Mjadala: viongozi au wawakilishi?

KXY

JF-Expert Member
Dec 31, 2011
880
327
Nawasalimu wakuu!

Wana jamvi naomba tusaidiane mawazo na tuelimishane kuhusu huu mjadala, kipi ni kipi, kiongozi ni mwakilishi, mwakilishi ni kiongozi au yote majibu/si majibu?

Ili kupata mwanga ni vizuri kujua maana ya haya maneno, samahani nitatumia tafsiri zake za kiingereza ili niweze kunukuu(nimekosa kamusi pepe/softcopy)

lead·er
noun
1. a person or thing that leads.
2. a guiding or directing head, as of an army, movement, or political group.

rep·re·sent·a·tive
noun
1. a person or thing that represents another or others.
2. an agent or deputy: a legal representative.
3. a person who represents a constituency or community in a legislative body..

Kutokana na maana hizo hapo juu(kwa uelewa wangu), kiongozi ni mtoa muongozo na uongozi wake utatumia utashi wake zaidi anaweza kuwashirikisha au asiwashirikishe katika maamuzi anayochukua kikubwa awe na ushawishi kwa kundi lake.
Tukija kwa mwakilishi huyu jukumu lake kubwa ni kuwakilisha waliomtuma na sio kufanya kile anachofikiria yeye, ukifikiria kiundani zaidi dhana ya uwakilishi ni vyema anayewakilisha akiwa na maono sawa na anaowawakilisha ili aweze kuamini katika anachokipigania.

Kutoa mfano wa maana hizo hapo juu, Mh Mbowe ni kiongozi wa chama chake na ni mwakilishi wa jimbo lake kama mbunge.

Kuna mwanafilosofia mmoja wa karne ya 18 Edmund Burke alitoa kauli iliyoleta utata kuhusu uwakilishi, alisema;

“A representative owes the People not only his industry, but his judgment, and he betrays them if he sacrifices it to their opinion.”

Kwa maelezo ya huju jamaa ni kwamba mwakilishi anatakiwa asimamie maamuzi yake hata kama yatapingana na maoni ya anaowawakilisha. Huu ni uwakilishi au ni uongozi?

Nimeweka hii mada jamvini ili tuweze kufahamu nani ni nani katika jamii yetu na ana majukumu gani. Tukiweza kujua yupi ni kiongozi na yupi ni mwakilishi na tukijua maana ya hizo nafasi tunaweza kutambua mjumbe, mbunge, waziri na wengineo wanatakiwa watufanyie nini.

Naomba mchango wenu wadau, tunaweza kuwatumia hawa na wengine kama mifano, wabunge, mawaziri, madiwani, Rais.

Nawasilisha,
KXY.
 
Salaam KXY !

Uongozi ni muktadha wa utaasisi japo si falsafa zote nyuma ya taasisi za leo za mwanadamu ni kamili ama tuseme timilifu. Ndiyo maana katika kisomo cha darasani, ufafanuzi rahisi wa kiongozi ni 'Mtu mwenye madaraka katika jamii'. Sasa utajiuliza tena, madaraka ni kitu gani?

Madaraka ni sehemu ya muundo wa kujiendesha kwa jamii ili kudumu na kustawi. Adili la muundo wa jamii wa jamii inaweza kuwa ni nasibu; kadri watu wanavyokuwa waadilifu kwa kile chenye kuwaweka pamoja kwa jinsi ya fikra, mawazo, hisia na imani basi hao watakaa pamoja na kugawana majukumu ya shughuli zinazofanya sura ya jamii yao. Ikiwa sehemu ya watu katika jumuiya wataacha kuwa na fikra zenye mshikamo basi jamii hhiyo inaingia kwenye nasibu ya mvunjiko.

Mataifa huinuka na mataifa huanguka kutokana na sababu za kuhafifika kwa utii wa adili ama mwelekeo wa jamii kuelekea adili jingine lililobora zaidi... Uongozi kwa mfano ni taasisi ya karibu zaidi na kule kushikiza adili katika makundi ya watu. Uongozi huwa ni kielelezo cha nguvu ya kuwaweka watu katika milki moja na namna ya yake ya utambuliko dhidi ya nyingine yenye muktadha kama wake.

Kulingana na asili ya utaratibu wa ushirika wa taasisi, kiongozi anaweza kuwa muwakilishi ama mtawala. Uongozi unaweza kuwa ni amana--tunu anayokabidhiwa mtu kulingana na utaratibu fulani na kwa mfumo fulani ulioshika hatamu ndani ya jumuiya. Mfumo ndiyo unafanya nani aingie na kutoka lini ili kupokezana amana hiyo kwa tija zaidi ya maslahi ya jamii nzima. Namna hii ya uongozi huambatana na muktadha wa itifaki--ilivyo muktadha wa mila; katika kufafanua mahusiano ya mtu mmoja na nidhamu ya kujiwakilisha mbele za watu akiwa kama kiongozi vile vile yafanywayo na yule asiye kiongozi kuelekea kwa kiongozi. Huu ni mwanzo wa urasmishaji wa taasisi; mpangilio wake na ushawishi.

Haya yote yanahusu katika modeli ya jamii yenye mfumo wa kujifungua kwa ndani. Upo muktadha mpya uongozi ambao mimi kama mtu ninapendekeza kwa siku hizi na zama hizi. Huu ni mfumo wazi wa uongozi.

Mfumo wazi wa uongozi ni dhana inayopelekea kuwa--uwezo na sifa ya mtu kuongoza katika muktadha wowote wa taasisi unategemea uhuru wa elementi za taasisi kuwezekana kupanguliwa na kupangiliwa upya kwa namna mbalimbali na hivi kupelekea hadhi na sifa tofauti ya taasisi kwa wakati hata wakati. Kwenye mfumo uliojifungia sehemu ya utaratibu wa mtu kutenda ni maelekezo yatokanayo na kile chenye maridhiano miongoni mwa jamii kwa sheria na taratibu za kufungia mipaka ya jambo.

Katika mfumo wazi, dhana isiyomaarufu na isiyotumika sana kwa siku hizi, hakuna sheria yenye kubana hasa ila tu mapana ya shughuli, harakati na pilika za jamii kwa ukundiko wenye kueleweka vizuri na kila mjumbe afanyaye idadi yake. Wafanyao ushirika kwa namna hii, ni wenye kukidhi haja ya kuwa na maarifa na upeo wa daraja fulani lililo la msingi na wastani kwa wote, kuleta tija katika ule 'utabia wa kishirika'--lakini mtiririko wa vitendo vyao upo katika njia/kanuni zinazoruhusu mtu mmoja mmoja kuwezekana kuboresha muktadha kitendo na hivi kuongeza tija na kuinua daraja la hadhi ya shirika nzima.

Ninatumia usanifu wa modeli hii mpya ya uongozi katika kutengeneza mashauri ya sura mpya kuendesha biashara na basi kubadilisha hadhi ya uchumi wa dume wa leo. Uchumi ukibebea hadhi hii ya mfumo wazi unapata sifa ya kuwa 'Uchumi Mama'--sehemu ya ufafanuzi wangu juu ya huu upo kwenye uzi 'Introduction: Social Entrepreneurship Synthesis' katika Jukwaa la Elimu....

Kuna namna hii, mtu yeyote katika utaasisi anaweza kuwa ni kiongozi--kwa minajili ya utaratibu wake, Uongozi ni kuchagua-- si nafasi/wadhifa. Upatapo wazo bora kuhusu kubadili sura ushirika wako na wewe, kwa kupitia nguzo za mwongozo wa modeli ya ushirika katika mfumo wazi; kuchagua kuongozea katika hilo, basi wewe ni kiongozi. Je, unaweza kubuni namna ya ushirika na taasisi za namna hii? Hii ndiyo changamoto inayopasa kuwa vichwani na moyoni mwa wengi sasa.

Naomba nikatishe mtiririko wa mashauri hapa, nikukaribishe katika uzi huo pia.

Hakika kuna mengi ya kumulika.

Baraka
 
Ubarikiwe pia mose!

Nimeuona huo uzi, link hii hapa

naomba ufafanuzi katika dhana ya uongozi wa uwakilishi, majukumu ya kiongozi wa aina hii ni yepi na anajitofautisha vipi na kiongozi mtawala?
 
KXY, upendo,

Swali uliloweka kwangu sina jinsi ila kubaki kwenye mashauri ya kifalsafa...

Dhana ya 'Mtumishi' na 'Mtawala' sifa ijayo na ukweli wa kijinsia--Utumishi ni hadhi ya kike na Utawala ni hadhi ya kiume. Labda ninaweza nikakushangaza kidogo nikisema kuwa hakujapata kuwa na 'Kiongozi mtumishi' katika ule uhalisia wa jambo, japo mara nyingine na hasa katika mifumo ya ijayo na taasisi za kileo za serikali huonekana kana kuwa inaelekea katika namna ya kuweka 'viongozi watumishi' katika hatamu.

Pungufu hilo lililotajwa linatokana na uadilifu wa leo uliolemea katika huluka za mifumo dume.

Jingine ninaweza kukuambia lakini linaweza kuwa geni--Uzima wa viumbe hai vyote unavyovijua huja kwa utangamano wa jinsi ya kike na ile ya kiume. Ushirika wowote wa viungo vya mwili mmoja ukidumu katika hivi ndivyo 'afya' na bukheri inahusu. Asili ya kiume husonga kuelekea 'Nguvu' na hali ile ya kike 'Hutunza' na kutimilisha mahitaji kimwili wowote wenye kuja kwa asili ya namna yake.

Katika Jumuiya yeyote, asili ya kike na kiume lazima kuwa ni sehemu ya mfanyiko wa milki na ustawi. Utawala una mipaka kwa milki yake kwa kuwa ni hiyo inayotathminisha vinono ya kufaidiwa na watu wake. Vinono vya kuneesha watu katika ardhi ndiyo huchora na kudhihirisha picha ya uchumi kama mwili wa mabadilishano, mtegemeano na uhusiano kwa vizio vyake vyote vya kutoka kaya ndogo ndogo hata kuelekea katika matabaka. Ujumla wa watu wote na fahari yao kuwa ni taifa, dola na hata himaya kwa sifa mahususi za utaasisi wake mkuu--wenye kukutana uso kwa uso na taasisi zingine kwa mahusiano yake ya kimipaka. Kwa asili ya Mama Dunia, hakuna nchi yeyote iliyo ni kisiwa hasa ila tu ni binadamu wanapendelea kubuni na kuchora mipaka yako juu ya uso wa dunia ili kudumisha utaasisi wao wa kinchi.

Dhana ya Jamhuri kwa mfano, ni nchi ya watu yenye serikali--yenye 'viongozi' wenye kuwawakilisha wananchi ili kupambanua muktadha wa ustawi wa kaya za wake kwa waume na watoto na maslahi yake kitaifa. Yumkini kuna miundo mingi ya kiserikali lakini kiini ni 'Utambuliko'. Kama vile kaya hutambulika kwa ukoo, utaifa ni kuhusu 'Jina' pia. Mtu yeyote akisimama hutaka kutambulika yeye ni nani na miongoni mwa akina nani basi kwa upande mwingine. Hulka hii rahisi--amini usiamini ndiyo kiini cha michakato yake yote.

Kulingana na historia na uzoefu wa mwanadamu, 'Jina na utukufu' vimekuwa ni lulu ya kujipambanua na vile vikomo vya uwezo wa uzalishajimali kwa mfano, vimepelekea ile silika ya 'Will to Power--Nia kuelekea Mabavu'--usemi wa Friedrich Nietzche; kuchukua mkondo wake. Kutokana na silika hii, adili kuu kwa mapana ya jamii nyingi kwa miaka na miaka, zama na zama limekuwa likitafuta kujinasibu na ule uwezekano wa 'Super Structure--Muundiko Mkuu'--usemi wa Walter Rodney; yenye mfano wa Kiume. Sehemu ya kuwa mataifa mengi kwa mfano mungu huwa na jinsia ya Kiume si lolote ila tu kuwa ni muakisiko wa hamu ya wengi kudhani fahari kuu ya uzima wote labda ni sharti kuwa ni ya 'Kiume'...

Sasa adili la kiume ndiyo sababu ya dola zote na himaya zote zilizofaulu kufikia vilele vya 'udume' kuanguka; kwa kuwa nguvu ya kiume bila kutangamana nyingine ya kike husonga halafu ikaishia kwenye kule kubomoka--isirudi tena upya. Kufahamu hili kwa kina na sura mbali mbali inafanya kuwa ni rahisi kutabiri kwa nini Marekani itaanguka kidola na uchumi--hata China inayoonekana kuimarika itafikia nasibu ya kikomo hicho hicho. Siku zote katika kilele cha tawala kwa adili la mfano wa kiume, mwamuzi wa mwisho kwa ubatili wake ni 'Uchumi'. Hii ndiyo jinsi asili ya kike hujirudishia zake kudhalilishwa, kutoheshimika na kutambulika kwake--Taifa moja huinukia lingine ili kupora na kuubaka utajiri wa lingine. Ama kwa ulimwengu wa leo ulina maarifa zaidi, taifa moja litajaribu kuhujumu lingine ama hata kutishia vita lingine ili kuonekana lenyewe ndiyo lenye nguvu ya kijeshi na utawala bora kuzidi mengine...

Tawala za leo za serikali zinafuatisha maoni na falsafa za wafikirifu wa siku za utaamuliko huko Ulaya kama akina Montesque, kufuatia mashauri ya wafikirifu wa zamani wa Kigiriki--ni yeye aliyejadili juu usukaji wa taifa kwa mtenganisho wa matawi makuu matatu katika kinachotajwa vile vile ni kusawazisha nguvu. Shauri hili ndilo limeleta mihimili mitatu ya dola; na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mfano inafuatisha itikadi hii. Montesque alipendekeza utaasisi wa dola unaoenenda wa mfumo wa kujifungia ndani. Kuona kwake kuwa mkataba kati ya watawala na wataliwa ni wajibu kuakisi 'utumishi' na 'uwakilishi', basi yeye alisema kuwepo na namna ya mihili mitatu ya dola--baraza la kutunga sheria, mahakama na mwili wa watendaji wa serikali katika serikali. Mwili wa watendaji kwa mfano ni chombo kinachosimamia utekelezaji wa maagizo ya mihimili yote miwili iliyobakia ikiwemo kuhakikisha sheria za nchi zinazingatiwa kote juu ya nchi ambapo Sheria hizo zinatungwa na kupitishwa na wajumbe wa baraza la kutunga sheria kwa utaratibu wa chombo chao na kwa kupande mwingine Mahakama inasikiliza na kuamua mashauri yote juu ya 'Utekelezaji wa Haki'.

Ufikirifu wa Montesque si muundo kuelekea katika 'mfumo kamili'... Ni wazi haya yote yamekuwa mawazo na mabadiliko juu ya adili kuu kuongoza taifa lakini harakati za kutafuta maridhiano kamili zimekuwa zikiendelea. Katika usanifu huu kwa mfano, mwanabaraza la kutunga sheria kwa kuwakilisha kwake raia wa jimbo lake katika mchakato wa bunge; yeye ni kiongozi--kwa maana mtiririko wa vitendo vyake vinaukaribu na watendaji wa serikali wanaotekeleza maazimio na makusudio makuu ya shughuli za serikali. Wanapopeleka sauti ya wawakilishwaji wao ni watumishi, wanapoongoza mipango ya utekelezaji na nafasi yao kama wadau sambamba wa shughuli za serikali wao viongozi. Lakini kwa kiasi gani hawa ni 'viongozi watumishi'? Labda dhana ya uongozi wao ni wadhifa/madaraka ya kiofisi na ile nafasi yao katika muundo mzima wa vyombo vya utawala. Na ndivyo hivi ukomo wa utendaji wao 'unatawaliwa' na 'Sheria za Nchi'. Sheria Mama ya zote ni muktadha wa maelekezo ya Utaasisi mzima wa Jamhuri unaoitwa ni Katiba. Ikiwa tunataka kufanya mfumo huu usiwe ni wenye hadhi ya kujifungia ndani hatuna budi kubadili muktadha wa katiba na kusanisi uhusiano kati ya 'Sheria' na 'Miundo' ya taasisi... Hili linahitaji upeo wa kutosha kwa raia wote na kuifafanua upya misingi ya haki isitegemee 'mashauri ya kupitishwa' kama sheria ila kuwa ni mbegu fulani za kweli za maumbo yenye 'hadhi ya Uzima'. Jambo pekee lenye kuweza kunasibisha hili ni kurudisha utangamano wa jinsia ya kike na ya kiume kwa ngazi ya vyombo vyote vya jamii--maarifa yaliyokosekana miongoni mwa 'Viongozi' wa kisiasa na wanavisomo wa leo... Inawezekana kuna adha ya mifumo na kujikita kwa taasisi za watala zinakwamisha nuru za visomo vipya--kwa vyovyote vile sasa tumefika katika hitaji hili na hasa.

Serikali kwa mfano, japo leo nyingi zimetawaliwa na mifumo ya tawala za kisiasa. Tabia ya watu kufikiri serikali ni ya kutegemewa inakuja kutokana na fikra finyu za kuiona hiyo kama 'baba' atayepaswa kuleta mkate kwa mtaji wa nguvu zake; kama vile hiyo ndiyo 'kichwa' cha yote... Ukweli ni wanasiasa ndiyo wanaofaidika na ujinga wa wengi kutoelewa vizuri muktadha wa nchi zao kufanyika. Mifumo ya utawala imetaasisha mchakato wa vyama vya kisiasa kupokezana hatamu kwa kugombea nafasi za 'kuongoza' serikali kwa misingi ya utaratibu wa kura za raia. Kuna udhaifu mkubwa kabisa katika michakato ya leo hii ya kile kinachoitwa ni 'Demokrasia' lakini itoshe kusema, kuhama kutoka kwenye mifumo ya kujifungia ndani na kuingia katika mfumo wazi demokrasia itakufa na kufufuka kujakudhahirika ni muktadha wa upacha wa mawili--mkondo wa tekinokrasia na mkondo wa meritokrasia. Viwili hivi ndivyo vitatimiliza sura ya serikali ya watu waliotaamulika na kutosheleza utangamano wa hadhi kiume na ya kiume kwa wakati.

Katika mpangilio wa mambo duniani leo hii, muktadha wa huduma kwa jamii katika serikali umetengenezewa muundo wa wizara zilizo chini ya taasisi wa Urais ama Cheo kama hicho--kufanya wizara zote ziwe zinaratibiwa katika mtindo usio wa asili ya namna nyingine ila tu kule kutaasisha mnyororo wa maamuzi, amri na mamlaka... Ndivyo hivi hata kushughulika na mapana ya ustawi wa jamii huja kwa ufanisi wa kusua sua karibia siku zote tena kwa kuzongwa na matumizi mabaya ya ofisi za umma na ama upendeleo wa matunda ya 'haki' kwa matabaka yenye aidha kufungamana na nguvu za kibiashara ama umaarufu fulani. Hii ni kwa kuwa wanadamu wakikosa nuru kwa haki na hekima, huzaa namna ya mioyo yenye uchafu--yenye kuelekea katika makusudio yenye kuharibika upesi. Vile vile ni ukweli kwamba kwenye mifumo yenye asili ya udume, RUSHWA HAIWEZEKANI KUTOKOMEZWA. Haijalishi hata Rais aanzisha taasis ya Kuzuia Rushwa chini ya mamlaka yake--rushwa kuondoka ni muhari.

Ni kwa minajili ya hayo na mengine ambayo sijadadavua hapa ninalingania watu wa Afrika tuamke na kufanya Nchi Mpya... Ninataka tusimame na kusonga mbele zaidi kuliko demokrasia na 'shughuli chafu' ya siasa na ili kufanya 'Mama Afrika', bara la mfano ambapo kila mtu ataishi kwa nuru ya kheri na haki, neema, heshima ya utu, fanaka na kile nitachokizungumzia kama 'Liberiti'...

Tunahitaji kusuka ndoto pamoja--'Ndoto Afrika'; tunahitaji mwongozo wa elimu sahihi--tuuite huu 'Liberiti Afrika'...

Baraka
 
  • Thanks
Reactions: KXY
Mose anaandika kuliko hata Mzee Mwanakijiji! hivi huwezi kutupa ka summary?
nikimaliza kusoma na nikifikiria kuanza kujibu mwanzo hadi mwisho naona niache tu...
 
Mose anaandika kuliko hata Mzee Mwanakijiji! hivi huwezi kutupa ka summary? nikimaliza kusoma na nikifikiria kuanza kujibu mwanzo hadi mwisho naona niache tu...
hahahaa..summary ya Mose utaielewa kweli?
 
KXY, upendo,

Tunahitaji kusuka ndoto pamoja--'Ndoto Afrika'; tunahitaji mwongozo wa elimu sahihi--tuuite huu 'Liberiti Afrika'...

Baraka

Nashukuru kwa maelezo yako ya kina.

Picha niliyoipata ni kwamba adui yetu si yule tunayeaminishwa kuwa ni adui bali mfumo mzima ndio adui namba moja. Huwa napata shida sana kukubaliana na mfumo wa kuchagua viongozi tuliochaguliwa, yani mchague huyu au yule kwa maana nyingine mtu mmoja tu mwenye ushawishi mkubwa(kisiasa au kiuchumi) anaweza panga safu ya wagombea anaowataka yeye na ninyi mchague mmoja kati yao.

Safari yetu ni ndefu na kubadili fikra za watu inahitaji tukio kubwa sana kutokea kwa mfano kuanguka kwa taifa la Marekani, watu wanapenda kuiga penye mafanikio bila kuangalia gharama ya mafanikio hayo.
 
Mmeamua kuwa wanafalsafa sio, tunafuatilia kujua nani mfuasi wa plato na nani mfuasi wa aristoto kisha tutawapambanisha na socrates.
 
Mmeamua kuwa wanafalsafa sio, tunafuatilia kujua nani mfuasi wa plato na nani mfuasi wa aristoto kisha tutawapambanisha na socrates.
Mkuu watu wameenda beyond uliowataja sasa na wao watukuwa na wafuasi wao..are you in???
 
Back
Top Bottom