Mke alihama chumba, nimechukua msichana wa kazi, kuna kosa hapo?

Da sitaki kuamini kama una mke mpoke hivi, yani mtu mmeo atembee na kijitu unaishi nacho ndani, harufu asubuhi kinaamka mnaonana na kinaingia jikoni kinampikia mmeo, kwanini usikivunje miguu. Kwa tafasil hii una mke bora sema tu amepatwa na mstuko tu na ni hasira zitapoa. Sijawahi ona mke mpole hivi angekuwa mwingine huyo binti angekuwa hana pua. Wanawake wengine wamebarikiwa upole do!!
 
Hizi story za kutunga bwana shidaaa.., anyway km ni kweli basi sawa endelea kula vyombo mkuu.
 
Mie nakupongeza sana, wanawake wa namna hii si wa kubeza na kujishusha kana kwamba Fala flan,kumbe hata kahama chumba bado anakupenda, alihis kumkosa yeye chumban utakosa mwanamke wa kulala naye,amebiip wewe ukampigia kabisa,miez miwili ni mingi sana kwanza ulijitahid sana, usishangae yeye and bwana anamkaza huko nje then anarud chumba cha watoto,wewe usiku unajichafua bure, tena angekuwepo pia rafiki yake wa karibu ungemshawish naye ukala mzigo Ili ajifunze akizila wenzie wala bwana, atajilaum badae ukiamua kumuoa huyo binti na yeye akarud chumban kama mke
 
Mmefanyiana huko halaf unakuja kuomba ushauri huku? Nipe namba ya mkeo niusikilize na upande wake halaf ntakuja kukushauri
 
Duuu huyo house girl ni mnafiki na ndo chanzo cha kuisambaratisha ndoa yako anakuchonganisha ili aingie yeye na akimwagiwa maji ndo atashika adabu
 
Katika kitu ambacho sitakaa nikifanye ni mtu kujanirekrbishia ndoa yangu!!!wengi huwa tuangukia pua hapa na ndiyo mwanzo wa kuachana jumla(tulipendana wenyewe hatukumshirikisha mtu na tunagombana wenyewe na tunasuluhisha wenyewe""tunashindwana wenyewe na tuaachana wenyewe "")usijifanye mjuaji kwenye mahusiano ya watu
 
Watu wote waliotushauri wakati fedha zake zimepotea na baadae yeye kuhama, wadhamini wetu ndio walikua wasuluhishi wakuu, kila mara walikuja home kumsihi arudi chumbani kwetu akawa anakubali tukibaki wawili anadai alikua anawafurahisha tu hawezi kurudi

Watu aliotaka yeye watusuluhishe niliwakataa maana walikua ni sehemu ya mgogoro
Unatakiwa kuwa na msimamo wako kama mwanaume rijali usiyumbishwe na watu simamia kile unachokiamini
 
Sa kama umeshajua wewe ni mshindi na mkeo hafai ushauri unataka wa nini tena? Mi nahisi mkeo alishaona we sio na huyo HG mshaanza zaman Haiwezekan uhamie tu chumbani kwake tena mna watoto wanaona aisee sijui wanakufkirije kama baba ni Aibuuuu!
Huyu anafasana (mtoa mada)kuwa komando kwa ujasiri wake vuta picha kama hg asingekuwepo anahamia wapi kama siiyo kwa mtoto ila simlaumu kabisaaaaa yote haya kayataka mkee
 
Arrrg nachefukwa kuna mibaba mingine ina maamuzi ya vivulana,yani kweli umkomoe mkeo kupitia msaidizi???hapo usubiri na mimba tu usipofanya maamuzi ya kumtoa huyo kahaba mwenzio,
 
Nawasalimu wote,

Tangu mwezi February mwanzoni tumekuwa na mgogoro na mke wangu, mgogoro huu ulitokana na yeye mke kupoteza pesa zake za mkopo kiasi cha tshs million sita katika mazingira ya kutatanisha, akadai mimi ndie nimechukua pesa zake, tulipoitwa kwenye usuluhishi niliona niliona ni udhalilishaji hivyo nikagomea vikao vyote

In retaliation akaamua kuhama chumba na kwenda kwa watoto,
hivyo February yote sikupata matrimonial right na March yote pia sikupata.Baadae nikagoma kula chakula chake baada ya accurate intelligence information kuwa kuna dawa kama unga unga hivi huwa anadumbukiza kwenye chakula nilichoandaliwa mimi na mara zote msichana wa kazi hukimwaga kile chakula na kuniandalia kingine, kesho yake wife humuuliza msichana wa kazi baba alikula kile chakula? Pia ameonekana akibeba nguo zangu kadhaa ikiwemo boxer na kuondoka nazo, alipohamia kwa watoto hakubeba nguo zake hivyo kila asubuhi huja kuchukua master bedroom maana ana funguo zake.

Sasahivi sili nyumbani na nguo natembea nazo kwenye gari, mwezi huu wa nne ulipoanza nimehamia chumbani kwa msichana wa kazi ndimo ninapoishi sasa, binti huyu amekuwa mwema kwangu na ananipenda kwa dhati, ni mzuri wa umbo na sura, in fact hakua msichana wa kazi ni ndugu katika ukoo wa mke, alikuwa amefeli form 4 hivyo akaomba huo mshahara wa msichana wa kazi tumpe yeye atusaidie kazi wakati anasubiria mambo yake yakae sawa.

Mke ameniletea watu wa serikali ya mtaa waje wamtoe yule binti, maana nilipohamia chumbani kwa binti, mke alitufanyia fujo isiyosemekana, kwamba binti aondoke, sasa mimi ningeishije wakati mke amehama chumba?
Sasa nafanya utaratibu nimtafutie chumba mtaani, huyu binti ana adabu na ni God fearing tofauti na mke wangu anaejifanya mlokole wakati anataka kunidhuru na madawa.

Naombeni mwongozo wenu katika kukabiliana na jambo hili, na pia mniambie kama nimekosea katika kulishughulikia suala hili.
Pole sana ila ungetueleza kwa umakini hizo pesa zilipoteaje and wewe ulikuwa unahusika vipi kwenye upotevu huo.
Chanzo ni hicho kama ukiwa wazi ni rahisi kukushauri lakini kama sivyo...........
 
Pole sana ila ungetueleza kwa umakini hizo pesa zilipoteaje and wewe ulikuwa unahusika vipi kwenye upotevu huo.
Chanzo ni hicho kama ukiwa wazi ni rahisi kukushauri lakini kama sivyo...........
Ameshaeleza kila kitu, amerudia zaidi ya mara kumi, Rudi page ya kwanza usome hadi ya mwisho utaona maelezo
 
Arrrg nachefukwa kuna mibaba mingine ina maamuzi ya vivulana,yani kweli umkomoe mkeo kupitia msaidizi???hapo usubiri na mimba tu usipofanya maamuzi ya kumtoa huyo kahaba mwenzio,
Msaidizi ni mnyama? Msaidizi sio binadam? Si ajabu ni mzuri kuzidi mke wa mshikaji

Mwanamke uame chumba miezi 2 unaishi kwa watoto halaf leo unipangie nikalale na nani?

Ni mara ngapi tumeona mwanamke ameolewa na tajiri lakini bado anatembea na dereva wa bosi?
Au anampa uchi mlinzi wa getini

Jf kwa pretendency ni balaa
 
Back
Top Bottom