JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 630
- 957
- Uzalishaji duni: Uzalishaji wa miwa, malighafi ya sukari, unaweza kuathiriwa na mambo kama hali mbaya ya hewa, magonjwa, au mbinu duni za kilimo. Hii inaweza kusababisha upungufu wa sukari katika soko la ndani.
- Usafirishaji na ugavi: Matatizo katika usafirishaji na ugavi wa sukari kutoka viwandani kwenda kwenye masoko yanaweza kusababisha uhaba. Miundombinu duni ya usafirishaji inaweza kusababisha usambazaji usio wa kutosha wa bidhaa.
- Upungufu wa fedha za kigeni: Kutokana na uhaba wa fedha za kigeni, nchi inaweza kukabiliwa na ugumu katika kuagiza sukari kutoka nje, ambayo inaweza kusababisha upungufu katika soko la ndani.
- Udhibiti wa bei: Udhibiti wa bei na sera za kifedha zinaweza kusababisha wazalishaji kushindwa kutosheleza mahitaji ya soko au kusababisha upungufu wa bidhaa.
Nini kifanyike kukabiliana na tatizo hilo Tanzania?
Kwanza kabisa, serikali inaweza kuchukua hatua za haraka ili kupunguza uhaba wa sukari na kupunguza athari zake kwa wananchi. Hapa kuna baadhi ya hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa:
- Kuongeza uzalishaji wa sukari: Serikali inaweza kuchukua hatua za kuhamasisha wakulima wa miwa kuongeza uzalishaji, kuboresha mbinu za kilimo, na kuhakikisha kuwa viwanda vya sukari vinafanya kazi kwa ufanisi ili kutosheleza mahitaji ya soko.
- Kuagiza sukari: Serikali inaweza kuagiza sukari kutoka nje ili kukidhi mahitaji ya soko wakati ambapo uzalishaji wa ndani hautoshi. Hata hivyo, hatua hii inaweza kuwa ni suluhisho la muda mfupi na inaweza kuathiri sekta ya kilimo ya ndani.
- Kudhibiti bei: Serikali inaweza kuchukua hatua za kudhibiti bei ili kuzuia kupanda kwa bei kwa viwango visivyokuwa vya kawaida. Hii inaweza kujumuisha kudhibiti bei ya rejareja na kuhakikisha kuwa wafanyabiashara hawatumii hali hii kama fursa ya kuongeza faida kubwa.
- Kuhimiza ushindani: Serikali inaweza kuchukua hatua za kuhimiza ushindani kati ya wazalishaji na wafanyabiashara ili kuhakikisha kuwa kuna chaguo zaidi kwa wananchi na hivyo kudhibiti bei.
- Kuongeza uelewa wa umma: Serikali inaweza kufanya kampeni za elimu kuhusu matumizi sahihi ya sukari na njia mbadala za lishe ili kupunguza matumizi ya sukari na kuhimiza lishe bora.
Kushiriki Mjadala bonyeza Link hii https://jamii.app/UhabaWaSukari
UPDATES
- PROFESA KENNETH BENGESI, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari TanzaniaMsimu uliopita hali ya uzalishaji wa Sukari ilifikia rekodi ya juu kabisa 460,000 Nchini, wakati huo mahitaji yalikuwa 490,000 kulikuwa na upungufu wa Tan 30,000
Mwaka huu (2024) uzalishaji mpaka sasa ni 370,000, kwa namna yoyote hatuwezi kufikia lengo tulilojiwekea la kufikisha Tani 550,000 kutokana na Mazingira ya Mvua
Ndani ya kipindi cha Miaka 10 tumefika katika kiwango cha juu cha uzalishaji wa Sukari, tulikotoka Mwaka 2001 tulikuwa tunazalisha Sukari chini ya Tani 200,000
Mwaka huu (2024) kuna pengo kubwa na hivyo upungufu utakuwa mkubwa kuliko ulivyokuwa Mwaka 2023
- DAVID MULOKOZI, Mkurugenzi Mtendaji wa Mati Super Brands LTD - Manyara
Sisi tunahusika na utengenezaji wa vinywaji vikali na vinywaji vingine ambavyo utengenezwaji wake unahusisha Sukari
Hali ya Sukari sio nzuri Nchini, hii haikuanza siku moja, sukari ilianza kupotea taratibu hali ambayo ilisababisha sisi tuliopo Mikoani tukaanza kwenda maeneo mengine kuitafuta, hiyo ikasababisha mazingira ya kupandisha bei ya bidhaa kutokana na changamoto ya uzalishaji
Ndani ya Mwezi mmoja kuna viwanda kadhaa vya utengenezaji wa vinywaji vikali vimefungwa kutokana na uhaba wa Sukari, ukichanganya na uhaba wa Dola kumekuwa na ugumu wa kuendelezea uzalishaji
Uhaba wa Sukari umesababisha kuwe na changamoto katika uzalishaji wa mambo mengi
- PROF. KENNETH BENGESI, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania
Mvua kubwa zimesababisha uvunaji wa miwa kuwa mgumu, miundombinu ikaharibika ikawa ngumu kuendeleza uzalishaji, sio kwamba hatuna miwa, changamoto ni hizo nilizozitaja
Pia, uagizaji wa Sukari siyo jambo la wiki moja, inaweza kuchukua hadi miezi miwili hadi mitatu, mfano Sukari inaweza kutolewa India, Brazil au Thailand ambapo nako kuna mabadiliko ya utoaji Sukari kutoka kwenye Nchi zao
Baada ya UVIKO-19 bei ya Sukari ilipanda zaidi ya mara tatu kote Duniani kutokana na mabadiliko ya Soko la Sukari yaliyotokea katika Nchi nyingi
- BERNARD KIHIYO, Mkurugenzi wa Chama cha Walaji Tanzania
Kumekuwa na ahadi nyingi nzuri kuhusu Sukari, tukiambiwa hili litaisha au itakuwa hivi lakini baada ya muda jambo halimaliziki
Sisi tuna Mtandao wa Walaji Mikoa yote, tunapata ripoti kuhusu uhaba wa Sukari pamoja na bei kuwa juu, sio jambo jema
- PROFESA KENNETH BENGESI, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania
Sababu kubwa iliyosababisha bei ya Sukari kupanda sio Tozo, ni upungufu au uhaba wa SukariHiyo ikasababisha Wafanyabiashara ambao sio Waaminifu kuanza kupandisha bei
Sukari inayozalishwa ndani haina Tozo, Tozo ni kwa ajili ya Sukari inayoagizwa kutoka nje. Mfano Serikali imefuta Ushuru wa Forodha lakini bado bei zikawa zinapandishwa, hapo ni suala la uadilifu
Tulivyokuwa kwenye UVIKO-19, Nchi ambazo ni wauzaji wakubwa wa Sukari walikuwa kwenye ‘lock down’, hiyo ilisababisha upatikanaji wa Sukari kwenye Soko la Dunia ukashuka, sasa hivi ndio tumeanza kupata nafuu
- AHOBOKILE MWAITENDA, Mshauri wa Fedha na Kodi
Unaweza kukuta mzalishaji mmoja wa Sukari anatengeneza Sukari Mkoani Kagera, baada ya kuzalishwa inapelekwa kwenye kituo nje ya mkoa huo kwa ajili ya kuanza kusambazwa kisha ndio inarejeshwa kwenye kituo husika kama sehemu ya usambazaji
Hiyo ni moja ya changamoto inayoweza kusababisha kukosekana kwa usambazaji mzuri wa Sukari
- PROF. KENNETH BENGESI, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania
Miaka mitatu ya nyuma, Fedha ya Zambia haikuwa na mlinganisho mzuri na Fedha yetu, kwa sasa hilo tatizo halipo
Sukari inayoingia kutoka nje lazima iwe na vibali vyote muhimu, ikitokea imeingia bila kufuata utaratibu ndipo utaona inaanza kuuzwa kwa bei ya chini, ndivyo ilivyokuwa ikitokea Sukari iliyoingia kinyume cha Sheria kutoka Zambia
- DAVID MULOKOZI, Mkurugenzi Mtendaji wa Mati Super Brands LTD ya Manyara
Sukari ya nyumbani ikiwekwa sokoni hiyo hiyo ndiyo inunuliwe na makampuni yanayohusika na uzalishaji wa bidhaa kwa kutumia sukari ni rahisi kusababisha changamoto ya uhaba kwa kuwa Viwanda vinatumia Sukari nyingi zaidi
- PROF. KENNETH BENGESI, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania
Hakuna upungufu wa Sukari kwa ajili ya matumizi ya ViwandaNitoe wito kuwa Wazalishaji wa viwanda ambao wanatumia Sukari katika uzalishaji wao waje Bodi ya Sukari tuzungumze tutawezesha wapate Sukari badala ya kutegemea ile inayozalishwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani
- SEIF MAALIM SELASSIE, Mgombea Urais 2020 kupitia AAFP
Ingetokea nimechaguliwa na kushinda Urais wakati nagombea wala tusingekuwa na mjadala huu wa Sukari kwa sasa, kwani ningekuwa nimeshughulikia changamoto hiyo mapema
- PROFESA KENNETH BENGESI, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania
Wanaokamatwa kwa kuuza Sukari kwa gharama ya juu ambayo si bei elekezi, sio Wafanyabiashara wadogo tu hata wakubwa. Tunachoangalia ni kwa mfano wanaouza Sukari Kilo moja Tsh. 6000. Kama kuna wanaoendeleza kuuza kwa bei kubwa Mwananchi atoe ushirikiano kwa Bodi tutawawajibisha wanaofanya hivyo
Kuna watu wasipopata Sukari kipato kinakuwa hakina uhakika, ndio maana Serikali ilifuta Tozo mbili ya Kodi ya Ongezeko la Thamani VAT na ile ya Ushuru wa Forodha Isingekuwa hivyo Wananchi wa kipato cha chini wangeweza kuuziwa Sukari hata Tsh. 10,000, tulipoona bei hazishuki ndipo tukaweka bei elekezi