Mke wa jirani yangu ananisumbua

Nduka Original

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
1,012
816
Nimueleweje huyu mke wa jirani yangu. Mimi nimeoa na pia familia zetu ziko karibu sana ila simuelewi jirani yangu. Siku hizi anavizia nikiwa natoka asubuhi akisikia gari anatoka getini na kuniletea either matunda au chochote kile. Wiki end hii kaniletea bukta eti anasema ya kulalia. Je nifanyeje nimwambie mke wangu?
 
........ Je nifanyeje nimwambie mke wangu?
Mke anajua kuwa kwa wale ulio wakatalia unamwambia, Je wale mliokubaliana, mbona huwa humwambii???? Hata yeye atakuwa anakwambia wanaume wanao msumbua hasa wale tu aliowakatalia, mbona wale aliowakubalia hakwambii????????
 
Na wewe uepewa bukta unapokea? Halafu unajiuliza umwambie mkeo????? Loh.......
 
Mke anajua kuwa kwa wale ulio wakatalia unamwambia, Je wale mliokubaliana, mbona huwa humwambii???? Hata yeye atakuwa anakwambia wanaume wanao msumbua hasa wale tu aliowakatalia, mbona wale aliowakubalia hakwambii????????

Hilo nalo neno! Binafsi nimekuwa nikitafakari sana hii issue ya mke kukuhadithia waliomtongoza, naona kama inakuwaga magumashi vile!
 
Ninga ningali nimepatwa na muadharax2,shetani akaniambia katwuaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!
 
shame on her...sasa asubuhi asubuhi anamuacha mumewe na kukuletea wewe bukta! mambo mengine bana,
 
Mwambie mkeo akusindikize ukitoka getini Kama mara 3 ivi na mabusu Kama njiwa akiona hayo hatorudia tena,na wewe hujui kusema ahsante na usipokee?

Kwani huyo mke wa jirani hajui kwamba jamaa ameoa...? Swali la pekee ni kumuuliza mtoa mada, je dhamira yake inamwambiaje?
 
sjui kwnn bahati kama hizi huwa hazitokei..! ingekua mm hata kama angekua halipi aisee angelipia tu gharama za 'usumbufu na uendeshaji'
 
We unapewa bukta na unakubali!!?? Yaani wanawake wa siku hizi hivi tatizo ni nini? Kuna uhaba wa wanaume au?
 
Mpige picha umuweke hapa anakupa bukta au zawadi nyingine, ama sivyo alinacha tupu hizi za mabwege wanaotamani mitala bila kuweza hata kuwa na mke mmoja.
 
Zamani zetu ningeshauri wala usimwambie mkeo labda ukaombe ushauri kwa mama mzazi......

Sina hakika kama vijana wa siku hiz bado mnawatumia vizuri wazazi wenu!!


Babu DC!!
 
Na baada ya vyoote amuambie mkewe amshukuru mke wa jirani kwa bukta ya kulalia.

Angekuwa na mke mwenye akili ndefu kama mie, namuambia 'jirani asante kwa bukta. Sie hulala bila nguo, so inanifaa mie wakati niko masika. Next time umpe bukta kubwa manake hizi hipsi na wowowo langu havienei'
Mwambie mkeo akusindikize ukitoka getini Kama mara 3 ivi na mabusu Kama njiwa akiona hayo hatorudia tena,na wewe hujui kusema ahsante na usipokee?
 
Back
Top Bottom