuu hawapo ziarani, ninaamini tunalo la kujifunza katika siasa za ulanga in general. Ilianza kabla ya uhuru na imeendelea kuwa hivyo baada ya uhuru.

kilimo kwanza wananchi.
 
They have nothing to change, tumechoka na mauzauza ya kipuuzi. tena wawe makini na mawe this time watatupiwa, ulinzi kwa nchi hii ni mdogo sana.
 
Wote wanapima upepo mwaka 2010 ni maeneo mengi watashangaa hakika .Chadema wazidi kujiweka sawa tu .CCM wanapima upepo ndiyo maana unaona harakati zote . Au kuna madini huko nini maana inawezekana wanatafuta namna ya kuwahamisha wana Ulanga ?Maana bwana wawekezanji ndiyo wenyewe
Hahahaaaa, hahahaaaaaaaaaa Lunyungu, kazi ipo Muraa

Tatizo ni vijisenti vya kukodisha wazomeaji ili kuhalalisha agenda yao ndani ya Ze-comedy 2 weeks ago,

Waliandaa mashabiki wao pale mtimbira na wanafunzi wameanza kuhusishwa na mkakti wa kummaliza Ngasongwa katika uso wa wakuu wa nchi, walishindwa kwa Shein na Jk ila timing imekubali kwa Mama Salma ingawaje naye amewastikia maana familia ya JK imeanza kuhusihwa na waliojitokeza sasa Mama alienda kwa shughuli zake na pia kuuona ukweli huo.

Tunataka maendeleo na si umri wala sura ya mtu wakuu.

Kilimo kwanza wakuu
 
Back
Top Bottom