Mjadala: Tatizo la kujieleza kwenye usaili wa kazi

Sipo

JF-Expert Member
Jul 25, 2008
2,139
91
Kuna tatizo la kujieleza wakati muomba kazi anapoenda kwenye usaili. Uzoefu unaonyesha kuwa wasailiwa wengi huwa wanachanganyikiwa na kushindwa kujibu maswali kwa ufasaha na kujikuta wanakosa kazi.

Thread hii lengo lake ni sisi wanaJF kuelezana mambo ya muhimu ya kufanya/kuzingatia wakati wa kufanyiwa usaili.

Karibuni

---------------
phil_kabuje: Epuka lugha hizi za mwili (body languages) wakati wa kufanya usaili (interview)

1.Epuka kukunja mikono yako kifuani hii huonyesha kujiamini kupita kiasi, dharau au wakati mwingine huashiria kutokubaliana na kile kinachozungumzwa

2. Kama umesimama, jitahidi unyooke, epuka kuegamia ukuta au kupishanisha miguu (kuchora alama ya X). Kama umekaa usiegamie sana kiti kwani hii huonyesha ishara ya uvivu. Kaa ukiwa umenyooka

3. Epuka kuwa wakwanza kukwepesha macho kwa haraka unapomuangalia anayekufanyia usaili au aliyekuuliza swali. Hii huonyesha kukosa kujiamin au tabia ya udokozi. Daima angalia mbele usiiname chini unapoulizwa maswali

4. USITAFUNE KITU chochote mdomoni iwe pipi au vidole vyako (hasa kwa wanawake)

5. Usionyeshe Ishara yoyote mbaya unapomzungumzia muajiri wako aliyepita (hata kama ndiye sababu ya wewe kuacha kazi)

6. Usiwanyooshe vidole wanaokufanyia usaili

7. Usitikise sana kichwa kupita kiasi. Ni vizuri kutikisa kichwa unapoonyesha kuelewa kile unachoambiwa, lakini mara nyingine inawezekana ukaulizwa swali la mtego ambalo hutakiwi kukubali!

8. Usiweke mikono nyuma au mfukoni unapoingia ndani au ukiwa umesimama. Hii hunyesha hali ya kutotaka kuwa muwazi, au majivuno.

9. Unachokizungumza kifanane na uso wako. Mfano unapozungumzia kitu kinachokufurahisha halafu una sura nzito, una hatari! Jitahidi kutoa tabasamu kila unapoulizwa swali au kuelezea kitu

10. Usiangalie sana juu ishara ya kukumbuka kitu. Hii huonyesha kutokuwa na hakika ya kile unachokizungumza!
 
Kuvaa kiofisi, kufika mapema katika eneo la usahili, kujiandaa kisaikolojia hasa kwa kujiuliza maswali ambayo unahisi unaweza kuulizwa, ni vyema kuuliza watu wenye uzoefu na usahili ili wakupe michango yao, uwe na uhakika na unachokijibu, kama hujui sema 'haujui' na utakifanyia kazi, usitetemeke, kabla ya usahili vuta pumzi kwa nguvu, usiongee haraka haraka! pia usivae nguo ambazo hunamazoea nazo kiasi cha kukufanya usiwe huru!
 
JP ya muhimu sana ulosema hapo, plus sikiliza maswali kwa makini, usishushe pumzi unapoulizwa swali (as if kilichoulizwa kimekuchosha), be confident, be honest (kama hujui usisite kusema, kama hujaelewa au kusikia swali vizuri), dont loose focus.
 
Usipanie kujibu maswali kwa pupa, sikiliza kwa makini na wakati wa kujibu husiangalie pembeni au juu au kufikicha vidole. Waangalie wanaokusaili moja kwa moja pasipo kusita wala kupepesa macho kwa uwoga.
 
@Journal Pape,

Ni kweli kuwahi mapema eneo la tukio kunasaidia kukuandaa kisaikolojia kuliko umefika umechelewa kwanza uta-panic.
 
Kuna tatizo la kujieleza wakati muomba kazi anapoenda kwenye usaili. Uzoefu unaonyesha kuwa wasailiwa wengi huwa wanachanganyikiwa na kushindwa kujibu maswali kwa ufasaha na kujikuta wanakosa kazi. Thread hii lengo lake ni sisi wanaJF kuelezana mambo ya muhimu ya kufanya/kuzingatia wakati wa kufanyiwa usaili. Karibuni

Nitasema machache:

1. Hakikisha CV yako ni yako kweli (usiandike sifa au uzoefu ambao huna!). Kama ni kazi inayotaka uzoefu, maswali mengi yatataka kutest uzoefu wako katika maswala kadhaa. Ni vema ukajiandaa vizuri kuelezea kazi ulizokuwa unafanya, mafanikio na challenges ulizokutanana nazo na jinsi ulivyozitatua.

2. Jaribu kufahamu matarajio (requierements) ya kazi unayoiomba. Interviwer mara nyingi atauliza maswali ili kujiridhisha kama kweli you are up to the job!

3. Jaribu kuifahamu kampuni na shughuli inayofanya (bidhaa, wateja, challenges nk). Hii itakusaidia kujibu baadhi ya maswali. Unakuta mtu anaingia kwenye interview hata jina la kampuni anayoomba kazi anashindwa kulitamka kwa ufasaha halafu eti anaomba kazi ya kuwa afisa uhusiano!

4. Jaribu kufuatilia mambo mbalimbali yanayoendelea duniani(Current issues) na jinsi yanavyohusiana na kazi unayoomba au kampuni au tasnia inayokuhusu.

5. Hobbies,interests etc. Mara nyingi watu wanajiandikia tu kwenye CV hata vitu ambavyo kiukweli hawana interest navyo. Ukisema unainterest na football basi hakikisha kweli unafahamu mambo kadhaa kuhusu football. Au kama unasoma novel, basi kweli iwe unasoma. Si unaulizwa angalau uelezee kwa ufupi novel uliyoisoma karibuni, unaanza kujiuma hata title au muhusika mkuu humkumbuki!

nk, nk, nk
 
Wakati wa kujibu maswali kuwa brief, husitumie muda mrefu sana kujibu swali, kwa maaana usaili ni kama mtihani ukiongea sana utapoteza pointi ya msingi.
 
Husionyeshe kuwa umekariri baadhi ya maswali
that means ukiulizwa swali weka pose then ndio ujibu
sio kwa sababu hilo swali ulishalisoma kwenye website au kwenye kitabu then unaposikia linaanza kuulizwa hata kabla muulizaji hajamaliza nawe umeanza kujibu. Acha papara
 
Husionyeshe kuwa .....

Samahani kaka naomba nikusahihishe kdg hapo juu naona una common error ya maneno haya... Husionyeshe inabidi useme usionyeshe, Husitumie inabidi useme usitumie, n.k n.k. Hapo H haihusiki kabisa, samahani nimeona nitoe angalizo hili kwani nimeona hizi common error zinajitokeza sana humu jf. Sorry 4 this

Back to the topic, ni kweli kuingia kwenye intavyuu inahitaji kujiandaa kisaikolojia. Mi intavyuu ya kwanza kabisa kuna vitu kibao nilichemsha na baadae nikaja kugundua kuwa kumbe ningekuwa nimejiandaa kisaikolojia ningeweza kujibu vzr, na kazi nilikosa!! Nawashukuru wote waliotoa ushauri. Mungu awabariki
 
Samahani kaka naomba nikusahihishe kdg hapo juu naona una common error ya maneno haya... Husionyeshe inabidi useme usionyeshe, Husitumie inabidi useme usitumie, n.k n.k. Hapo H haihusiki kabisa, samahani nimeona nitoe angalizo hili kwani nimeona hizi common error zinajitokeza sana humu jf. Sorry 4 this

Back to the topic, ni kweli kuingia kwenye intavyuu inahitaji kujiandaa kisaikolojia. Mi intavyuu ya kwanza kabisa kuna vitu kibao nilichemsha na baadae nikaja kugundua kuwa kumbe ningekuwa nimejiandaa kisaikolojia ningeweza kujibu vzr, na kazi nilikosa!! Nawashukuru wote waliotoa ushauri. Mungu awabariki
Noted with thanks Sir!!!
 
kuvaa kiofisi, kufika mapema katika eneo la usahili, kujiandaa kisaikolojia hasa kwa kujiuliza maswali ambayo unahisi unaweza kuulizwa, ni vyema kuuliza watu wenye uzoefu na usahili ili wakupe michango yao, uwe na uhakika na unachokijibu, kama hukui sema 'haujui' na utakifanyia kazi, usitetemeke, kabla ya usahili vuta pumzi kwa nguvu, usiongee haraka haraka! pia usivae nguo ambazo hunamazoea nazo kiasi cha kukufanya usiwe huru!


ni kweli kuwahi mapema eneo la tukio kunasaidia kukuandaa kisaikolojia kuliko umefika umechelewa kwanza utapanic

Mfano mzuri tu nilikuwa tanga mwezi wa saba kulikuwa kuan Interview pale mamkla ya maji walio itwa kwa usahili walikuwa wachache sana 4 ila aliye pata job appearance and dress code was mbaya ilikuwa siyo kiofice wana JF alikuwa anamadevu kama osama shirt ya mikono mireku kakunja amenyoa kipara midevu kaiachia.

Pili swala la muda alichelewa kwanza kama 15mins jinalake lilipoitwa kwaajili ya kuingia kwa chumba cha interview walipotaka kumwita mtu mwingine ndio akawa ametokezea na akaingia sasa hapo niambie FL1 akili yake ilikuwa imetulia kweli na akaweza kujibu vizuri na akapata kazi?? mavazi yake na mwonekano wake tu? Ilikuwaje Meza kuu inayo wasahili ilimpitiusha huyo bwana?? Pili ilikuja kugundulika elimu yake ilikuwa ndogo zaidi kuliko ya wale wengine watatu?

Me nadhani kuna tatizo pia kwa jopo au meza kuuu inayowashili wanaoomba kazi.

Mie kwakweli ktk swala la usahili TZ kunavituko na vimbwanga vingi sana.

Pia walioajiliwa wengi wakuta sio elimu walizo somea na ungugunisation ni mkubwa kupita kiasi.
 
kiutaalama usaili ni kama sales in marketing,pale unanadi bidhaa zako,kwa suala la kuomba unaenda kuuza sifa na uzoefu ulionao kwa kazi ulioomba yaani hapa muajiri au wakala wa muajiri ni mteja wako.hivyo hakikisha kila unachonadi ni kweli kina sifa hizo.

jambo la muhimu sana uwe tayari kujibu kwanini unataka kufanya kazi na muajiri huyo vilevile kwani umeacha kazi ya mwanzo?

jitahidi kujua scale za mshahara za nafasi uliomba sio tu kwa muajiri huyo muhimu katika soko la ajira sifa zako na uzoefu wako unathamani gani?

Ukipewa nafasi ya kuwauliza swali jitahidi uulize usisime sina swali?
 
Back
Top Bottom