A
Anonymous
Guest
Kwenye mradi wa SGR huku tunapojenga Reli ya Mwendokasi, hadi kufikia Septemba 2023, imetimia miezi 9 pasipo Mkandarasi wa Mradi Yapi Merkezi kutuingizia malipo yetu katika akaunti za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Kwa ufupi ni kuwa tunakatwa fedha za NSSF kila mwezi kwenye mishahara lakini ukiangalia kwenye akaunti ya mfuko mara ya mwisho wapo waliowekewa malipo yao Januari 2023 na wengine Desemba 2022.
Tumejaribu kuhoji hatukuweza kupata majibu, sasa ukifikiria na hili punguzo la Wafanyakazi haşa kwa kipande cha Morogoro hadi Makutupora unadhani tutapata wapi tena hizo haki zetu?
Hawa jamaa wakikufukuza au ukimaliza mkataba na wasipokuongezea mkataba ukiwa bado unadai, tambua kuwa hiyo imekula kwako.
Kuna kipindi walifanya hivi tukapiga kelele mitandaoni wakaanza kutulipa, sasa wamerudia tena mchezo wao na wanakatibia kutuondoa kwenye ajira.
Wamekuwa wakifanya vikao na sisi Wafanyakazi wakidai wanataka kutoa likizo ya miezi mitatu kwa lazima na ambayo haina malipo, ulishaona wapi likizo ya miezi mitatu bila malipo tena ya lazima, maana yake ni kuwa wanataka tupate kazi kwingine kisha unakuwa umejifukuzisha.
Kuondolewa kwenye ajira si jambo geni, lakini kama wanataka kutuondoa basi iwe katika njia sahihi, wasitishe mikataba, watulipe fedha zetu zote, waingize na malipo yetu ya NSSF tuachane kwa amani.
Kingine tunaambiwa Awamu ya Kwanza na ya Pili ya mradi zimekamilika lakini Watanzania hatujiulizi kuwa kwa nini reli hazijaanza kutumia? Kuna vitu havipo sawa, tuamkeni.
Pia soma - Mkandarasi wa anayejenga Reli ya SGR adaiwa kuyumba kifedha, Serikali yatafuta mbadala kukamilisha ujenzi
Serikali yasema inashughulikia madai ya Wafanyakazi wa SGR wanaodai malipo ya NSSF