Mkataba wa Bandari: Mbunge Aida Khenani akiri kupelekwa Dubai, lakini mpaka wanarudi hakujua walikwenda kufanya nini

Uzima Tele

JF-Expert Member
Jan 20, 2023
1,101
2,345
Hakika shetani ana trick za ajabu sana anapotaka kutenda au anapotenda uovu wake kwa kuwatumia watu waovu hususani viongozi wenye dhamana kubwa za kuongoza nchi na wananchi wa nchi yetu..

Hebu twende pamoja, soma na sikiliza hii👇👇👇

Mkataba wa DP WORLD ni zaidi ya mkataba tu!

• Kumbe kulikuwa na timu mbili za wabunge. Moja ilienda India (kuzuga tu) na nyingine Dubai (kuliko na mpango mzima wa Rais Samia Suluhu Hassan na Prof. Makame Mnyaa Mbarawa). Aida Khenani yeye akapachikwa kwenye trip hii ya Dubai. Nadhani lengo likiwa ili waovu hawa waje kuwa na hoja kusema "hata CHADEMA walikwenda kule wakiwakilishwa na mbunge wao kuona uzuri wa uwekezaji wa kampuni hii..!!". Aidha bila shaka pia kuwa, ili wamtumie ndani ya bunge kuwa kama shahidi wa upande wa upinzani bunge litakapo - ratify mkataba huu. Kwenda kinyume, Spika Dr Tulia Ackson alionekana kushangaa na kupaniki kikatokea tulichokiona. Mpaka naibu Spika wa Spika ndugu Zungu naye akiwa kama back bencher, alisimama eti kumpa taarifa mbunge huyu!!

• Hauishia hapo, mbunge huyu ndani ya bunge akaendelea kuwashangaza wabunge wa CCM aliposema hakubaliani na mambo haya hadharani ndani ya bunge. Nadhani kimya kimya wakawa wanasonya amekula hela zetu bure huyu. Wakamzonga zonga mpaka akaipata fresh huku Spika Tulia Ackson akiwa amevaa koti la mwanasheria Mkuu wa serikali kujibizana naye, kumtoa hofu😂 na kumshawishi akubaliane na serikali..!

Haya ya Spika Tulia Ackson siku ile kiukweli yalikuwa ni kichekecho na upuuzi wa ajabu sana.. Ama kweli, rushwa hupofusha fikra na ufahamu wa mtu!!

• Walioenda India ripoti yao wala hata haihitajiki kwa sababu wahusika sio wahindi wa India bali ni waarabu wa Dubai ambako kabla huyu anayechaguzwa na kauli ya "nani kama mama" alishatangulia kabla kumalizana na "mfalme" na kuchukua chake mapemaaaa..!

• Hii haina shaka tena kuwa, nyuma ya mkataba huu kati ya DP World & Serikali ya Tanzania kuna rushwa kubwa imetembea kwa viongozi wetu.

• Hata hivyo mimi siamini kabisa kuwa huyu mama anaweza kuwa mbaya na mumiani wa kiwango hiki cha kufikia kuuza kipande cha nchi ya Tanganyika.

Maoni yangu binafsi

Ilisemwa na wahenga, ili nchi yoyote duniani ipate maendeleo ya kweli ya watu wake, lazima mambo haya manne yawepo katika ufanisi wake:

1. Ardhi
2. Watu
3. Siasa safi
4. Uongozi bora

Ukiyatazama hayo mambo na ukimsikiliza huyu mbunge ambaye kwa kweli ukimtazama usoni mwake na kile kitokacho kinywani mwake, hutapata shida kabisa kumwamini.

Ukiachilia mbali uwepo wa ardhi na rasrimali watu, Tanzania tunakabiliwa na tatizo moja kubwa la UKOSEFU WA SIASA SAFI ambayo imezaa tatizo la UKOSEFU WA UONGOZI BORA. Na matokeo yake ni haya tunayoshuhudia leo. Tunaulizanaga, hivi ni kwanini nchi yetu ni masikini hata baada ya miaka zaidi ya 60 ya uhuru? Jibu lake liko wazi sasa... Ukosefu wa uongozi bora wa nchi..!!

Laiti tungekuwa na hayo mambo mawili muhimu zaidi, hiki kinachoendelea sasa kati ya Tanzania na DP World, kisingekuwepo maana tungekuwa na viongozi walio madarakani wenye akili, ufahamu, hekima na busara na kujitambua.

Lakini kwa mkataba huu wa DP WORLD, inadhihirisha wazi sasa kuwa kumbe tuna viongozi wajinga, wasio wazalendo wa taifa lao, waliojaa tamaa ya kujilimbikiza mali kwa rushwa na kuwa tayari kujiuza kwa vipande vya fedha, wabinafsi, wala rushwa na wanaojipenda wenyewe na matumbo yao na hawa kamwe hawajawahi kutupenda sisi wananchi wa Tanzania..!!

Sara yetu wote ni:

Mungu wetu uliye juu mbinguni muumba wa mbingu na nchi na vyote vilivyomo tutie nguvu tupambane na hawa mumiani wanajiita viongozi wa nchi ya Tanganyika lakini kumbe ni mashetani katika sura za binadamu.. Amina

Rais Samia Suluhu Hassan katukosea sana Watanganyika kwa hili la mkataba wa DP WORLD kumuuzia bandari zetu zote za bahari na maziwa ya Tanganyika huku akiacha za kwao Zanzibar mikononi mwa Wazanzibari!
 
Mimi naona katika kila awamu ya bunge ya miaka mitano basi wabunge huwa wanakwenda nje ya nchi kwa mambo mbali mbali. Na wala siyo ajabu kuwa wengine wamekwenda Dubai na wengine kwenda India.
 
Sipingi huja ya mbunge lkn Kuna shida nyingine naiona kwa sisi wa bongo.
Hivi mbunge atoke Tanzania hadi Dubai hajui alienda kufanya nn? Hatupo serious kiasi hiki kweli?

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
Amenisikitisha sana huyo mbunge na hiyo statement yake, yaani hakujua hata malengo ya safari yeye amekurupuka tu kufurahia shopping ya Dubai? Loh!
 
Sipingi huja ya mbunge lkn Kuna shida nyingine naiona kwa sisi wa bongo.
Hivi mbunge atoke Tanzania hadi Dubai hajui alienda kufanya nn? Hatupo serious kiasi hiki kweli?

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
Kasema baada ya kuuliza wanaenda fanya nini alijibiwa na Mbarawa wanaenda kujifunza namna wengine wanavyoendesha bandari ili waje kuishauri Serikali.
 
Mbunge wa Nkasi ameviambia vyombo vya habari Mwanasheria mkuu wa Serikali hadi MKATABA wa milele wa bandari ya Tanganyika na waarabu unaletwa bungeni kesho yake hakuwa na taarifa.

"...hilo jambo lililetwa kwa uharaka wa ajabu na nikuhakikishie ndugu WAANDISHI hadi jioni ya kuamkia kesho ya MKATABA ule kuletwa bungeni AG hakuwa na taarifa yeyote!"

Mbunge Aida Khenani.
 
Kama ni kweli serikali imekosea sana,au ndio maana waziri Mkuu kapooza sana , pengine na yeye alizungukwa?

Mbunge Musukuma hili suala limemuacha uchi sana,ujinga wa viherehere kwa mambo mazito,kwa sasa simsikii tena,kaona haya ni maji marefu "kwerikweri " in MAGUFULI VOICE
 
Back
Top Bottom