Michango ya send off na harusi chanzo kikuu ndoa nyingi kuvunjika

Loading failed

JF-Expert Member
Sep 14, 2023
1,945
5,849
Wasaalam sana ndugu zangu

Wakubwa ni nani aliyetuloga , ni nani aliyetufanya kukosa akili na kutambua jambo hili baya tulilolifanya ndiyo utaratibu wa kuwa send off na kuwasindikiza kwenye ndoa wapendwa wetu

Ndugu zangu ndoa nyingi sana zina vunjika, ndoa nyingi sana zina migogoro, furaha hakuna , ni chuki na kufanyiana visa , ni wizi mtupu na masikitiko makubwa sana tunayo ya shuhudia kila kukicha , ndugu zangu vijana hawataki kuoa kwa kuona yaliyomo huko baada ya kuchungulia kwenye ndoa za watu, hofu na imetamalaki mioyoni mwao

Ndugu hii dhana ya kuchangishana mahela ya kufanya sherehe za send off pamoja na sherehe za harusi imekua ni ya mkosi sana kwenye ndoa za kila siku kwani michango hoyo ina sumu mbaya sana kutoka kwa wachangishwaji waliotoa fedha zao kwa masikitiko na kwa uchungu ili wasionekane hawashiriki kwa wenzao

Ndugu tunafahamu kabisa michango hii imekua ikitolewa kwa manung'uniko, mtu anaacha kula , ana acha mtunza mkewe au mume wake ili achangie sherehe za watu asionekane mbinafsi kumbe moyoni mwake anaumia sana , ni uchungu na wala siyo furaha, je unategemea huu mchango utaleta baraka kwako wewe muoaji na muolewaji au laana kwenye ndoa yenu?

Ndugu michango ya harusi imekua na mikosi mingi katika safari za ndoa za tuwapendao, kwa sababu michango hii inatoka pasi na makubaliano ya watoaji, unakuta mtu anataka mchango mume/ mke, rafiki/ndugu , mpenzi kike /kiume mmoja wao hataki ila mwingine anaforce hela zikachangiwe huu ni mgogoro mwingine huko ziendapo hakutakua na masikilizano wala amani ni migogoro daima na msitegemee mtakubaliana huko

Michango hii imebeba roho za wizi, fitina , chuki na visasi maana wakati mwingine mtu anaiba ili aweze kwenda kutoa mchango , mbaya zaidi mwingine anajiibia ili tuu aonekane ametoa kumbe moyoni mwake anaumia sana ni huzuni kwa kweli

Hakuna mtu anayetoa mchango hata siku moja akafurahia wengi wana masikitiko na hawataki ni vile wanakua wasiri hawataki kusema ili wasionekane wabaya na wapendwa wao ila ukweli unabaki kua kama ulivyo. Yote haya yanabebwa na hayo mahela na yanakuja huko kwenye ndoa yenu na msitegemee mkaishi kwa amani hilo msahau kabisa

Wakuu maisha ya sasa kama unataka salama yako kwenye ndoa yako jigharamie mwenyewe sawa sawa na uwezo wako binafsi wa kiuchumi usitake kutesa watu na michango yako ya send off au harusi ukajakushangaa ndoa yako imevunjika pasi na kujua hiyo michango ndiyo chanzo kikuu cha wewe kufatwa na mikosi mingi huko ndoani

Kumbukeni sadaka / hela ya mtu ilipo ndipo na moyo wake ulipo, ametoa kwa moyo wa uchungu , masikitiko, unafiki, ugomvi, husuda, chuki, na kwa uongo huko huko hela imesafiri na haya matatizo kwenda kwenye ndoa zao na lazima ndoa ziyumbe na kuvunjika vipande vipande tuu

Nb: MCHANGO WA SEND OFF NA HARUSI NI MBEGU KWA WANA NDOA ,JE MCHANGO ULIOPEWA ULIPEWA KWA NAMNA GANI NA KWA MOYO UPI

Je, kilicho tolewa walitoa kwa moyo au ni kwa lazima na kwa hesabu yenu mliyo ipanga nyie ili mjivunie mikosi zaidi huko kwenye ndoa?
 
Michango haiumi kwa watu wako wenye ukaribu na wewe kwa maana kuna wale watu mpo pamoja katika shida na raha.

Na unajikuta unatoa tu kwa moyo bila hata kukumbushwa. Lkn kuna ile mtu hamna ukaribu labda mmekutana tu kwenye kikap cha kazi, tena mara moja au sehemu yoyote basi anakudaka anaanza kukuganda aiseeee basi tu.
 
Mtu ambae sio rafiki yangu na sio wa karibu yangu, au rafiki au mtu wa karibu analeta kadi ya mchango wa sijui binamu Gani, sijui kibwengo gani huo upuuzi ni ujinga mtupu.
 
Back
Top Bottom