Akilihuru
JF-Expert Member
- May 20, 2022
- 1,444
- 2,833
Naomba nitoe salam kwa member wenzangu wa JF.
Kwa mara nyingine, leo nawaletea historia ya mwanamasumbwi bora wa kike wa muda wote, na wa uzito wote (The GOAT) Laila Ali au unaweza kumwita 'She bee stingin' ni mtoto wa King wa mchezo huo duniani Muhammad Ali 'The Greatest'.
Laila Ali alizaliwa Dec 30, 1977. Huko Miami beach, Florida nchini Marekani. Pamoja na kusomea mambo ya biashara, kupata shahada mbali mbali na kumiliki baadhi ya biashara zake mwenyewe including kuanzisha kituo cha TV, kumiliki saluni nk.
Kama wasemavyo waswahili kuwa mtoto wa simba ni simba au maji hufuata mkondo, Laila alijikuta anaingia katika mchezo wa ngumi na kujizolea ushindi mkubwa katika mchezo huo wa pili kwa mashabiki duniani kama ilivyokuwa kwa baba yake Muhammad Ali. Alijiunga rasmi na mchezo huo mwaka 1999 na kustaafu mwaka 2007.
Katika historia yake ya miaka 8 katika mchezo huo, aliingia ulingoni kupigana mapambano 24 na mabondia tofauti tofauti. Na katika mechi zote hajawahi kupigwa hata moja.
Ameshinda mapambano 24.
Kati ya hayo mapambano 24, mapambano 21 alishinda kwa KO, na matatu kwa ushindi wa point, huku akiwa amewaacha wapinzani wake katika hali mbaya ya kipigo kikali kutoka kwake. Alistaafu huku chama cha mchezo huo kikiwa bado kinamuhitaji kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao katika mchezo huo.
Huyo ndio Laila Ali aka She bee stingin, Pretty baby au Madame Butterfly ambae alikuwa kipenzi kikubwa cha baba yake Mohammad Ali.
Hapo chini nitaweka picha mbali mbali za ushindi wake
Laila Ali baada ya ushindi akiwa na baba yake mzazi ambae pia ndio King wa mchezo wa ngumi duniani Mohammad Ali (The Greatest)
Laila akiwa tena na baba yake Muhammad Ali, baada ya ushindi.
Laila Ali akiwasulubu wapinzani wake kisawa sawa.
Laila akiwa na tuzo zake
Enzi za baba yake Muhammad Ali