Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

yote ilikuwa kukuingiza kingi na UKAJAAA

Hujaingiza yeyote kingi zaidi ya kuzidi kujifunua jinsi ulivyo mdini na mbaguzi wa hali ya juu. Mimi hapa natizama mwelekeo wa the new Game Theory aliyekuwa "amejificha kwa muda sana".
 
Hujaingiza yeyote kingi zaidi ya kuzidi kujifunua jinsi ulivyo mdini na mbaguzi wa hali ya juu. Mimi hapa natizama mwelekeo wa the new Game Theory aliyekuwa "amejificha kwa muda sana".
Wana JF,

Nashukuru mwana JF aliyeweka hadharani MOU husika. Ningependa tu kuongezea machache na hasa historia ya jinsi na kwanini MOU hiyo ilizaliwa:-

1i) Wote mtakumbuka kuwa huko nyuma Serikali ilitaifisha Shule na nyingi za madhehebu ya Dini. Utaifishaji huo uliendana pia na Ardhi, hasa ikizingatiwa kuwa wakati shule zinajengwa zilijengwa kwenye maeneo ya madhehebu ya dini na papo hapo kukukiwa na kanisa, nyumba za mapadre na kadhalika. Hii ilikuwa hivyo kwa shule nyingi za Middle School (Model Schools, Upper Primary kama mnavyojua majina yalibadilika sana kati ya 1962 hadi 1965 hivi na ndipo pia mtihani au darasa la nane lilipofutwa rasmi).

2) Kwenye miaka ya 1980 madhehebu yakataka warudishiwe ardhi yao, hasa ardhi ambayo ina majengo mengine yasiyohusiana na shule hizo. Mchakato wa mjadala ulishika kasi, mwaka 1986 Baraza la Maaskofu Katoliki TEC, lilipopitisha azimio rasmi,na kumtaka Katibu Mkuu, awasiliane na Serikali, kuanzisha mchakato wa kufanya survey na kutenga ardhi ya shule rasmi kutoka kwenye ardhi inayotumika kwa huduma nyinginezo za madhehebu ya dini. Wakati huo mimi Dr. Slaa, ndiye nilikuwa Katibu Mkuu wa TEC baada ya kupokea rasmi kazi hiyo December, 1985. Wakati huo madhehebu yaliisha kudai yarudishiwe Shule zao kwa kuwa zimegeuka kuwa aibu kwa kukosa ukarabati, na ziko kwenye hali mbaya sana. Serikali ilikuwa imekataa ombi hilo kwa lengo la kuwa Shule hizo zinawahudumia watanzania wote bila ubaguzi, jambo ambalo ndilo lilikuwa lengo kuu la utaifishaji, na sababu ya utaifishaji ilikuwa bado inaendelelea.

3) Wakati mawasiliano yalipoanza na Serikali wakati huo kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Elimu, Serikali iliomba TEC na madhehebu ya Dini kwa ujumla, kama yanaweza kusaidia ukarabati wa shule hizo kwa kuwa ziko kwenye hali mbaya na hali ya uchumi wa nchi haikuwa nzuri na hivyo mapato ya Serikali.

4) Wakati mchakato huo kwa upande wa Elimu umeanza kulikuwa pia na mgogoro kati ya Serikali na TEC baada ya Serikali kuichukua Hospitali ya Bugando almost kwa utaratibu huo huo wa kuitaifisha. Hospitali hiyo ilikuwa kwenye awamu ya Pili ya ujenzi kwa msaada mkubwa wa Shirika la Misereor( Shirika la Maendeleo la Baraza la Maaskofu Katoliki la Ujerumani) toka Ujerumani.

5) Katibu Mkuu wa TEC alipowasiliana na Wahisani walikataa kata kata kujihusisha tena na ujenzi au ukarabati wa Shule au Hospitali ( Hospitali, vituo vya Afya na zahanati) kwa kuhofia kuwa Serikali ya Tanzania imekuwa ikitaifisha huduma hizo bila majadiliano ya aina yeyte, na hawawezi kuwekeza fedha za walipa kodi wao ( ujerumani Madhehebu ya dini yanapata fedha rasmi kutoka kodi ya wananchi) kwa ratio waliyokubaliana kuendana na idadi ya madhehebu ya dini. Lakini walikuwa tayari kuendelea na huduma mbalimbali za kusaidia madawa na elimu kwa shule zilizoko bado chini ya madhehebu kwa kuwa hawawezi kuwaadhibu wananchi na watoto.

6) Kwa kuwa shughuli zote za Bugando zilikuwa zinaelekea kusimama na kulikuwa na mgomo kila siku, kwa madaktari na manesi na watumishi, Serikali ikaomba tujadiliane upya juu ya mambo makubwa mawili a) Utoaji huduma katika sekta za huduma za Jamii, b) Kuwa na chombo cha mawasiliano na majadiliano kati ya Ikulu na madhehebu ya dini, na kwa kuwa madhehebu ni mengi wakaomba chombo hicho kiundwe na viongozi wakuu wa madhehebu yaliyokuwa yanajulikana kwa mujibu wa Sheria, hivyo Bakwata ( Waislamu- sitaki kuingia kwenye mjadala wa kama Bakwata ni chombo kinachowasilisha waislamu au la), Tanzania Episcopal Conference TEC na CCT ( kwa madhehebu zaidi ya 60 yaliyoko chini ya Christian Council of Tanzania) . Baada ya Mashauriano tuliunda chombo hicho kikiwakilishwa na Mwenyekiti na Katibu wa vyomb o nilivyovitaja hapo juu. Uratibu ulikuwa unabadilika kila mwaka katika ya madhehebu hayo, vivyo hivyo kwa Sekretariat. Kutokana na utaratibu huo tuliweza kupatia ufumbuzi matatizo yaliyokuwa yakijitokeza mara kwa mara na ikawa rahisi kwa Serikali kuwasiliana na chombo hicho badala ya kila dhehebu peke yake, na kwa upande wetu pia chombo hicho kikatupa nguvu ya kujadiliana na serikali (power of negotiation).

7) Kutokana na hali mbaya ya Shule Serikali, ikaomba madhehebu ya dini kusaidia ukarabati wa shule zilizoonekana zitafungwa kutokana na hali mbaya , nasi kwa upande wetu kwa nia njema ya kuisaidia Serikali lakini pia kuwahudumia watanzania tuliwasiliana na Wahisani ambao walikazia msimamo wao kuwa hawako tayari kuingia kwenye shughuli za ujenzi wala ukarabati kwa kukosa msimamo wa wazi na au wa kisheria wa Serikali ya Tanzania kuhusiana na utaifishaji wa huduma hizo. Serikali ilipojulishwa, ilichukua hatua ya kuanzisha mchakato mzima wa kupata suluhu ya jambo hilo. Ndipo akapewa jukumu hilo, Mhe. Anne Makinda wakati huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, na mkutano wa kwanza ulifanyika Kurasini Conference Centre (TEC) Mikutano ya baadaye ilikuwa ina alternate kati ya TEC na CCT. Hii ni kwa sababu huduma zilizokuwa zinajadiliwa ni za TEC na CCT ( ambao walikuwa wameathirika na utaifishaji huo). Hatimaye, Serikali ilikubali kuwa haitataifisha tena, na kwa kuthibitisha hivyo, ikawa tayari kuwekeana MOU na madhehebu ya Dini.

Ndipo tukaanzisha mchakato wa majadiliano na Wahisani, na wahisani, nao katika umoja wao kati ya dhehebu la kikatoliki Ujerumani na Kilutheri pia la Ujerumani tukaanzisha mchakato wa namna bora ya kutoa huduama za jamii. Daima Serikali ilishirikishwa kama Observer katika michakato hiyo, na kwa upande wa Ujerumani Serikali yao nayo ilishirikishwa katika timu za majadiliano. Hatimaye, makubaliano yalifikiwa, na ndipo ikazaliwa chombo kipya Christian Social Services Commission (CSSC), chenye Secretariat yake ( Katibu Mtendaji wa kwanza akawa Dr. F.Kigadye aliyekuwa Mkurugenzi wa Bugando). Huduma za kilichokuwa Christian Medical Board (ya TEC na CCT ikavunjwa na kuwekwa chini ya CSSC) na idara za Elimu zilizokuwa chini ya TEC na CCT huduma zake zikaunganishwa na kuwekwa chini ya CSSC. Ndiyo MOU iliyosainiwa na Askofu Stanford Shauri wa Diocese ya Ruvuma, Mwenyekiti/Katibu Mkuu wa CCT wakati huo, na Askofu Josephat Lebulu, wakati huo Askofu wa Jimbo Katoliki la Same, na Mwenyekiti wa TEC. Kwa upande wa Serikali kama sikosei aliweka saini Mhe. Edward Lowassa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (au Waziri sikumbuki).

8) TEC na CCT nazo zikawekeana na Wahisani Mkataba MOU yao ya ndani ili kupata misaada ya ujenzi, ukarabati na uendelezaji wa huduma zote za jamii . Huduma hizo zinaendelea hata sasa japo sasa kwa kiwango kidogo baada ya mkataba wa awali kwisha.

Narudia tena, namshukuru sana aliyeweka kwenye JF MOU hiyo. Ninarudia kuwaomba wenzangu, tumetumia muda mrefu sana kujadiliana kwa hisia ya aina mbalimbali. Watanzania hatukuzoea huko nyuma kuulizana dini zetu, wala kabila wala ukanda. Haya mambo tukiyaendekeza Taifa letu litakuwa hatarini. Tukumbuke kubomoa ni kazi nyepesi sana, sekunde lakini kujenga tena inachukua muda mrefu na ni kaz ngumu, na wakati mwingine hata ukifanikiwa huwezi kujenga kama ilivyokuwa. Nashauri ili JF ibaki na heshima yake ya Home of Great Thinkers tupende kufanya Research zaidi kabla ya kulaumiana au kuhisiana, kama mtu hana taarifa za kina awaombe wenye taarifa. Kama mnavyoona mimi nilikuwa nafahamu historia yote, nafahamu MOU, lakini sikuwa nayo. Mtu huwezi kujua kila kitu na au kuwa na kila kitu, we need to complement each other. Tunaweza tukidhamiria, na JF itabaki na hadhi na heshima yake daima.
 
Wana JF,
Nashukuru mwana JF aliyeweka hadharani MOU husika. Ningependa tu kuongezea machache na hasa historia ya jinsi na kwanini MOU hiyo ilizaliwa...

Mheshimiwa mbunge hakuna anayelaumu bila kufanya research,naomba usome kitabu cha DR.SIVALON kanisa katoliki na siasa Tanzania,kuna upendeleo wa wazi kabisa baina ya serikali na wakristu.hakuna anayelaumu kwa hisia laa bali kwa ushahidi wa UDINI wa kanisa,soma The Mwembechai killings.

shule kama Forodhani iliyopo Dar-Es-salaam Posta inahitaji matengenezo gani? ok wamerudishiwa kanisa kutokana na hii MOU lakini hivi sasa waislam hawasomi wamezuiliwa.wanasoma wakristu watupu.shule kama Mazengo ilikuwa ina msaada mkubwa kwa watanzania wote hivi sasa imerudi kanisani,Magamba,chuo cha Benki Iringa wamepewa wakristu. na sehemu nyingi sana.

lakini shule kama Tambaza,Azania,Jangwani,Zanaki,Lumumba primary school,Mnazi Mmoja shule ya msingi zilikuwa mali ya waislam,hakuna hata moja imerudishwa kwa waislam.

kama ilikuwa MOU imelenga na waislam kupitia Bakwata mbona hakuna sehemu inayoonesha kuwa Bakwata walisaini?

na waislam waliposema wenzetu wamepewa na sisi tumeandaa MOU yetu walifukuzwa,bwana Slaa usawa uko wapi?

Mheshimiwa Mbunge nilitegemea uwe NEUTRAL kwenye hili lakini umeshindwa kuficha UDINI wako na kupendelea upande wako.

well and good kumbe siku zote unajua kuwa Kanisa linatufaika na MOU,kwanini lipokuja suala la Mahakama ya Kadhi usiwaambie wabunge kuwa MOU serikali inasaidia kanisa kwa pesa, basi na hawa wenzetu serikali igharamie fedha kwenye mahakama yao kama inavyofanya kwa kanisa.

mwaka 2006 Lowassa huyo huyo kupitia MOU kaja Marekani na kuchukua bilioni 14 za Hospital ya Bugando.

mwaka 2005 Sumaye alifanya ziara rasmi Marekani ya kidini tu na kutumia milioni 500 kwa shughuli za MOU.

Hospital ya Muhimbili kuna majengo ya waislam kama Sewa hajji na Mwaisela.basi na sisi turudishiwe.

Bwana mbunge siku zote wanapokuwa viongozi wakuu wa kiislam basi choko choko za kanisa hazikosi.mfano barua za kichungaji za maaskofu 1987 wakati wa Mzee Mwinyi na hili la sasa kwa JK mara waraka wa kanisa n.k
lazima tuambiane na kulaumiana ndio dawa sio kunyamaza.
 
Nzuri kafu na sisi maf wamefulia mkuu

Wewe unaaminije gazeti ambalo halijatupa evidence? Si mara nyingi tu hawa nao wamesema uongo na mara nyingi huwa hata wao wana pick hizo tetesi hapa na kuzibandika kwao?
Najua na wao nimemba hapa wambie walete soft copy kabla hatujaanza mijadala ya huo mkataba.
Inawezekana ni mkataba clean kama vile ilani ambayo mmeipigia kelele mwisho imebainika haikuwa mbaya! Hata Makamba kathibitisha hilo.
:)
Mzee wa BK MJINI gazeti hili halijawahi kushtakiwa ni kati ya magazeti makini TZ.SO FAR ni MWANAHALISI ndio linapelekwa mahakamani kila mara kwa kuandika bila evidence, hukumbuki lilifungiwa miezi mitatu.
 
- Saafi sana Mkulu K2 penye uongo ukweli hujitokeza juu zaidi, Mwanahalisi hawana mpinzani bongo, maana sasa hata Tanzania Daima kuna mkono wa mafisadi na wala sio siri, na yes I said it!

Respect.

Kamanda FMEs!
 
Nadhani its about time JF wakawaexpose hawa magazeti ambayo yanachukua data humu bola kutoa props to JF

hii ni aibu nadhani tunaweza kuanza na ma editors wa haya magazeti and i am sure its a war of words ambayo they wont win
 
Mheshimiwa mbunge hakuna anayelaumu bila kufanya research,naomba usome kitabu cha DR.SIVALON kanisa katoliki na siasa Tanzania,kuna upendeleo wa wazi kabisa baina ya serikali na wakristu.hakuna anayelaumu kwa hisia laa bali kwa ushahidi wa UDINI wa kanisa,soma The Mwembechai killings.

Kwa nini kitabu kimoja tu ndio kisomwe? Tanzania yote inaweza kuandikwa na mtu mmoja tu na ndiye akawa na facts zote?

shule kama Forodhani iliyopo Dar-Es-salaam Posta inahitaji matengenezo gani? ok wamerudishiwa kanisa kutokana na hii MOU lakini hivi sasa waislam hawasomi wamezuiliwa.wanasoma wakristu watupu.shule kama Mazengo ilikuwa ina msaada mkubwa kwa watanzania wote hivi sasa imerudi kanisani,Magamba,chuo cha Benki Iringa wamepewa wakristu. na sehemu nyingi sana.

Sema kwamba, shule zote za wakristo zirudishwe na zile za waislam zirudi. Au sio.

l
akini shule kama Tambaza,Azania,Jangwani,Zanaki,Lumumba primary school,Mnazi Mmoja shule ya msingi zilikuwa mali ya waislam,hakuna hata moja imerudishwa kwa waislam.

Naona hapa unataka kusema kuwa waislam warudishe kile chuo cha Tanesco walichopewa na serikali na wamekifanya chuo kikuu cha kiislam.

kama ilikuwa MOU imelenga na waislam kupitia Bakwata mbona hakuna sehemu inayoonesha kuwa Bakwata walisaini?

na waislam waliposema wenzetu wamepewa na sisi tumeandaa MOU yetu walifukuzwa,bwana Slaa usawa uko wapi?

Chama cha mapinduzi kimetawala Tanzania kwa miaka kibao sasa. Viongozi wa ccm wengi ni waislam, kwa nini wanawaonea waislam? masikini waislam wanaonewa na waislam wenzao?

Mheshimiwa Mbunge nilitegemea uwe NEUTRAL kwenye hili lakini umeshindwa kuficha UDINI wako na kupendelea upande wako.

well and good kumbe siku zote unajua kuwa Kanisa linatufaika na MOU,kwanini lipokuja suala la Mahakama ya Kadhi usiwaambie wabunge kuwa MOU serikali inasaidia kanisa kwa pesa, basi na hawa wenzetu serikali igharamie fedha kwenye mahakama yao kama inavyofanya kwa kanisa.

Kama vile ambavyo serikali imekuwa inasaidia mahujaji?!

mwaka 2006 Lowassa huyo huyo kupitia MOU kaja Marekani na kuchukua bilioni 14 za Hospital ya Bugando.

mwaka 2005 Sumaye alifanya ziara rasmi Marekani ya kidini tu na kutumia milioni 500 kwa shughuli za MOU.

Hospital ya Muhimbili kuna majengo ya waislam kama Sewa hajji na Mwaisela.basi na sisi turudishiwe.

Bwana mbunge siku zote wanapokuwa viongozi wakuu wa kiislam basi choko choko za kanisa hazikosi.mfano barua za kichungaji za maaskofu 1987 wakati wa Mzee Mwinyi na hili la sasa kwa JK mara waraka wa kanisa n.k
lazima tuambiane na kulaumiana ndio dawa sio kunyamaza.

Kama vile ambavyo wakati wa Mkapa waislam walikuja na chokochoko na misemo ya mapanga shaa shaa. Same standard au vipi?
 
Last edited:
sita.jpg

Ukisikia kupiga ikulu ndio huku.Kimyaaaaa,watu wamepotea kabisa na waliopo wanaonekana wamepoteana.Asante kwa kutufunua
 
Kwa hiyo jamani huu mkataba tuufananishe na MYK? je uko katika katiba na sheria za nchi kama wanavyotaka ndugu, marafiki na jirani zangu waislamu?
Mbona sioni kosa lolote katika mkataba huu?
 
Jamani mimi swali langu moja tu ina maana ni kweli shule ya Forodhani haipokei tena Waislamu??

Nadhani kama serikali ilimua kufanya makubaliano hayo na taasisi za wakristo peke yake huku ikiwakatalia waislamu na taasisi zao itakuwa sio haki kabisa basi taasisi za kiislamu zina kila haki ya kupinga makubaliano hayo.

Nadhani kuwe na mwongozo kutoka serikalini kwa ajili ya dini zote ili kuondoa malalamiko yeyote yanayoweza kujitokeza, kwa sababu hivi sasa hii nchi inaelekea kubaya.
 
Last edited:
Mkatanba huu hauna dosari yoyote! Unajua serikali inajishughulisha na mambo ya mwili - maendeleo ya watu. Haijishughulishi na mambo ya kiroho (uwanja wa dini). Kumbe wale wote walio tayari kuisadia serikali kuleta maendeleo kwa watu inawajengea mzingira mazuri ili waweze kuisadia katika kuleta maisha bora kwa kila mtanzania.

Wakristo wanajishughulisha na mtu mzima (mwili na roho). Wanahubiri Injili na kujishughulisha na maendeleo ya jamii. Hapa kwenye maendeleo ndipo wanapokutana na malengo ya serikali. Tunakuwa wadau hai, washiriki katika kazi zake. Ndiyo maana inawajengea mazingira ili watoe hizo huduma. Serikali iliingia kwenye MoU kwa shabaha hiyo!

Ndugu zetu waislamu, wao wanajishughlisha ZAIDI na mambo ya kiroho (ibada). Kwa kiwango kikubwa hawana habari na shughuli za maendeleo ya watu (huduma za jamii). Hii inawafanya wasiwe washiriki wakubwa wa serikali kwa sababu hawaiingii katika majukumu ya serikali. Kumbe inakuwa vigumu kwao "kufaidi" mazingira yaliyojengwa na serikali kwa ajili ya wale walio tayari kuisadia katika kuleta maendeleo ya watu. Kulalamika kwao hakuna msingi. Wakitaka kuyatumia mazingira haya lazima waanze kujishughulisha na maendeleo ya watu. Sidhani kama serikali itawakataza.

Tena kwa mtazamo wangu waislamu wakiamua wanaweza kufanya makubwa zaidi kuliko wakristo kwa sababu wanapata misaada mingi sana kutoka nchi za kiarabu. Misada yao ni mikubwa kuliko ya wakristo kutoka ulaya na marekani. Shida ya hawa ndugu zetu ni ubinafsi na vipaumbele. Fedha inaishia kwenye mifuko ya wachache. Na kiasi kinachobaki wanajenga misikiti kila mtaa, tena misikiti mikubwa kuliko ya Dubai. Ndiyo mwisho! Wanapaswa kubadilika, ndiyo wataachana na mambo ya lalamu. Kulalamika hakusaidii. Tufanye kazi jamani!
 
Geeque,

..kulingana na maelezo ya Dr.Slaa ni kwamba Bakwata walikuwa wakihudhuria vikao vya majadiliano baina ya serikali na Kanisa.

..nini kilitokea kiasi kwamba ktk MOU Bakwata wala jumuiya yoyote ya Waislamu haipo ni kitendawili kikubwa.

..nadhani watu wa kwanza wa kuwahoji wanapaswa kuwa Bakwata wenyewe. vilevile labda Dr.Slaa anaweza kutusaidia kutupa majibu.

..lakini wakati tunasubiri labda tungejiuliza ni shule zipi na hospitali zipi zilikuwa za madhehebu ya Waislamu na zikataifishwa?
 
JokaKuu,

Nadhani itakuwa muhimu kwa Bakwata na Serikali kutoa maelezo yao kuhusiana na na Jumuiya za kiislamu kutokuwepo katika MOU walioingia na kanisa. Kwa sababu haya mambo ya dini yataleta mtafaruku mkubwa sana ndani ya nchini. Tunajua kila upande utavutia kwake lakini ni muhimu kwa serikali kuwa dhabiti katika kuhakikisha hakuna upande unaoona kuwa umeonewa.

Kama nilivyosema mwanzo nadhani ni muhimu kwa serikali kuweka mwongozo kwa jumuiya zote za kidini kuonyesha njia gani za kufuatwa ili kuweka makubaliano yeyote na serikali katika utoaji wa huduma zao za kijamii.
 
Mkatanba huu hauna dosari yoyote! Unajua serikali inajishughulisha na mambo ya mwili - maendeleo ya watu. Haijishughulishi na mambo ya kiroho (uwanja wa dini). Kumbe wale wote walio tayari kuisadia serikali kuleta maendeleo kwa watu inawajengea mzingira mazuri ili waweze kuisadia katika kuleta maisha bora kwa kila mtanzania.

Wakristo wanajishughulisha na mtu mzima (mwili na roho). Wanahubiri Injili na kujishughulisha na maendeleo ya jamii. Hapa kwenye maendeleo ndipo wanapokutana na malengo ya serikali. Tunakuwa wadau hai, washiriki katika kazi zake. Ndiyo maana inawajengea mazingira ili watoe hizo huduma. Serikali iliingia kwenye MoU kwa shabaha hiyo!

Ndugu zetu waislamu, wao wanajishughlisha ZAIDI na mambo ya kiroho (ibada). Kwa kiwango kikubwa hawana habari na shughuli za maendeleo ya watu (huduma za jamii). Hii inawafanya wasiwe washiriki wakubwa wa serikali kwa sababu hawaiingii katika majukumu ya serikali. Kumbe inakuwa vigumu kwao "kufaidi" mazingira yaliyojengwa na serikali kwa ajili ya wale walio tayari kuisadia katika kuleta maendeleo ya watu. Kulalamika kwao hakuna msingi. Wakitaka kuyatumia mazingira haya lazima waanze kujishughulisha na maendeleo ya watu. Sidhani kama serikali itawakataza.

Tena kwa mtazamo wangu waislamu wakiamua wanaweza kufanya makubwa zaidi kuliko wakristo kwa sababu wanapata misaada mingi sana kutoka nchi za kiarabu. Misada yao ni mikubwa kuliko ya wakristo kutoka ulaya na marekani. Shida ya hawa ndugu zetu ni ubinafsi na vipaumbele. Fedha inaishia kwenye mifuko ya wachache. Na kiasi kinachobaki wanajenga misikiti kila mtaa, tena misikiti mikubwa kuliko ya Dubai. Ndiyo mwisho! Wanapaswa kubadilika, ndiyo wataachana na mambo ya lalamu. Kulalamika hakusaidii. Tufanye kazi jamani!

Maelezo na madai yako Babuyao yamejaa upotoshaji mkubwa, nadhani hii haitajenga kuleta uelewano na hatimae kuondoa shutuma mbalimbali ambazo zipo mpaka hivi sasa. Kuamua kuandika chochote kilichopo moyoni mwako bila ya kufanya utafiti wa madai yako sidhani kama ni jambo la busara. Kila mtu ana mawazo lakini sio kila mawazo yamejaa utu ndani yake.
 
Ndio kwenye bandiko la Dr Slaa kasema na Bakwata walikuwapo katika mchakato wa kwanza wa mazungumzo na serikali, lakini ghafla wakatoweka maana hawakuwa na taasisi za kijamii walizotaifishwa na hivyo kwamba wangeweza kuomba serikali iwarudishie.
Waligundua kuwa wao hapo hawahusiki na wakajitoa.
Kama alivyosema msemaji mmoja hapa, waislamu wanapata pesa nyingi sana toka nje, lakini vipaumbele vyao kwa ajili ya jamii yote ya kitanzania ni nini? Hapo ndipo tunataka akina kanda2, mfumwa,GT, na wakeleketwa wengine mtwambie. Vipaumbele vyenu kwa jamii ya kitanzania nyinyi waislamu kama mgekuwa na MOU na serikali ingelikuwa nini? Hii MYK? au OIC?
Sikiliza. Hata rais mwislamu alijua juhudi za wakristo katika kuijenga sisi m na akanywea na kukubali wawe na MOU. Nyie mbumbumbu mko mnapiga kelele tu kwa sababu ya vitu ambavyo havitasaidia jamii yote.
 
Swali ni Je hii MOU kati ya Serikali na Jumuiya za Kikristo ililenga zaidi kwenye miradi ambayo ilishataifishwa au hata miradi yote ijayo? Kama pia inahusisha miradi yote ijayo kwa nini serikali isiweke mwongozo kwa jumuiya zote za dini mbalimbali na sio jumuiya za Kikristo pekee?

Kwa sababu madai makubwa ya Waislamu ni kwamba walikataliwa na Serikali kuingia nao MOU ilhali Jumuiya za Kikristo zikiwa zimekubaliwa.
 
Inafaa waislamu waoneshe hiyo MoU yao iliyokataliwa. Tujiridhishe. Tusiandikie mate na wino upo, tutakuwa hatutendi haki. Kama ni kweli walikataliwa basi lazima kulikuwepo sababu NZITO. Vinginevyo siamini wala sielewi kwa nini serikali iwakatalie kama mambo yao wameyaweka sawa. Yawezekana hawakutimiza baadhi ya masharti. Waoneshe sababu kwa nini MoU yao ilikataliwa. Shida wanaishia kusema MoU yao ilikataliwa bila kuonesha sababu zilizotolewa na serikali.
 
Babuyao,
Nakubaliana nawe kwa hili, nadhani ni muhimu kwa Serikali na Jumuiya ya Kiislamu husika kutoa maelezo ni kwa nini waliwakatalia/walikataliwa kuwekeana makubaliano na serikali. Hii itatusaidia wengi kujua tatizo liko wapi.
 
Geeque,

..ingekuwa vizuri kama ungesoma maelezo ya Dr.Slaa. yeye alihusika na suala hili wakati akiwa katibu wa TEC.

..kwa kifupi mazungumzo kati ya Kanisa na serikali yalianza 1986, halafu hii MOU ilisainiwa miaka ya 90 wakati Lowassa ni waziri ktk Ofisi ya waziri mkuu.

..sasa tangu wakati huo mpaka leo kama Bakwata wangekuwa na nia ya kusaini MOU ya aina yoyote na serikali binafsi naamini wangepewa nafasi hiyo.

..vilevile serikali ya Mkapa walitoa majengo ya Tanesco kuwa Chuo Kikuu cha Waislamu. sasa mali kama zile, na ukizingatia kwamba zilikuwa za Tanesco, hazihamishwi bila mkataba unaotambulika kisheria.

..sidhani kama serikali ikiamua kufanya jambo fulani na Waislamu basi lazima ifanye jambo hilohilo kwa Wakristo. tukiwa na mawazo kama hayo ndiyo mwanzo wa frustration zisizokwisha.
 
Back
Top Bottom