MKE: Hivi nini hasa sababu ya kuwa na mke?

hata mie naingia ndoani sababu wenzangu wote wana/meolewa.nataka watoto na sitapenda kuwalea peke yangu as they want both parents.sitapenda kuwa mzee bila kuwa na watoto wa kunisaidia sio utegemezi bali hata kiafya wale wasiokuwa na watoto wanazeeka vibaya'...:smilez:
 
Kuna msemo wazungu hupenda saana kuutumia.wanasema

in africa children are the retirement pensions......
 
mke......a best friend...
a soulmate....
someone who is a bit special in ur life...
someone you run to for advice or for comfort...
someone to trust
...Dah! nina jamaa yangu anamuona mke wake ni zaidi ya pilato....jamaa kwa karibu mwaka wa 3 sasa hataki kuchukua likizo anaona nyumba yake kama kituo cha polisi.
 
Ndoa ni mpango wa Mungu. m'me ataachana na wazazi wake, naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa si wawili tena bali ni mwili mmoja. vivyo hivyo m'ke ataachana na wazazi wake naye ataambatana na mumewe.
 
mke......a best friend...
a soulmate....
someone who is a bit special in ur life...
someone you run to for advice or for comfort...
someone to trust
Exactly The Boss, hiyo ndo sababu muhimu ya kuoa/kuolewa. hayo mambo ya kupikiwa, kuguliwa, KUPATIWA WATOTO mtu yeyote anaweza kukufanyia sio lazima awe mkeo/mumeo. na ndio sababu hayo yote niliyoyataja wanaweza kutokea ndani ya ndoa still wanandoa wakaendelea kubaki kama wanandoa, hapa nina maana, tunashuhudia ndoa nyingi zina watoto wa nje ya ndoa, kuna wadada wa kutusaidia kupika, kufua nk lakini mke anabaki kuwa mke (someone you can run to and get comfort)
 
Kwa akina kaka/baba waliooa au wanaotarajia kuoa.
Mmeoa au mnataka kuwa na mke ili iweje?

Naona baadhi ya wanaume wakidai huduma mbalimbali
  • kuanzia kupikiwa,
  • kufuliwa,
  • kuoshewa vyombo,
  • kutunziwa na kulindiwa nyumba,
  • kuburudishwa nakadhalika. Hapo sijaongezea
  • kuzaliwa watoto na matunzo yake,
  • kutunza wazazi wazee au wasiojiweza,
  • kuhudumia miradi na mifugo.
    Nadhani siyo vibaya kuwa na uelewa wa pamoja katika hili.Huenda itasaidia katika management of expectations na pia kurekebisha pale ambapo hapako sawa kwa wote.
    Hivi kweli mke ni kwa ajili hii? Hebu tupate mawazo kutoka kwenu. Akina dada/mama mnaweza kuchagiza.
...La hasha! nilipotamani kuoa halikunijia wazo eti mke atanifanyia hayo tajwa hapo juu. Ilikuwa ni sababu ya Mapenzi tu! ili awe wangu, wangu peke yangu. Hayo mengine ni matokeo tu.
 
We are "half" in many aspects...:psychologically,emotianally,physically,etc....we need the other half to have a balanced equilibrium in those aspects of life.In no way naweza kuishi bila kuhitajia the other half....provided siwezi kuzini hence I must get married
 
...La hasha! nilipotamani kuoa halikunijia wazo eti mke atanifanyia hayo tajwa hapo juu. Ilikuwa ni sababu ya Mapenzi tu! ili awe wangu, wangu peke yangu. Hayo mengine ni matokeo tu.

Mbu umesema kweli, mengine ni matokeo tu!
 
Kama walivyosema wengine sababu kuu ya kuoea/kuolewa ni kuwa na mwenza wa kudumu, kupendana na kutunzana. Hizi huduma ulizozitaja (kwenye red) kwa kweli ni expressions tu za huko kupendana na kutunzana kati ya wawili wa ndoa. Na hizi expressions zinategemea sana utamaduni wa watu na wakati, ndiyo maana huduma hizo zinatofautiana kutoka jamii moja na jamii nyingine. Lakini pia zinabadilika kutokana na kupita kwa wakati, elimu ya wahusika, nk. Kwa maneno mengine hizi expressions za companionship and love ni vitu very dynamic. Ndiyo maana leo hii kutokana na wakati na elimu mengi ya zamani yamebadilishwa au kuboreshwa katika jamii zetu kuhusiana na mahusiano ya mume na mke kwani mengi ya hayo yalikuwa yanamtumikisha mwanamke na kumpa upendeleo mwanaume.

Nimefurahishwa sana na hitimisho lako kuhusu huduma hizo nilizozitaja kuwa ni expression of love!
Inakuwaje basi mtu anaposhindwa ku express love kwa namna.mtindo huu wakati mwingine inamgharimu maisha? Tumesoma/kusikia mwanaume akimpiga na wakati mwingine kumuua mwenzi wake kisa ati alichelewa kupika, hakufaya jambo fulani etc.
 
Nimefurahishwa sana na hitimisho lako kuhusu huduma hizo nilizozitaja kuwa ni expression of love!
Inakuwaje basi mtu anaposhindwa ku express love kwa namna.mtindo huu wakati mwingine inamgharimu maisha? Tumesoma/kusikia mwanaume akimpiga na wakati mwingine kumuua mwenzi wake kisa ati alichelewa kupika, hakufaya jambo fulani
etc.

binadamu ni kiumbe wa ajabu sana, wakati mwingine hufanya kitu bila kujua sababu ya kukifanya na moja ya mambo yanayofanywa maranyingi bila wahusika kujua sababu ya kuya fanya ni kuoa nakuolewa.... kimsingi kila mtu ana sababu zake na si lazima zifananne na sababu za wengine ama sababu zinazokubalika katika jamii. matendo ya kupika, kufua nk. katika ndoa wakatimwingine ndio mapenzi yenyewe na ni halisi kama mapenzi na sio mara zote ni "just" expression of love bali wakati mwingine ni neutral duties zisizoweza kuathiri mapenzi yao kwa namna yoyote ile.

kuna watu wanaoa kwa ajli ya kufanyiwa kazi hizo tu basi, kuna baadhi unakuta kama watoto anao tayari, kama ni accompany hana upweke wa kiwango chochote na kama ni msaada wa maisha hana uhitaji huo kwa kiwango chochte ila anahitaji mtu wa kushughulika na mambo hayo ya kupika usafi , kutunza mazingira, mifugo nk na ambaye atamwamini hadi chumbani kwake na atakayeweza kumhudumia namna yoyote takayotakiwa mfano wakati wa ugonjwa bila kupata vikwazo vya mipaka ya kijamii (social distance). ndoa nyingi za mitala huwa zina maudhui kama haya. na ukichunguza utakuta maeneo ya vijijini amabako "wage labor" haijazoeleka (hasa siku za nyuma kidogo) mitala ilikuwa suluhisho, na kuna wakati hata mke mkubwa humlazimisha mumewe aoe mke au wake wengine ili yeye apumzike hizo "kazi" hasa baada ya umri kuanza kumtupa mkono....

magomvi yanayolipuka atika ndoa kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu hayo yaliyotajwa ni "matokeo" tu ya ugomvi ambao tayari unayala mapenzi yao na si "ugomvi" wenyewe ndio maana utasikia mara nyingi abla ya kipigo kuwa mfano "... we mwanamke siku nyingi nakuona unaanza kiburi, sasa leo nitakuonyesha..." hii inaonyesha kuwa nyumba ilikuwa na utulivu tu wa utambo na sasa hali imetibuka...

nimeona maishani mwangu ndoa zenye sababu tofauti nyingi tu.. kwa mfano,
1.ndoa zinazotaka watoto tu
2. zinazolenga kuthibitisha kuwa wahusika wamekuwa wakubwa
3. zinazolenga kusaidia wanafamilia wengine kwa kuwapa mahari kupunguza umasikini wa familia
4. kusawazisha tofauti za kijamii hasa pale ambapo mfano agemates wote wamo ndani ya ndoa na waahusika wanataka kuingia ili walingane na agemates
5. kupunguza kero toka kwa jamii kuwa "utaoa lini?"
6. uthibitisho wa kutokuwa na nuksi maishani (hasa kwa wasichana)
7. kudhibiti tamaa za mwili
8.nk

so mjadala ni mpana na mrefu, sababu ni multidimensional......
 
Kwa akina kaka/baba waliooa au wanaotarajia kuoa.
Mmeoa au mnataka kuwa na mke ili iweje?
Naona baadhi ya wanaume wakidai huduma mbalimbali kuanzia kupikiwa, kufuliwa, kuoshewa vyombo, kutunziwa na kulindiwa nyumba, kuburudishwa nakadhalika. Hapo sijaongezea kuzaliwa watoto na matunzo yake, kutunza wazazi wazee au wasiojiweza, kuhudumia miradi na mifugo.

Nadhani siyo vibaya kuwa na uelewa wa pamoja katika hili.Huenda itasaidia katika management of expectations na pia kurekebisha pale ambapo hapako sawa kwa wote.
Hivi kweli mke ni kwa ajili hii? Hebu tupate mawazo kutoka kwenu. Akina dada/mama mnaweza kuchagiza.
Wakati utakapofika wa kuolewa you will understand the whole meaning of marriage! Hayo unayoyasema ya kufuliwa sijua kuburudishwa they trivials, haileti tabu hata kidogo au kuwa second thought when it comes kumfulia mme/mke unayempenda!

Katika context ya kiblia ndoa ni kiini cha upendo! It is a simulation of the great God's LOVE being reduced to a family level parants acting as small gods yaani upendo kwa vitendo. Jinsi baba au mama anavyohangaika bila maswali kulinda na kuilisha famila yake ndivyo baba yetu wa mbinguni anavyotulinda na kutulisha kama famila yake Kama mwanadamu tu mwenye mapungufu yote haya unaweza mpa mtoto wako mkate wala sio jiwe, samaki wala sio nyoka....! Mambo haya huwezeshwa tu na strong bond inayoitwa upenda! Ukianza kuhoji kwa nini namfulia, nampkia namburudisha ujue upendo wako una doa! Love does not ask why!!!!!!!!!!!
 
Jana nilihudhuria ibada takatifu ya ndoa ya RC. Padre alichonga mno! Kawaambia kwa dhati kabisa wanandoa wapya na wa zamani kuwa ndoa si kitu rahisi. Wasifikirie wanaingia kwenye mteremko bali kwenye maisha ya kuvumiliana. Kwamba ukweli, kuheshimiana na kuaminiana katika yote hasa katika KUJAMIIANA. Pia kazi kubwa ya wanandoa ni kutakatifuzana ili mwisho wa siku kila mmoja aione pepo na si kukwazana kama ilivyo sasa. Tatizo siku zote litabaki kwenye utekelezaji wa hayo
 
...aaarrgghh,
anasema tu huyo. (kumradhi Roman Catholics 'wenzangu')
Angeruhusiwa kuoa na kuujua 'moto' wake hata yeye angeisamehe hiyo 'one way ticket' to Peponi.
 
Wakati utakapofika wa kuolewa you will understand the whole meaning of marriage! Hayo unayoyasema ya kufuliwa sijua kuburudishwa they trivials, haileti tabu hata kidogo au kuwa second thought when it comes kumfulia mme/mke unayempenda!

Katika context ya kiblia ndoa ni kiini cha upendo! It is a simulation of the great God's LOVE being reduced to a family level parants acting as small gods yaani upendo kwa vitendo. Jinsi baba au mama anavyohangaika bila maswali kulinda na kuilisha famila yake ndivyo baba yetu wa mbinguni anavyotulinda na kutulisha kama famila yake Kama mwanadamu tu mwenye mapungufu yote haya unaweza mpa mtoto wako mkate wala sio jiwe, samaki wala sio nyoka....! Mambo haya huwezeshwa tu na strong bond inayoitwa upenda! Ukianza kuhoji kwa nini namfulia, nampkia namburudisha ujue upendo wako una doa! Love does not ask why!!!!!!!!!!!

Hapo kwenye bold pamenikuna sana! Asante kwa ushauri.
Nikirudi kwenye michango ya wengine, nadhani zaidi ya asilimia 80 ya wanaooana hufanya hivyo kwa shinikizo na siyo kwa vile walipanga toka awali kuwa nitaoa/kuolewa kwa vile nahitaji mwenza, au nitakuwa ninampenda mtu sana hadi niwe siwezi kuishi bila yeye, au kwa vile nitakuwa nahitaji watoto, au kwa vile umri wangu utakuwa umeenda.
In short most marriages husababishwa na "shinikizo fulani"....and this explains why most couples are so unhappy in their marriages.
 
naishukuru ndoa kwa kunisaidia ku loose weight, kitambi chote kimetoweka bila kwenda GYM. wale ambao wana tatizo la overweight ningewashauri wajitose kwenye ndoa haraka iwezekanavyo.
 
Mimi dhumuni langu la kuoa litakuwa ni kupata mwenza/ mwandani wangu ambaye tutashirikiana naye katika kusafiri safari ya maisha na kujenga familia

Mimi hayo siafikiani nayo. Mtu ninayempenda siwezi kumdai yote hayo. Nitamdai penzi tu basi. Ndoa ni kushirikiana. Sioni ubaya wowote wa mimi kuingia jikoni na kukorofisha na siku zingine yeye anaingia na kukorofisha. Nafanya hivyo sasa nikiwa bado mseja na endapo ikatokea nikaja kuoa sitabadilika. Nitaendelea kupika, kufua, na kufanya usafi. Na hapa kwenye usafi ndio kabisaaa simwamini mtu. Mimi niko msafi kupitiliza na huwaga simwamini mtu mwingine anifanyie usafi.

Kwenye watoto mwanamke hanizalii. Tunazaa wote ingawa yeye ndio atabeba mimba. Lakini kama mimi ndio baba mtarajiwa basi nitakuwepo kila hatua ya huo ujauzito. Muda ukiruhusu tutaenda wote kwenye madarasa ya Lamaze na mambo mengine yahusuyo ujauzito wake nitashiriki. Sio sawa kumwacha mwenzio ahangaike peke yake kama vile alijipa mimba mwenyewe.

Matarajio yangu ni penzi la kweli tu. Nikilipata hilo basi mengine yatajipa. Shida inakuwa utajuaje kama mwenzako anakupa penzi la kweli? Huo ndio mtihani haswa.
Mke sio kwa ajili ya hayo uliyoyaainisha hapo juu (kwa maono yangu). Mke ni kwa ajili ya kuishi pamoja na kufurahia maisha. Siwezi kufurahia maisha kama mke wangu hana furaha.

I salute mkuu!!
 
naishukuru ndoa kwa kunisaidia ku loose weight, kitambi chote kimetoweka bila kwenda GYM. wale ambao wana tatizo la overweight ningewashauri wajitose kwenye ndoa haraka iwezekanavyo.

...ha ha haaaha... pia sababu ya kufa mapema kwa maradhi yasiyoambukiza ila ya kujitakia kama BP, kisukari, Stroke na Heart attacks!
 
Mimi nilioa baada ya kufika mahali nilipoona kwamba ni mpweke na kuwa nahitaji mtu mwingine wa kukaa naye atakayefanyika faraja katika maisha yangu. Mtu ambaye atatimiliza haja ya moyo wangu ambayo nikiwa mwenyewe siwezi.

Kumbuka mambo mengi uliyoorodhesha kama sababu ya kuoa/kuolewa mhusika anaweza kuyafanya lakini yako mengine yasiyowezekana mpaka awe na mwenzake. Kwa hiyo maisha ya ndoa ni sehemu nyingine muhimu sana ya maisha ya mwanadamu ambayo wawili hao wanapaswa kuishi kwa AMANI, FURAHA, UPENDO NA UVUMILIVU. Kila mmoja anapaswa kumtegemea mwenzake na wawili hao wasaidiane kwa kila jambo.
 
Back
Top Bottom