Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mimi hujiuliza mtu haoni haya kumwambia mtu amchangie harusi yake? Kwani hili ni jambo la muhali mkubwa sana.

Unawezaje kuomba kwa kitu cha anasa? Kwa nini huridhiki na uwezo wako?

Kuna mawili,

Ama ufanye harusi utakayoalika watu wachache lakini kwa kiwango cha "ufahari" wa kukutosha kwa hizo pesa ulizonazo [Kama wanavyofanya Wazungu]. Harusi nzima mnaalika watu wasiozidi 40 katika kubana matumizi.

Ama ufanye harusi utakayoalika watu wengi lakini ukashusha viwango vya "ufahari" ili kukidhi hizo pesa ulonazo
[Kama harusi za Kiswahili za zamani]. Wageni unawapa sadaka ya chakula kidogo, mnapiga cherekochereko kazi imeisha

Hii ya kutaka kujifakharisha kwa pesa za mwengine, sivyo, ni kujidhalilisha tu
 
Mi nina harusi ya mwana natakiwa nitoe lak 5 nimeduwaaa, but as long ni mwana from primary, kitaa, chuo na hata kwenye career tunagumiana. Daily mjini lazima nijisachi tu japokuwa roho inauma maana budget ipo deficit

unaona sasa,unazidisha umasiki tu hapo.
 
Kwakweli michango imezidi jamani, mimi siku hizi kwakweli naipotezea sana hiyo michango ya harusi
 
Hutakiwi kusubiri watanzania wengi waliache. Wewe fanya yako vile unavyotaka, watanzania wengine waache wafanye watakavyo. Uhuru wa mawazo huanzia ngazi ya familia, kama hata harusi yako mwenyewe hupati uhuru wa kuipanga usitegemee uhuru wa kuamua kuhusu mambo makubwa zaidi ya jamii.

Ze markopolo & Kiranga hapa tunakuja katika swala la malezi...!

kuna watu wamelelewa kuheshimu maamuzi ya wazazi... mfano nakupa "arranged marriage"

inawezekana labda katika malzei uliyolelewa wewe wazazi walikufundisha kuwa na ile independent thinking lakini si jamii yote ya kitanzania wamelelewa malezi ya aina hiyo..! wakuu mi nazunguzia reality nini kitachotokea huko mtaani!.. kubali tukatae as long as wazazi wapo hai swala la ndoa linakuwa halipo kwenye control yako tena! .. family & wazazi wana take over!
 
Njiwa,
unachosema ni kweli kwa kiasi fulani, lakini wazazi hawawezi kukushikia kiboko ukaombe michango. Tunachokataa siyo wazazi kuhusika ila tabia iliyozagaa ya watu kupanga bajeti kubwa kuliko uwezo wao halafu wanafanya kama ni jukumu la jamii kukamilihsa bajeti hiyo kupitia michango. Whether chanzo kiwe wazazi au marafiki lakini yule anayetembeza bakuli la michango anabeba jukumu la lawama ya usumbufu huo anaousababisha kwa jamii.
 
nadhani sasa m2 akitaka kuoa au kuolewa,wajipange sio kuchangisha watu cz ts becaming too much.ela yote yaishia kwenye michango mpk unashindwa kufanya maendeleo yako... au wadau mnasemaje?

Ndugu yangu, bado unachangia harusi wewe? Mimi nikipata kidogo napeleka kwa watoto yatima walau visiku vyangu viendelee kusogea. Harusi zenyewe hawakai hata miezi sita wameshaachana.

Nimeokoka kuchangia harusi.
 
Eti umchangie mtu aoe! Na wakiachana waombe mchango pia! Mi sichangi siku hizi. Kwanza mi sikuwahi kuchangiwa I had less than 20 people at my receiption!
 
kwa maksudi kabisa nimeelekeza mada yangu kwa viongozi wa madhehebu ya kikristo kwa sababu huko ndiko kulikoshamiri harusi za kifahari lakini zinazotokana na michango ya harusi kutoka kwa ndugu na marafiki. Tumefika pabaya. Kwa mtu anayepata mshahara wa laki tatu kwa mwezi ambao ndiyo mshahara wa vijana wengi wanapaswa kuchangia ili nao waje wachangiwe mara nyingi hujikuta wakitumia mshahara wote katika michango ya harusi. Ni vigumu kwa serikali kutunga sheria kuzuia michango ya harusi. Lakini viongozi wa kidini wana uwezo wa kutoa mwelekeo. Mtu anayetaka harusi ya kifahari na ana uwezo wa kuigharamia bila ya kuomba michango na aendelee. Nawasilisha.
 
Mimi nadhani serikali ianze kutoza kodi kwenye michango ya harusi.
 
Kwani kanisa ndo limeweka viwango vya gharama za harusi?Na ukifuatilia vizuri utakuta viongozi wa kanisa wanahitaji watu wanne tu ili waweze fungisha ndoa, I mean Bw/Bi harusi na wadhamini kwisha.Bila kujali hata mavazi uliyovaa yana thamani gani.

Kwa upande wangu mimi sijaona shida ya michango ya harusi kwani ni michango ya hiari, huna pesa unakaa pembeni wenye nazo watachangia ila kumbuka WHAT GOES AROUND COMES AROUND siku yako ikifika kama hukuwa mtu wakutoa kwa wenzako utaipenda unless uwe fisadi utaweza fanya bila michango.

Mfano, nakumbuka harusi yangu ili-cost kama 9m, cash niliyotoa mimi ilikuwa kama 1.5m yaani gharama zote hapo mpaka nikakabidhiwa wife kanisani,Sasa kweli unaweza niambia michango ni mibaya nikakuelewa kweli?

Na huwa natoa nikiwa nayo na kama sina huwa nakuwa muazi na nina eleweka tu.

Na kwa yeyote mwenye kadi ya mchango wa harusi just ni-PM takurushia kwenye MPESA.

KUTOA NI MOYO SI UFISADI.
 
Ni kawaida kwa jamii yoyote duniani kuoa ama kuolewa na hasa kwa binadamu aliyekamilika. Kimsingi kuoa ni jambo la heri kwa mtu kupata mwenzi. Na ndugu jamaa na marafiki kuchangia kwa mawazo mali na misaada mingine ya kijamii ili kufanikisha shughuli hiyo kukamilika.

Hata hivyo uchangiaji huu umekuwa wa kiholela mno, kwani waoaji na wanaoolewa ni vyema wakawa na utaratibu mzuri wa kugawa kadi hizo. Nasema hivi kwa sababu kuwa mgawa kadi anapaswa kufanya mawasiliano na mtu anayetaka ampe kadi kwa ajili ya kumchangia mchango huo. badala ya kuzigawa kadi hizo pasipo hiari ya mchangiaji, maana mgaw kadi unashangaa anakuletea kadi, ama anaibwaga mezani kwako kama ni ofisin au anawaachia watoto kama ni nyumbani.

Ombi langu kwa waoaji wote fanyeni mawasiliano kabla ya kugawa kadi maana sasa zimekuwa kero kiasi kwamba ndani ya mwezi mmoja unaweza kugawiwa kadi zisizopungua kumi na wote wantaka mchango usiopungua elfu hamsini. kwa namna hii hatuwezi kwenda kabisa.

Hata hivyo niwaombe watanzaia wenzangu tunahitaji kubadilika ili mitizamo yetu isilenge zaidi katika uchangiaji wa harusi, tunahitaji kuchangia zaidi katika elimu kwani kuna vijana wetu hawana hata dwati la kukalia, yatima, wajane na wenine wengi wenye mahitaji badala ya kuchangia harusi.

Kufanya harusi kubwa katika kumbi kubwa zenye kugharimu mamilion ya shilingi za kazi gani, kwani hazina tija kwa maendeleo ya taifa hili ambalo wananchi wake wako katiak wimbi la umaskini mkubwa.
 
nilishaacha siku nyingiiiiiiiii kuchanga, tena wasivyo na adabu wameweka na viwango!! ndio kabisaaaaaaaa, yangu yakinikuta nitajua mbeleni! ila kwa sasa hell no! imekuwa ni business, unajikuta u spend a lot kwenye hii makitu!
 
Hoja yako nimeependa sana.

Kweli kuna watu wanatoa taarifa ndani ya muda mfupi. Mfano Mwezi mmoja au miwili. Hapo usipomchangia anakuja leta lawama kibao.

Pia kuna wengine wanapanga kufunga ndoa miezi ya Dec, Jan, na february. Kwa kweli miezi hii haijakaaa vizuri kwa michango ya harusi.

Mwezi Dec. ni maandalizi ya sikukuu ya X-mass pamoja na ada za watoto shuleni.

Mwezi January pale bado tunachakalika na ada.

February tunalipa madeni tulikokopa ili kulipa ada za watoto.

Hivyo mimi binafsi miezi hii mtu akiniletea adi au kunialika kikao cha harusi itakayofanyika miezi hii, najua huyu ananitafuta ubaya tu.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Ni bora sana umeliona hilo mku. Kinsingi michango ya harusi imefikia pahala inaboa ile mbaya na inarudisha nyuma maendeleo sana. Mwenzie ninazo saba hivi sasa na wote wanafunga ndoa kati ya January5 na Februari 23. Binafsi naona shida yetu watanzania ni kupenda kujipandisha hata pale tunapokuwa hatuna kitu. Utakuta mtu ni maskini lakini anataka harusi ya kifahari. Matokeo yake anamwaga kadi akidhani watu wanapenda sana kuchangia starehe zawengine kumbe angeweza kufanya kisherehe kinachoendana na uwezo wake na bado akawa ameoa vile vile. Mwenzenu nimeamua kuwa sitachanga tena miharusi na hata mimi sitaomba mchango wa mtu yeyote kwa ajili ya haruasi. Nitakuja kuomba nikiumwa na nitakapohitaji na mimi niende India nikatibiwe ila kwa hili la harusi wanajamvi mtanisamehe kwani sitawaomba michango. Nimeona ni ushenzi sana.

Ni kawaida kwa jamii yoyote duniani kuoa ama kuolewa na hasa kwa binadamu aliyekamilika. Kimsingi kuoa ni jambo la heri kwa mtu kupata mwenzi. Na ndugu jamaa na marafiki kuchangia kwa mawazo mali na misaada mingine ya kijamii ili kufanikisha shughuli hiyo kukamilika.

Hata hivyo uchangiaji huu umekuwa wa kiholela mno, kwani waoaji na wanaoolewa ni vyema wakawa na utaratibu mzuri wa kugawa kadi hizo. Nasema hivi kwa sababu kuwa mgawa kadi anapaswa kufanya mawasiliano na mtu anayetaka ampe kadi kwa ajili ya kumchangia mchango huo. badala ya kuzigawa kadi hizo pasipo hiari ya mchangiaji, maana mgaw kadi unashangaa anakuletea kadi, ama anaibwaga mezani kwako kama ni ofisin au anawaachia watoto kama ni nyumbani.

Ombi langu kwa waoaji wote fanyeni mawasiliano kabla ya kugawa kadi maana sasa zimekuwa kero kiasi kwamba ndani ya mwezi mmoja unaweza kugawiwa kadi zisizopungua kumi na wote wantaka mchango usiopungua elfu hamsini. kwa namna hii hatuwezi kwenda kabisa.

Hata hivyo niwaombe watanzaia wenzangu tunahitaji kubadilika ili mitizamo yetu isilenge zaidi katika uchangiaji wa harusi, tunahitaji kuchangia zaidi katika elimu kwani kuna vijana wetu hawana hata dwati la kukalia, yatima, wajane na wenine wengi wenye mahitaji badala ya kuchangia harusi.

Kufanya harusi kubwa katika kumbi kubwa zenye kugharimu mamilion ya shilingi za kazi gani, kwani hazina tija kwa maendeleo ya taifa hili ambalo wananchi wake wako katiak wimbi la umaskini mkubwa.
 
Sijawahi kuwa na utaratibu wa kuchangia harusi, ukiwa na shida nyingine your mostly welcome, wabongo wanapenda sana sifa za kijinga, unajua huna uwezo fanya kile chenye uwezo wako, usipomchangia ndo ujue umeshakuwa adui yake na kukununia juu.
 
mimi mwenyewe huwa nachangia kwa hiari nikichangishwa sichangii na siku ya harusi yangu sichangishi anaetaka atachangia kwa hiari.
 
Back
Top Bottom