Fahamu maswali ya muhimu unapoitwa kwenye usaili

Wild Flower

Member
Jul 20, 2023
80
96
Moja kati ya Maswali ya mtego unayoweza kukutana nayo kwenye Usaili

Wakati wa Usaili wa Kazi, unaweza kuulizwa Swali kama Tueleze au twambie kuhusu wewe (imezoeleka kusemwa Tell Us about Yourself).

Swali hili halihitaji utaje Jina lako kisha unyamaze kusubiri swali lingine bali Mwajiri hutaka kusikia mambo muhimu 4 unapojitambulisha.

1. Ukimaliza kutaja Majina yako na Elimu yako, anza kwa kumweleza Mwajiri Ujuzi na Sifa ulizonazo ambazo zinaendana na Majukumu ya nafasi uliyoomba

2. Eleza uzoefu wako wa Kazi au ujuzi ulioupata kwenye Kazi ulizowahi kufanya hapo awali zikilingana Kimajukumu na nafasi unayofanyia Usaili

3. Zungumza kuhusu Mafanikio mahususi uliyoyapata kwenye Kazi au Maisha Binafsi

4. Malizia kwa kueleza wewe ni Mtu wa aina gani na kitu gani ambacho utakifanya endapo utapewa nafasi ya Ajira kwenye Taasisi hiyo.
 
Wasomi poleni sana maana mnateseka sana wallahi …

imegine unavoenda kwenye interview unavokua mdogo kama pirton na mpole kama shilingi mia 😞

huwezi amini kama ni wewe umesugua miaka mingi darasani kabisa unavokua mpole
 
Back
Top Bottom