Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Mwanaume kimaumbile hataki kuona aina ya mashindano na mke. Anapogundua kuwepo kwa aina ya mashindano, huwa anajitahidi sana kuhakikisha kwamba, anashinda. Katika juhudi yake ya kutaka kushinda ndio hapo anapofanya vituko vikubwa na vya ajabu zaidi. Mwanamke anashauriwa kuhakikisha kwamba hampigii magoti mwanaume, bali anaepuka kushindana naye. Mwanaume anaweza kumuudhi mwanamke, badala ya mwanamke kusema, ‘mwache tu,' na kuanza kufanya vituko kama kumkasirikia, kutomjali, kuonyesha kwamba hata yeye ni ‘mbabe,' anatakiwa kuonyesha kukerwa kwake kwa kiwango cha mumewe kujua kwamba amemkera. Baada ya hapo aendelee kufanya mambo yake kama vile hakujatokea jambo.
Kwa mfano mume ametoa majibu yasiyopendeza kwa mkewe, mke anaweza kumwambia mumewe kwamba hajaridhishwa na majibu hayo. Bila kujali mume amejibu nini, mke anatakiwa kuendelea kufanya mambo yake kama vile halijatokea jambo lolote. Kama mume ni muungwana, hatakaa kimya, baada ya muda atamuomba mke radhi. Mwanamke yeyote anaweza kujaribu jambo hilo leo.
Kwa hiyo mwanamke anatakiwa kujua ‘ubabe' ndiyo asili ya mwanaume na upole na upendo viko ndani ya damu ya mwanamke na ndio maana huwa inasemwa kuwa, kama mwanamke akitaka anaweza kumfanya mumewe akafuata kila anachomwambia (kwa manufaa ya wote)kwa kutumia silaha yake ya upole na upendo. Lakini ni wanawake wangapi wanaitumia silaha hii? Bila shaka sio wengi na ndio maana wengi hushindwa kulinda ndoa zao.