Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Malogi76 wewe harusi yako ulichangiwa?

Okay,nimekifunza kitu,ukishapita hiyo hatua huoni sababu ya kuchanga kwakuwa unaye mwenza!

Basi waache vijana wachangishane
 
Malogi76 wewe harusi yako ulichangiwa?

Okay,nimekifunza kitu,ukishapita hiyo hatua huoni sababu ya kuchanga kwakuwa unaye mwenza!

Basi waache vijana wachangishane
Jaji hujanielewa sijui...mimi niliomba kwa wazazi sitaki harusi kubwa na waliokuja wanawajuwa wao hao watu ambao sijawahi waona ...mimi kuchanga ni ndugu tena wa karibu.kama sikujui...sijawahi kukusikia hamna sababu ya mimi kuchanga sababu sitokuja.hii ni kwa upande wangu mimi
 
Aamin, Aamin, Aamin. Niseme kweli, kama ilivyo kwako; kwangu pia nuru mpya imeng'ara katika maisha yangu kwa hayo uliyoeleza hapa nimepata nguvu mpya na afya mpya kiroho.

Mimi huwa nawashangaa sana watu wakikaa vijiweni na kusema "binadamu wabaya" mara utasikia "ooh Dunia hii hakuna wa kukusaidia zaidi ya ndugu yako" n.k n.k mimi huwa nawasikiliza tu na kusema; Hakika atakayekufaa kesho humjui kwasababu mimi mwenyewe nimewasapoti watu ambao siwajui na hata nikionana nao kesho hawatanikumbuka wala sitawakumbuka.

Kitu kikubwa pia nilichojifunza maishani mwangu ni kuwa tenda wema na usisubiri shukurani. Malipo ya wema wa aina hii hulipwa na Mwenyezi MUNGU mwenyewe kwako mwenyewe au hata kwa kizazi chako. Maajabu ya wema ulioufanya utaanza kuyaona ukiwa na shida, utashangaa watu wa kukusaidia wanajitokeza tu bila hata kujua wametokea wapi tena huwajui na cha ajabu zaidi hawahitaji malipo kutoka kwako!!! Kanuni ya wema ni ya ajabu sana sana sana.

Kubwa zaidi tukumbuke kuwa tunavotenda wema ni tunatimiza kusudi la Mwenyezi MUNGU. Tujifunze kuwa unapotenda wema huwenda ukawa umefanya muujiza mkubwa sana kwa yule uliyemtendea bila hata wewe kujua. Kwa wema wako huenda yule uliyemtendea akakesha usiku kucha akimshukuru Mwenyezi MUNGU kuwa amemjibu maombi yake!!! Sote Hatujui lakini huwenda mtu uliyemsaidia aliomba Mwenyezi MUNGU amsaidie jambo, nawewe ukajitokeza ukafanya lile lile kama alivoomba kwa mwenyezi MUNGU! Tazama jinsi mtu huyu atakavomshukuru Mwenyezi MUNGU kwa kumjibu maombi yake. Kifupi ni kuwa kila mmoja hapa duniani katumwa na Mwenyezi MUNGU aje atimize kazi fulani alizopangiwa lakini wengi wameamua kufuata mambo yao wenyewe yanayowafurahisha wao na nafsi zao bila kujali walichotumwa na Mwenyezi MUNGU ndio maana harusi wanachangia 50,000/= lakini kwa mgonjwa na mwenye shida anatoa 500! Ni vitu vya ajabu sana vinatendeka hapa duniani hadi vinachekesha na kuhuzunisha.
Kwakweli mimi nishajisemea moyoni mwangu kuwa kwenye haya mambo ya kipuuzi ya sherehe zisizo na maana watu wanatumia milioni kumi kwa siku kwa kula na kunywa hawataniona kamwe na nipo tayari kulaumiwa na hata kutengwa maana ninajua kuwa watakaonifaa si hawa ninaowadhania bali Mwenyezi MUNGU ataniletea watu nisiowajua na hata kunizika watanizika. Napenda sana niwapate ndugu wa kiroho kama wewe wawe jirani zangu katika maisha yangu maana hata ktk nyakati za huzuni watanipa faraja ambayo pengine singeipata mahali pengine popote.

Asante tena na tena. Kama ulivyosema wema wa kweli usio wa kinafiki na usiotegemea malipo kamwe haupotei bure na mibaraka yake yaweza kuonekana leo au baada ya vizazi vitatu vijavyo. Unapotenda wema unapanda mbegu ambayo baadaye huko mbele ya safari itakuja kuzaa matunda mema. Yawezekana hata isiwe kwako lakini matunda yake siku moja binadamu mwingine atavuna. Mpaka leo huwa najiuliza yule mzee asingejitokeza pale Bugando sijui leo ningekuwa mtu wa aina gani.

Na watu wengi hudhani kuwa pengine kutenda mema ni lazima kutoa pesa na mizawadi mikubwa mikubwa. Kumbe hata matendo madogo madogo tu yanatosha sana kuamsha wema uliomo mioyoni mwa binadamu wenzetu na hata kuwafanya wajione wana thamani hapa duniani.

Leo nimejifunza mambo mengi mapya ya kuniimarisha zaidi katika ubinadamu wangu. Na pengine nikuhongereshe pia kwa kupata mwenza mwenye mitazamo inayofanana. Kizazi hiki kipya kimeshadadia mambo artificial na shallow sana kuhusu maisha yaani wakati mwingine mtu mpaka unaogopa. Ni kazi ngumu mno kusaka mwenza wa kudumu kwa vijana wa kisasa mpaka mtu waweza kukata tamaa.

Namshukuru aliyenifanya niingie katika thread hii na kukutana na mtu muhimu kama wewe. Hebu Mungu na Akaendelee kututumia kama vyombo (japo dhaifu tu) ambavyo kupitia kwavyo wema wake unajidhihirisha kwa waja wake hasa hawa masikini kabisa wasio na matumaini. Ubarikiwe sana wewe pamoja na wapendwa wako. Amen!
 
Habari ya leo wadau,

Hivi hii issue ya kuchangishana hela ili watu wafanye sherehe kuuuuuubwa ya harusi itaisha lini? Jamani zama zimebadilika hivyo yatupasa hata na sisi tubadilike pia, hali sasa hivi ni ngumu jamani si utani, mbaya zaidi unapangiwa kabisa kuwa kima cha chini ni kiasi flani cha fedha, tunatafutana ubaya ujue, ifike mahali furaha yako isiwaumize wengine.

Kama issue ni kufunga ndoa wewe nenda kwa Mchungaji/Paroko mueleza azma yako ya kufunga ndoa hivyo andaa fungu lako kodisha mapaparazi/wapiga picha tafuta sehemu tulivu ambayo mtaenjoy na baadhi ya mashuhuda, maliza mchongo bila kuwapa watu stress, kwa kufanya hivyo utakuwa umeepusha ndoa yako na manung'uniko ya watu, maana kama mjuavyo binaadam hawariziki utasikia mara oooh! pamoja na kuchangishwa fedha nyingi sherehe yenyewe ilikuwa na mapungufu kibao.

Hapa sasahivi tayari nina kadi za mchango 8 mpaka wengine hata siwafahamu, sasa najiuliza nitamchangia yupi nitamuacha yupi.

Nawasilisha.
Kuchangia harusi hulaziishwi. Kuna watu wanapenda kuchangia harusi na usipowachangisha hawaji kwenye harusi yako. Hapo vipi?
 
Kuchangia harusi hulaziishwi. Kuna watu wanapenda kuchangia harusi na usipowachangisha hawaji kwenye harusi yako. Hapo vipi?
Kwani ili uwe umefunga harusi lazima wao wawepo??? What if wamechangia halafu siku moja kabla ya harusi akafa je harusi yako haitafungwa kwasababu yy hayupo? Ishi unavoona inafaa, usiishi vile watu wanaona inafaa.
 
Mi kwasasa wanosahau kabisaaaaaa. Nachangia ndugu yangu, na mtu ninaefanya nae kazi Idara yangu tu. Aidha, harusi yenye pombe sichangii kabisa, siwezi kuchangia pesa yangu watu wakanywe pombe, ila kama mtu ni wa karibu sana na mimi nitampa zawadi baada ya harusi ambayo ni equivalent to mchango ambao ningeutoa.
Vilevile nawahusia vijana, msipende kuchangiwa harusi, kumbukeni kuwa hayo ni madeni!!! Zitakavoanza kujia kadi mfululizo usilalamike kama na ww ulichangisha watu

Kwa kusisitiza ni kuwa, mimi pia watoto wangu nitawafanyia sherehe kwa kuangalia uwezo wangu, sio kusumbua watu michango isiyo na tija. Nitawakaribisha ndugu na rafiki wa familia yangu, sio kuita watu weengi hata ambao hawana hata uhusiano na familia. Ni upuuzi usio na maana.
Sahihi kabisa ni bora ufanye harusi uliyo na uwezo nayo,kuliko kutegemea michango
 
TAREHE 29 KESHO KUTWA KUNA HARUSI MBILI ZA JAMAA NAWAFAHAMU YANI SHOOL MATE WA O LEVEL NA CHUO....TATIZO BUDGET YANGU TU ISHANSHINDA ANI NAISHIWA HATA MWEZI HAUJAISHA...NIMEAMUA KU MUTE TU SINA CHA KUTOA MAANA NINA MIZIGO MINGI AMBAYO MATUMUIZI YAKE YAPO TAYARI, NAHITAJI KULA VIZURI ILI NIZALISHE PIA YANI NI SHIDA......SIO LAZIMA KUCHANGIA PIA MUOAJI AJIPANGE....MI NTAJITAHIDI NISISUMBUE WATUIU SANA...JAPO NATOAGA CHOCHTE KI;LICHOPO 10,000 AU 20,000 ILIMRADI KUCHANGIA
 
Duuh!Mimi sichangii ataa cent moja na kadi zikiletwa nampa mwanangu andikie madudu yakee.nachangia misiba tuh.sijawai kuomba mchango wa mtuuh.
 
Kwani ili uwe umefunga harusi lazima wao wawepo??? What if wamechangia halafu siku moja kabla ya harusi akafa je harusi yako haitafungwa kwasababu yy hayupo? Ishi unavoona inafaa, usiishi vile watu wanaona inafaa.
Hatuishi ndani ya box tunaishi na jamii. Mchango kama watu wanajitolea kuna ubaya gani? Wapo watu wakiambiwa wachange wanakataa hamna kosa ni ombi, kuna wengine wanapenda kuchangia tu utakataa uwaambie sitaki michango yenu?
 
umaskini mbaya sana maisha mtu magumu.. hana kipato cha uhakika anasingizia harusi...

acha wenye uwezo wachangie wewe kama huna uchune...
 
bado hizo mambo zinawaendesha?? can't you have your own stand econimically! changia issue za muhimu na sio misherehe ya watu siju alipokuwa jirani wa binadam wa mdogo wa rafiki wa mpangaji mwenzako ukiwa chuo ambaye ni mke mdogo wa mkewe wakufijia
 
bado hizo mambo zinawaendesha?? can't you have your own stand econimically! changia issue za muhimu na sio misherehe ya watu siju alipokuwa jirani wa binadam wa mdogo wa rafiki wa mpangaji mwenzako ukiwa chuo ambaye ni mke mdogo wa mkewe wakufijia
Thank you.....@Madam Mwajuma umefunguka
 
Thank you.....@Madam Mwajuma umefunguka

eeehhh watu wanalazimishaga utafikir wanajua unazalisha kiqsi gani changia kwa hesabu nawe ukifanya yako fanya inayoendana na uwezo wako nikujikomoa tu unaishi nyumba yakupanga unafanya sherehe ya mil 20? foolish baadae eti Magufuli kabana umeshindwa kujenga
 
bado hizo mambo zinawaendesha?? can't you have your own stand econimically! changia issue za muhimu na sio misherehe ya watu siju alipokuwa jirani wa binadam wa mdogo wa rafiki wa mpangaji mwenzako ukiwa chuo ambaye ni mke mdogo wa mkewe wakufijia
Haaaaaa mbavu zangu mimi
 
Kweli kwa hali ya sasaivi kila kukicha mahitaji yanaongezeka na mishahara ipo pale pale,mimi nililetewa card ya harusi mchango laki5 au kuna list ya vitu uchague ukanunue ulete,fridge,cooker,kuweka mapazia,Sofa tena wamekwambia
ukisha chagua watakuelekeza wapi ukanunue,na hao watu hata wenyewe hawapikii gas wanapika na mkaa
nikasema wanatukomoa kila aliepewa card ya mchango wa hiyo harusi walisema mie ntakua nje ya nchi,wengine
sijui watakua makazini,nikasema ivi mtu unampa kiwango cha mchango atoe kwani ni harusi yake?

Hahaha hiyo nayo Kali
Ngoja mi nijipange nigharamie mwenyewe maana inaleta shida kweli hii
 
eeehhh watu wanalazimishaga utafikir wanajua unazalisha kiqsi gani changia kwa hesabu nawe ukifanya yako fanya inayoendana na uwezo wako nikujikomoa tu unaishi nyumba yakupanga unafanya sherehe ya mil 20? foolish baadae eti Magufuli kabana umeshindwa kujenga
Ningekuwa m/kiti wa kamati hlf michango ikafikia mil 20 nawashauri tu wanakamati tuandae shughuli ya mil 2 hlf fedha iliyobaki mil 18 tunamnunulia bwana harusi kiwanja cha mil 5 na material ya ujenzi akaanze maisha.
 
Back
Top Bottom