Mkakati wa kuwa na Bima ya Afya kwa wote na kuikuza NHIF

Merci

Member
Feb 6, 2012
90
135
Mheshimiwa Rais, naomba upokee maoni haya kuhusu NHIF.

Ili kufikia lengo la afya kwa wote na pia kuwa na NHIF stable, ni vema kila raia wa Tanzania mwenye NIDA hadi watoto wasajiliwe na kuwa wanachama wa NHIF. Michango ya NHIF iwekwe kwenye mfumo wa TOZO kwenye bidhaa kama umeme, maji na mizigo inayoingizwa nchini.

Hii itafanya kila mwananchi wa Tanzania kuwa na bima ya afya na pia upatikanaji wa michango utakua rahisi na pesa ya kutosha. Wananchi watakubali tozo hii kwakua wataona inafaida moja kwa moja kwenye afya zao.

Pia, jambo hili litakua sawa kiuchumi maana gharama kwa wanachi haitakua imewekwa kwenye kitu kimoja na kutokuleta "inflation". Hili litakua jambo jema sana kwa wananchi wako wote wenye vipato vya juu na chini.
Na mwisho, NHIF waanze kutumia mfumo wa biometric technology kuwatambua wanachama wake na kuzuia udanganyifu wa wagonjwa.
 
Umetaja tozo tena? Au sijaelewa?
Yani kwenye kuwa na bima ya wote tozo haikwepeki, lazima hapo serikali uwe na mbinu ya kuchoma fedha kwa kila mtu, kama si kwenye umeme, kwenye maji ama kwenye huduma za kifedha ndio kila mtu akatwe iende nhif, halafu mtu akiwa anaumwa ndio atatibiwa bure ama kwa gharama za chini
 
Bado hamjatosheka na hizi tozo zilizopo mvaa kibendera na bibi yake hawana wanachojua zaidi ya tozo.

Wasahapata wazo jipya hapa.
 
Back
Top Bottom