Huku wakiwapumbaza watanzania kwa Mpira, nyuma ya pazia wanauza Nchi

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,504
51,099
Ndani ya wiki hizi mbili kuna mambo ya kutisha yanaendelea nchini. Lakini kwa kuwa watawala wamegundua akili za Watanzania ni kufuatilia vitu vyepesi, wameamua kuinvest kwenye mpira wakati huku behind the scene wakiwa busy kuuza nchi na kupalilia ufisadi. Haya ni baadhi ya mambo ya kusikitisha yanayoendelea nchini ndani ya wiki hizi mbili

1. Waziri atoa rushwa ya mitungi 100 kwa kila mbunge
Wakati watu wakiwa busy kufuatilia kama Yanga atatwaa kombe, Waziri mwenye dhamana ya nishati amegawa mitungi 100 ya gesi kwa kila mbunge bure. Dhahiri shahiri hii ni rushwa, tena imetolewa bungeni na tena bila aibu spika ameibariki na kuitetea.

Wakati mwingine unajiuliza spika ana maslahi gani katika hili, utagundua kuwa anamaslahi mara mbili. Mosi, mume wake ni bosi pale EWURA, kwa hiyo spika ana conflict of interest kwa jambo lolote linalohusu EWURA litakaloletwa bungeni. Pili na yeye spika ni mnufaika wa mitungi mia ya bure!
Hii nchi inakwenda wapi?

2. Kuuza bandari
Hii kampuni ya Dubai iitwayo Dubai Ports(DP), imekuwa ikijaribu kutwaa Bandari mbalimbali. Mwaka 2006 ilijaribu kutwaa bandari huko Marekani lakini bunge la Marekani (Congress) lilipiga kura kukataa utwaaji huo.

Hata hivyo DP ilikuwa ikipigiwa chapuo na rais wa Marekani wa wakati huo George Bush. Kutokana na pressure kubwa ililzamika kampuni hiyo iuze share zake kwa kampuni ya Marekani ndo ifanye shughuli hizo.

Leo Samia anataka kutuletea yaleyale ya George Bush.

3. Kuna kila dalili kuna mkono wa CIA katika hili deal
Katika kujaribu kucounter nguvu ya China katika uwekezaji wa infrastructures hasa Africa, USA na washirika wake wanatumia front companies ambayo wamekita mizizi yao ili kutwaa hizi assets.

Hii move nina wasiwasi inaweza kuathiri uwekezaji wa Wachina katika bandari mpya ya bagamoyo. Na ni dhahiri Mmarekani hataki mchina ajenge hiyo bandari. Sasa swala hapa siyo kwamba kwa nini uwekezaji wa China kwenye bandari ni sawa ila wa Dubai ni no!. Jibu ni simple, Dubai wanaenda kufanya kitu rahisi ambacho sisi tukiacha uzembe na uvivu tunaweza kukifanya sisi wenyewe, wakati mchina anaenda kufanya kitu kikubwa!.

Kama tumewahi kukataa mchina asijenge bandari kwa sababu angeioperate kwa miaka takriban 40, Iweje leo tuone eti Dubai ipewe deal la miaka lukuki kwa kitu ambacho kimsingi kipo?

Mkapa aliuza NBC kwa makaburu kwa bei chee akaishia kujuta, Samia sasa anataka kuuza bandari kwa ahadi feki za modernization!.

WEKENI MKATABA WAZI TUUONE!
 
Ndani ya wiki hizi mbili kuna mambo ya kutisha yanaendelea nchini. Lakini kwa kuwa watawala wamegundua akili za Watanzania ni kufuatilia vitu vyepesi, wameamua kuinvest kwenye mpira wakati huku behind the scene wakiwa busy kuuza nchi na kupalilia ufisadi. Haya ni baadhi ya mambo ya kusikitisha yanayoendelea nchini ndani ya wiki hizi mbili

1. Waziri atoa rushwa ya mitungi 100 kwa kila mbunge
Wakati watu wakiwa busy kufuatilia kama Yanga atatwaa kombe, Waziri mwenye dhamana ya nishati amegawa mitungi 100 ya gesi kwa kila mbunge bure. Dhahiri shahiri hii ni rushwa, tena imetolewa bungeni na tena bila aibu spika ameibariki na kuitetea.

Wakati mwingine unajiuliza spika ana maslahi gani katika hili, utagundua kuwa anamaslahi mara mbili. Mosi, mume wake ni bosi pale EWURA, kwa hiyo spika ana conflict of interest kwa jambo lolote linalohusu EWURA litakaloletwa bungeni. Pili na yeye spika ni mnufaika wa mitungi mia ya bure!
Hii nchi inakwenda wapi?

2. Kuuza bandari
Hii kampuni ya Dubai iitwayo Dubai Ports(DP), imekuwa ikijaribu kutwaa Bandari mbalimbali. Mwaka 2006 ilijaribu kutwaa bandari huko Marekani lakini bunge la Marekani (Congress) lilipiga kura kukataa utwaaji huo.

Hata hivyo DP ilikuwa ikipigiwa chapuo na rais wa Marekani wa wakati huo George Bush. Kutokana na pressure kubwa ililzamika kampuni hiyo iuze share zake kwa kampuni ya Marekani ndo ifanye shughuli hizo.

Leo Samia anataka kutuletea yaleyale ya George Bush.

3. Kuna kila dalili kuna mkono wa CIA katika hili deal
Katika kujaribu kucounter nguvu ya China katika uwekezaji wa infrastructures hasa Africa, USA na washirika wake wanatumia front companies ambayo wamekia mizizi yao ili kutwaa hizi assets.

Hii move nina wasiwasi inaweza kuathiri uwekezaji wa Wachina katika bandari mpya ya bagamoyo. Na ni dhahiri Mmarekani hataki mchina ajenge hiyo bandari. Sasa swala hapa siyo kwamba kwa nini uwekezaji wa China kwenye bandari ni sawa ila wa Dubai ni no!. Jibu ni simple, Dubai wanaenda kufanya kitu rahisi ambacho sisi tukiacha uzembe na uvivu tunaweza kukifanya sisi wenyewe, wakati mchina anaenda kufanya kitu kikubwa!.

Kama tumewahi kukataa mchina asijenge bandari kwa sababu angeioperate kwa miaka takriban 40, Iweje leo tuone eti Dubai ipewe deal la miaka lukuki kwa kitu ambacho kimsingi kipo?

Mkapa aliuza NBC kwa makaburu kwa bei chee akaishia kujuta, Samia sasa anataka kuuza bandari kwa ahadi feki za modernization!.

WEKENI MKATABA WAZI TUUONE!
Kama uliyoandika ni ukweli, mtamkumbuka Magufuli sana na kuwalaani hawa akina Samira na Kikwekwe wake
 
Usipoteze muda, iko hivi. Sri Lanka walikuwa na rais kama Dkt Samia, alibinafisisha kwa mtindo wa ubia vitu vingi na kama kawaida project nyingi hizo wale wabia waliweka masharti magumu yaani mnaingia ubia kwa mtindo wa revenue sharing na ikitokea mapato hayatoshi basi inabidi muwe na makubaliano ya obligation fulani ya asset au waichukue hiyo asset waliyowekeza mpaka wamalize mkataba na hela waliyowekeza na matokeo yake Sri Lanka iliingia kwenye kupeana vyeo kwa kujuana kifamilia zaidi na matokeo yake nchi ikafilisika. Tatizo siyo kubinafisisha bali ni usimamizi wa makubaliano.

Yaani unampeleka msukuma kwenda Dubai eti kujifunza aje ashauri nchi???? Yaani kitakachotokea, hawa waarabu wataichukua bandari, watafanya hujama ili ionekane mapato hayatoshi, then wataichukua bandari 100% na asset zingine na wataiendesha kwa miaka 100 plus. Hii kitu haina tofauti na BRN ambayo ilikuwa project hewa aliyodanganywa Dkt Kikwete. Nia ya rais Dkt Samia inaweza kuwa nzuri ila naamini hakuna usimamizi kama wa Dkt Magufuli.
 
Yakiitishwa Maandamano utatoka Barabarani? Au unacho jua ni kulalamika? Sikiliza Malalamiko hayajawahi leta mageuzi kokote kule Duniani
 
Hii akili ya kuuzauza ni akili ya kudumaa. Tulipaswa tujiulize hao Dubai ambao miaka 50 iliyopita walikuwa hohehahe wamewezaje kuinuka?- Siyo sisi tunaenda kugawa rasilimali adimu kama bandari kwa mikataba dubious!

Kagame rais mwenye akili alisema Ukimpa bandari tu, umasikini byebye. Sisi tuna bandari lakini imetushinda!
 
Back
Top Bottom