Mjadala: Tatizo la kujieleza kwenye usaili wa kazi

Nitasema machache:

1. Hakikisha CV yako ni yako kweli (usiandike sifa au uzoefu ambao huna!). Kama ni kazi inayotaka uzoefu, maswali mengi yatataka kutest uzoefu wako katika maswala kadhaa. Ni vema ukajiandaa vizuri kuelezea kazi ulizokuwa unafanya, mafanikio na challenges ulizokutanana nazo na jinsi ulivyozitatua.

2. Jaribu kufahamu matarajio (requierements) ya kazi unayoiomba. Interviwer mara nyingi atauliza maswali ili kujiridhisha kama kweli you are up to the job!

3. Jaribu kuifahamu kampuni na shughuli inayofanya (bidhaa, wateja, challenges nk). Hii itakusaidia kujibu baadhi ya maswali. Unakuta mtu anaingia kwenye interview hata jina la kampuni anayoomba kazi anashindwa kulitamka kwa ufasaha halafu eti anaomba kazi ya kuwa afisa uhusiano!

4. Jaribu kufuatilia mambo mbalimbali yanayoendelea duniani(Current issues) na jinsi yanavyohusiana na kazi unayoomba au kampuni au tasnia inayokuhusu.

5. Hobbies,interests etc. Mara nyingi watu wanajiandikia tu kwenye CV hata vitu ambavyo kiukweli hawana interest navyo. Ukisema unainterest na football basi hakikisha kweli unafahamu mambo kadhaa kuhusu football. Au kama unasoma novel, basi kweli iwe unasoma. Si unaulizwa angalau uelezee kwa ufupi novel uliyoisoma karibuni, unaanza kujiuma hata title au muhusika mkuu humkumbuki!

nk, nk, nk

Kuna usaili mwingine, hasa wa nafasi mpya inayoanzishwa katika ofisi ambapo mwajiri anaaangalia karama(talent/potentials) zaidi kuliko elimu na vyeti. Nia hasa ni kutaka kujiaminsha kuwa UNAFUNDISHIKA. Katika hali hii kuwa mtulivu, yafahamu vema yalyo katika Wasifu yako kwani sehemu kubwa ya maswali ya usaili yatategemea huo wasifu wako.
 
mdau mmoja ametoa ushauri mbaya huwezi kumwambia aombe aulizwe kwa kiswahl watakumwaga faster coz inst. nyingi wanataka ujue lugha zote mbili,tchao
 
Vile vile unapojibu maswali uwe na mifano ili kuonyesha kuwa unafamu unachosema.
Mwisho wa interview (kwenye kuuliza maswali) jaribu kuuliza maswali kuhusu kampuni au shirika lao kwa ujumla (fanya research kabla).. hii inaonyesha kuwa upo keen!!

Kumbuka interview sio CV au unavyojieleza kwenye panel tu. Kuna vitu kama appearance na unavyoongea pia (character) ..wao wanaangalia mtu ambaye ata fit kwenye jamii/team yao kiujuzi na tabia pia!!
 
Kwenye Usaili vaa hivi

1. Suti- pendelea sana kuvaa kutokana na nature ya kazi uliyoomba, usivae suti tu inawezekana kazi unayoomba inahitaji mtu anayevaa simple tu. Angalizo hiyo ‘simple' uingalie pia

2. Kwa wanawake kama umevaa blauzi basi nagalia ile ambayo haitakuacha sehemu kubwa ya kifua na matiti yako wazi


3. Kwa wale wanaopenda kuvaa pete wanaume na wanawake waangalie aina ya pete watakazovaa, inapendeza kama una ya uchumba au ndoa, zile za urembo pete tano achana nazo siku ya usaili

4. Aina ya nywele hasa kwa wanaume ni suala la kuangalia pia kwa umakini, kwa wanawake pia


5. Unapoenda kwenye usaili kumbuka pia kuwa na mkoba mzuri wa kubebea document mbali mbali, hii itaonyesha ulivyo smart katika kuhandle vitu vya muhimu

6. Kumbuka pia kuvaa saa, sometimes unaweza kuulizwa muda ukaanza kung'aang'aa sharubu na kujikuta pia unachemka


7. Pia kujiremba kwa herreni ni sual muhimu kwa wanawake inabidi waangalie aina ya hereni lakini kwa wanaume please unless………….

Pia unaweza kusoma Mwananchi Disemba 9, 2009
 
Please any input here
I believe many people want to keep on learning
this is progressive lesson of all the time
 
Kikubwa kinacholeta matatizo ni kujitambulisha wewe mwenye kwa wanapanel.

Hivi unatakiwa uishie kwenye elimu au mpaka kazi unayoifanya kwa sasa au? msaada plz
 
kuvaa kiofisi, kufika mapema katika eneo la usahili, kujiandaa kisaikolojia hasa kwa kujiuliza maswali ambayo unahisi unaweza kuulizwa, ni vyema kuuliza watu wenye uzoefu na usahili ili wakupe michango yao, uwe na uhakika na unachokijibu, kama hujui sema 'haujui' na utakifanyia kazi, usitetemeke, kabla ya usahili vuta pumzi kwa nguvu, usiongee haraka haraka! pia usivae nguo ambazo hunamazoea nazo kiasi cha kukufanya usiwe huru!

Nimependa hii mada ila wengine ni waoga sana kiasi ile kuona tu panel ya watu zaidi ya five, basi hupata kigugumizi hata jina lake hakumbuki. Sasa huyu tutamsaidiaje?
 
nimependa hii mada ila wengine ni waoga sana kiasi ile kuona tu panel ya watu zaidi ya five, basi hupata kigugumizi hata jina lake hakumbuki. sasa huyu tutamsaidiaje?
Anachotakiwa mtu kama huyu ni kujizoesha kuongea kwenye watu wengi ili kuzoea kadamnasi au watu wengi zaidi. Ni suala la kujiamini tu wala sio ugonjwa huo. Asante kwa kuipenda mada ni kwaajii yetu sote kama jamii kajifunza kwa kubadilishana mawazo na uzoefu hata utaalamu tulio nao
 
Kila unayemwona eneo la interview mchukulie kama panel member, na kama kuna anaegawa magaezi eneo la interview kuwa makini kuwa unasome kurasa zinazoendana na fani yako na sio kukimbilia ukurasa wa michezo hata kama ni hobby yako, by so doing huyo mkuu atakulima maksi maana atakuwa anacheki kiaina unafanya nn na gazeti, be carefull!
 
Unapomaliza interview uwashukuru eg,: thanks for the fair interview and good afternoon/evening/night. Japo intreview yaweza kuwa sio fair. It makes royality
 
Unapomaliza interview uwashukuru eg,: thanks for the fair interview and good afternoon/evening/night. Japo intreview yaweza kuwa sio fair. It makes royality
Kuwashukuru ni jambo la muhimu sana. Thanks kwa kutukumbusha hili.
 
sasa kama kazi uliyoomba unatakiwa kujua kingereza maana yake ndo umeshachemsha
Inabidi kupata data mapema kuwa watatumia lugha gani, obvious the nature of the organisation field will tell you early kuwa kutatumika lugha gani.
 
Mfano mzuri tu nilikuwa tanga mwezi wa saba kulikuwa kuan Interview pale mamkla ya maji walio itwa kwa usahili walikuwa wachache sana 4 ila aliye pata job appearance and dress code was mbaya ilikuwa siyo kiofice wana JF alikuwa anamadevu kama osama shirt ya mikono mireku kakunja amenyoa kipara midevu kaiachia.

Pili swala la muda alichelewa kwanza kama 15mins jinalake lilipoitwa kwaajili ya kuingia kwa chumba cha interview walipotaka kumwita mtu mwingine ndio akawa ametokezea na akaingia sasa hapo niambie FL1 akili yake ilikuwa imetulia kweli na akaweza kujibu vizuri na akapata kazi?? mavazi yake na mwonekano wake tu? Ilikuwaje Meza kuu inayo wasahili ilimpitiusha huyo bwana?? Pili ilikuja kugundulika elimu yake ilikuwa ndogo zaidi kuliko ya wale wengine watatu?

Me nadhani kuna tatizo pia kwa jopo au meza kuuu inayowashili wanaoomba kazi.

Mie kwakweli ktk swala la usahili TZ kunavituko na vimbwanga vingi sana.

Pia walioajiliwa wengi wakuta sio elimu walizo somea na ungugunisation ni mkubwa kupita kiasi.


labda alijuana na panel, hivyo ilkuwa ni interview fake
 
Mkuu umenikumbusha mbali sana. Usaili wangu wa kwanza kabisa nilichemsha kuliko kawaida, kwanza wakati wa kujibu maswali nilikuwa sijatulia kabisa maana nilikuwa naswing kama Hip Hop musician, halafu nilikuwa naongea slang. Nikaulizwa swali: Are you a raper? nikawambia NO, swali lingine; Do you like music? nikawaambia YES, more especially Reggae music. Can you sing one of your favorite songs?, nikawaambia YES nikaanza kuimba wimbo wa Bob Marley unaitwa Ride Nite Ride, niliimba mpaka chorus, nilichoshangaa wasaili wote wakawa wanaangua hawana mbavu. Mwisho wa siku nilikosa kazi, nilipowasimulia masela wangu wakaniambia ,mzee umechemsha sana,how can you sing in interview..From that day nilijifunza kwamba katika usaili ni vizuri kuwa serious, kwa maana ya kuongea kistaarabu, kuvaa kiofisi, kuacha masihara, kujiandaa kwa maswali kama tunavyojiandaa katika mitihani darasani (fanya rehesal before mpe mtu maswali ambayo unathani utaulizwa awe anakuuliza na wewe unajibu). Ukweli toka siku hiyo nimehudhuria karibu interview tano na zote nilifanikiwa kupata kazi, zingine nilizipiga chini kutokana na maslahi.
 
Back
Top Bottom