Mkapa alitumia 2.65bln Kusuluhisha Kenya!

Kama Mkapa Alitumia Kiasi Hicho Koffi Anan Alitumia Kiasi Gani?
Haya Mambo Ni Mazito Kweli Kweli. Mkapa Alikuwa Amekaa Pembeni Mwa Anani Na Sikuona Role Yeyote Ile. Mwaka Wa
 
kwa mtaji huu vyama vya upinzani havitaona ikulu milele.
Vita dhidi ya rushwa ni kubwa mno, ubadhirifu ni mkubwa mno na unawamalizia muda wote,

hawataweza kujipanga milele,mimi naona kuna ujanja wa kuwaweka bize na haya mambo wasijipange kuchukua nchi kwa uchaguzi.
Ila nawaasa.
msijisahau, jiandaeni majimboni mwenu wakati ndio huu.
wakati mnapiga kelele na wananchi wanafurahi, basi hakikisheni huko majimboni mnapokelewa pia.
tunatak aviti vya wapinzania mashujaa viongezeke
 
Mie naomba Mmuache Mkapa kwa hili,Kosa la Mkapa Hapa ni lipi kama siyo wivu tu ambao umewajaa watanzania wengi.Na wakati mwingine huwa nahisi maneno aliyoyasema Mkapa ni kweli,Watananzania ni Wavivu wa Kufikiri.

Yeye alichaguliwa kuwa Msuluhishi tu,Na kuhusu Malipo yeye yalikuwa hayamhusu kama Alilipwa na Serikali au alilipwa na UN au AU,Mpaka kieleweke hiyo siyo habari ya kujadili humu ndani na haina maana yeyote ila inajadilika kwa maana ingine ila siyo kwa kumhusisha Mkapa.

Mkapa kama Rais Mstaafu lazima apewe Ulinzi akiwapo sehemu yoyote ambayo kuna Machafuko na hata akiwa Nchini,Deligate yake ya TISS na Daktari wake wanalipwa na Serikali.Kwa kfupi kama ana Watu kumi na walikaa Nairobi kwa Muda huo wote ulitegemea watumie Sh. Ngapi.Mkapa kama Rais lazima akae katika Hoteli ya 5 stars.

Pia Wakati akienda Nairobi aliondoka na Wasaidizi ambao ni wataalam wa ambao mbali mbali waliokuwa wakifanya majadiliano ya Hapa na pale kabla ya kufikia hitimisho.Hapa Kuna mambo mawili AU ina utaratibu ambao Nchi huchangia gharama mbali mbali za Umoja huo na inawezekana Tanzania iliombwa kufanya hivyo.

Tuwe tunaongea hivyo na vigezo na kwa mpangilio unaofaa na siyo kisa mkapa.Wewe ulitaka Afanye kazi Bure.Amesoma na lazima alipwe kutokana na anachofanya
 
mkuu hapana sio wivu bali ni haki yetu kujadili iwapo tunatiashaka matumizi makubwa ya serikali kwani hatimaye tunaoumia ni sisi.

mimi naamini maswali ya kujiuliza ni

- jee serikali ndio iliyolipia gharama za juhudi za usuluhishi au ni un, au n.k?

- kama serikali iligharamia je ilifanya hivyo kwa sababu zilikuwa juhudi binafsi za tanzania au iliombwa kufanya hiyo? je kofi annan nani alimlipia?

mara nyingi serikali ya nchi mwenyeji ndio inahusika na ulinzi wa kiongozi mgeni (labda wamarekani ambao husisitiza kuongoza ulinzi wa kiongozi wao) kwa hali ya kenya basi serikali ya kenya iliwajibika na ulinzi wa mkapa na naamini kama walinzi kutoka bongo walikuwa sio zaidi ya watatu (kumbuka huyu ni rais mstaafu na sio current).

hata kama alikaa nyota 5 kiwango kilichotajwa ni kikubwa sana. sasa swali ni jee bwm alihusika hapa? binafsi sidhani kama alihusika labda kama baada ya shughuli alipeleka madai ya "imprest" vinginevyo naamini wa kuwabana ni hao walioidhinisha hayo matumizi waeleze kulikoni? inawezekana na wao ndio wameamua kujichotea chao mapema.
 
Mie naomba Mmuache Mkapa kwa hili,Kosa la Mkapa Hapa ni lipi kama siyo wivu tu ambao umewajaa watanzania wengi.Na wakati mwingine huwa nahisi maneno aliyoyasema Mkapa ni kweli,Watananzania ni Wavivu wa Kufikiri.

Yeye alichaguliwa kuwa Msuluhishi tu,Na kuhusu Malipo yeye yalikuwa hayamhusu kama Alilipwa na Serikali au alilipwa na UN au AU,Mpaka kieleweke hiyo siyo habari ya kujadili humu ndani na haina maana yeyote ila inajadilika kwa maana ingine ila siyo kwa kumhusisha Mkapa.

Mkapa akama Rais Mstaafu lazima apewe Ulinzi akiwapo sehemu yoyote ambayo kuna Machafuko na hata akiwa Nchini,Deligate yake ya TISS na Daktari wake wanalipwa na Serikali.Kwa kfupi kama ana Watu kumi na walikaa Nairobi kwa Muda huo wote ulitegemea watumie Sh. Ngapi.Mkapa kama Rais lazima akae katika Hoteli ya 5 stars.

Pia Wakati akienda Nairobi aliondoka na Wasaidizi ambao ni wataalam wa ambao mbali mbali waliokuwa wakifanya majadiliano ya Hapa na pale kabla ya kufikia hitimisho.Hapa Kuna mambo mawili AU ina utaratibu ambao Nchi huchangia gharama mbali mbali za Umoja huo na inawezekana Tanzania iliombwa kufanya hivyo.

Tuwe tunaongea hivyo na vigezo na kwa mpangilio unaofaa na siyo kisa mkapa.Wewe ulitaka Afanye kazi Bure.Amesoma na lazima alipwe kutokana na anachofanya

Uliyosema yote ni sahihi kwa maana ya "hawezi kufanya kazi bure" lakini umepatia kabisa kwa kusema tunaweza kubadili angle kwa kuanza na kuhoji, kwanza Je, kwa gharama hizo, Watanzania wangeulizwa ama kumpeleka Mkapa Kenya ama kununua mahindi ya njaa, nadhani wangeamua kununua mahindi ya njaa ama kukarabati barabara mbovu huko vijijini japo nusu kilometa ama kununua japo madawati na kujenga vyoo badala ya kusubiri wezi wa madini yetu watujengee.

Lakini pia huna sababu ya kumzuia Mpaka Kieleweke kuweka hii mada hapa, tena mada ambayo imejadiliwa bungeni na serikali haijatoa maelezo. Tusubiri maelezo ya serikali hata kama Gembe unahusika kutoa majibu hayo, tusubiri wakijibu bungeni na kukubaliwa maelezo yao ndipo mjadala unaweza kubadilika.

Tukijadili tusijangalie sisi tu "tuliosoma" tuwangalie na mama na bibi zetu ambao "hawakusoma" kule vijijini kama wananufaika na huo "usomi" wetu. Ndio maana hata Mugabe anawaambia aliye msafi ndiye amnyoshee kidole yeye, sasa Mkapa ni msafi?
 
Nitaweka hansard ya kipindi cha jana jioni mara nikiipata kwani hii inatia uchungu sana sana ,na hata asubihi hii mwanasheria mkuu wa serikali anasema eti kuwa serikali haina idadi ya kesi za kubambikiwa ambazo wananchi wamebambikizwa.

Dr.Slaa alisimama na kutaka muongozo wa Spika kwani ripoti ya Jaji Kisanga ya Haki za Binadamu ambayo wabunge walipewa nakala ilikuwa na vielelezo vya hizo kesi ila spika kaamua kiumwokoa huyu mwanasheria mkuu ambaye hasomi ,kwa kweli serikali hii ipo kama inataka kuanguka vile kwani kila siku kila mtu anakuja na jambo la mauzauza humo ndani ya bunge.
 
Tanzania ni nchi maskini, wananchi wengi ni hohe hahe, mlo wa siku kwao ni shida, huduma za msingi kama afya, elimu na maji hawapati, barabara na miundo mbinu kwa jumla ni duni, uchumi wa nchi haukui na Taifa kwa ujumla limekuwa likizidi kudidimia. Haya ni mambo ambayo Serikali yetu inatakiwa kuyaangalia kwa uapana na kwa kuyapa kipaumbele. Hii tabia ya kuhamisha rasilimali zetu chache kwenda kushughulikia matatizo ya nchi nyingine ni dhahiri kuwa inatugharimu wananchi wa kawaida. Kama ni utaratibu wa AU na UN kuomba nchi wanachama kushughulikia matatizo ya nchi nyingine pindi yatokeapo kwa gharama zao, ni muhimu sasa tukasema HATUWEZI kwa kuwa hatuna uwezo kiuchumi wa kulipia gharama hizo. Yametokea Kenya, Comoro, Darfur, Lebanon, na bado hayataisha utasikia Zimbabwe, mara DRC, lini tutashughulikia mambo yetu ya msingi? Hebu fikiri 2.65 bilion zingetosha kujenga madarasa mangapi na kununua vitabu na madawati mangapi? Kila siku Serikali inatudanganya kuwa hakuna hela za kulipa arrears za mishahara kwa walimu lakini wanapata hela kulipia mambo yao. NAOMBA SERIKALI IACHE KUKIMBILIA MAMBO YA NJE KWA KUTAKA SIFA HUKU IKIACHA YALE MATATIZO YA NDANI YAKIZIDI KUELEMEA WANANCHI WAKE, TABIA HII HAILETI TIJA NA INAZIDI KUDUMAZA TAIFA LETU.
 
Wabunge wetu, amabo baadhi yao ndio wamekuwa mawaziri hawapendi kusoma taarifa muhimu.
sasa taarifa za kawaida itakuwaje?
ni reflection ya watanzania 80%
wachache wetu wanasoma sana.
wengine wengi wanapenda wasimuliwe porojo, uzandiki, na fitina wazidake, wazitumie kama hoja.
jambo ni hatari nanchi yetu itakata miti yote kutengeneza karatasi kuprinti mambo ambayo hayasomwi.
bora wampe Shigongo makaratasi ya bure kwani umbeya wake ndio unasomwa.
 
Kwa mpango huu ukijumlisha matumizi ya Mkapa na JK unaweza kupatwa na kiharusi

".....amakweli Tanzania nchi ya asali na maziwa.....tutaacha kunenepeana kweli"

kwenda Kenya kwa wiki 2 tumetumia mapesa yote hayo sasa tukienda kusuluhisha Zimbabwe si zinaweza kuzidi zile za EPA
 
Shilingi ngapi zimetumika kwa kamati ya mwafaka ya CCM na CUF kulinganisha na zilizotumika kusuluhisha WAKENYA? Naona Serikali imekwepa kujadili suala la Mkapa mbele ya ujumbe wa Kenya ambao sasa wanazungumza na wabunge, Dodoma
 
Nitaweka hansard ya kipindi cha jana jioni mara nikiipata kwani hii inatia uchungu sana sana ,na hata asubihi hii mwanasheria mkuu wa serikali anasema eti kuwa serikali haina idadi ya kesi za kubambikiwa ambazo wananchi wamebambikizwa.

Dr.Slaa alisimama na kutaka muongozo wa Spika kwani ripoti ya Jaji Kisanga ya Haki za Binadamu ambayo wabunge walipewa nakala ilikuwa na vielelezo vya hizo kesi ila spika kaamua kiumwokoa huyu mwanasheria mkuu ambaye hasomi ,kwa kweli serikali hii ipo kama inataka kuanguka vile kwani kila siku kila mtu anakuja na jambo la mauzauza humo ndani ya bunge.
Usiseme Mkapa Ndiye ametumia Pesa hiyo,Sema kwamba Pesa ambayo serikali ilitumia katika Kusuluhisha mgogoro wa Kenya.

Halisi,
Je mahindi ni bora kuliko Maishaa ya wakenya Ambao walikuwa wakiuana kila siku?Je ni hivyo unafanya kwa jirani yako?embu ukichukua hivyo vivyo sivyo ulivyouliza kwamba kama watanzania wakiambiwa watoe pesa ili kuokoa maisha ya jirani au wanunue Chakula cha Ziada wangechagua jambo lipi?
 
Shilingi ngapi zimetumika kwa kamati ya mwafaka ya CCM na CUF kulinganisha na zilizotumika kusuluhisha WAKENYA? Naona Serikali imekwepa kujadili suala la Mkapa mbele ya ujumbe wa Kenya ambao sasa wanazungumza na wabunge, Dodoma
Hizo ni nyingi zaidi ya hizo za kenya sababu mazungumzo yameanza toka 2002.
 
Kwa mtaji huu, inawezekana mkapa hakutaka mgogoro umalizike!!!!!!! Lakini wa kuulizwa hapa si Mkapa bali ni serikali! Ngoja tusubiri majibu ya serikali! Yawezekana na JK safari zote hizi za AU anatumia pesa yetu!!!!!!!!! Kwa kweli tutakufa kwa pressure. Mkapa anaenda kutumbua Nairobi na magunia ya midola (siyo ya Zimbabwe), mzee mwinyi anapanda mlima Kilimnajaro kuchangisha vijishilingi ambavyo havijai hata kiganja!!! Lazima waulizwe na waseme. Mkapa sifa za usuluhishi hana, hata haieleweki alienda kufanya nini!
 
Hizo ni nyingi zaidi ya hizo za kenya sababu mazungumzo yameanza toka 2002.

Unajua hizo mgogoro wa CCM na CUF zina unafuu kidogo. Kwanza ni kwa maslahi ya moja kwa moja ya nchi yetu na pili hatukutumia dola na kama kuna waliozipata (akina sefu) basi walijenge vijibanda hapahapa kwetu. Lakini huyo wa kwenda kuzilipa kwenye five star kenya ni tofauti. Usijeambiwa amefungua akaunti huko!!
 
Hizo ni nyingi zaidi ya hizo za kenya sababu mazungumzo yameanza toka 2002.

Nami naamini zinaweza kuwa zaidi, lakini ngapi? ili mjadala uanzie hapo.
Usiseme Mkapa Ndiye ametumia Pesa hiyo,Sema kwamba Pesa ambayo serikali ilitumia katika Kusuluhisha mgogoro wa Kenya.

Uko sahihi kabisa, maana Mkapa pamoja na matatizo yake, hana mamlaka ya kuchukua fedha serikalini na kwa kweli tunaweza kukuta hata hizo fedha Mkapa mwenyewe hajatumia hata senti tano. Unaweza kukuta Mkapa kalipiwa na Kofi Anan ama NGO zao za kimataifa. Kuna kitu hapa. Tusimwangalie Mkapa tuangalie fedha.

Halisi,
Je mahindi ni bora kuliko Masiha ya wakenya Amabo walikuwa wakiuana kila siku>?Je ni hivyo unafanya kwa jirani yako?embu ukichukua hivyo vivyo sivyo ulivyouliza kwamba kama watanzania wakiambiwa watoe pesa ili kuokoa maisha ya jirani au wanunue Chakula cha Ziada wangechagua jambo lipi?

Gembe, kupanga ni kuchagua. kuna mtu hapa alisema nishati si suala la usalama wa taifa na wewe unaweza kusema mahindi/chakula si maisha na si usalama wa taifa. Sina pingamizi na wewe kama ni kweli kwamba kama si Mkapa kwenda basi suluhu ya Kenya isingekuwapo, lakini wakati ule tuliambia kwa kelele nyingi kwamba Kikwete ndiye aliyewasuluhisha Wakenya. Lakini jambo la msingi hapa ni kwambe, Je, fedha hizo zimetumika kweli? Je, ni bajeti halali? Je, nani anawajibika kulipia gharama za usuluhishi na ni nani aliyemtuma ama kumuomba Mkapa? Je, alikwenda kwa kivuli gani, UN, AU ama wastaafu? Nadhani kupanga ni kuchagua, ama kusuluhisha Kenya, Zanzibar ama kuchangua huduma za jamii ndani ya nchi yetu. Ndio maana Zitto alisema ni lazima Usalama wa Taifa warudi kazini ki kweli kweli ndipo utaona, kama tulinufaika ama kuathirika na matatizo ya Kenya? Kumbuka pia "kufa kufaana"
 
napendekeza pesa zote za richimunduli,aka dawson,EPA,na za vijisenti zitumike kujenga hospitali tatu kubwa na kuwekewa vifaa vya kisasa kabisa.na kila mwaka tuhakikishe tunajenga hospitali moja kila mkoa,kwani pesa tunazo.
 
Unaweza kukuta Mkapa kalipiwa na Kofi Anan ama NGO zao za kimataifa. Kuna kitu hapa. Tusimwangalie Mkapa tuangalie fedha.

Haswa,
tusiangalie mtu, tunagalie mali ya taifa, manake tukishikia bango watu badala ya ishu hatufiki mbali, akijichomoa, tunabaki hatuna kitu wala mtu.
sisi tunachohitaji ni kujua matumizi ya pesa zetu basi.
 
Back
Top Bottom