Mjadala: Gharama na njia nafuu za kujenga nyumba ya kuishi Tanzania

Kwa tabu ninayoipata kwa kulala humu store...nakupongeza sana mkuu....umefanya kitu cha maana sana kwa uzao wako....sisi wengine hata matumaini ya kufyatua tofari hatuna.......pia mkuu usitake mbwembwe za finishing za gharama gonga mabati kwenye madirisha....weka hata mlango wa mabati hamia kwako...haraka sana...mkuu.....ukiwa kwako ni raha sana.....
 
Unajua dirisha la aluminium complete haipungui kilo 3 una dilisha 11 mlango mzuri mninga 250000 ceiling gypsum kwa nyumba yako hyo makadilio M 3.5 tiles bado Mabomba mziki wake usikie tu bado shimo la Maji taka bado Fundi hajaimba cement name
Gypsum powder kaka hapo bado sana wiring nilisahau

Jaman ndo mana kasema vijana tusiogope yn kujenga ni taratibu sasa vitisho vya nn?hivi unajua mziki wa kupaua wewe?mbao zilivyo bei juu plus bati la maana mhh,mi nampa hongera sn ameniinspire sn kwan hata mimi ni mfanyakazi na mshahara mzuri tu nina kiwanja bt naogopa kuanza ujenz nahis km ntakwama njiani.
 
Milango na madirisha tayari ninayo na ni Mkongo pure. Hayo mambo mengine kidogo kidogo. Ujenzi haufanywi siku moja, cha msingi usiifikirie pesa yako kwenye ujenzi, na usiwaze mpaka upate hela ya kufanya mambo yote kwa pamoja. Unaweka pesa kidogo kidogo. Kwa mfano ukipata 300k unanunua boksi kadhaa za tiles unaweka ndani, haziharibiki. Sisi masikini huwezi kufanya vitu vyote 'at a go'

Hongera sn bro,kweli umeniinspire,Big up
 
Jaman ndo mana kasema vijana tusiogope yn kujenga ni taratibu sasa vitisho vya nn?hivi unajua mziki wa kupaua wewe?mbao zilivyo bei juu plus bati la maana mhh,mi nampa hongera sn ameniinspire sn kwan hata mimi ni mfanyakazi na mshahara mzuri tu nina kiwanja bt naogopa kuanza ujenz nahis km ntakwama njiani.

Mkuu usiogope.......wewe anza......hata ukiishia njiani......utapandwa na mori hutakubali kuangalia nyumba ikiwa kimini.........hakunaga nyumba inayoisha......mdogomdogo utatoboa........
 
Hongera mkuu kwa jitihada hizo sio kwamba nakudis yaani kwa jinsi ulivyojenga hiyo nyumba utahitaji ukimalizia katika UBORA huohuo lakin
Pengine nikuambie tu mpaka unaamia hiyo nyumba itakuwa imekula gharama mara 3 zaidi Ya hiyo gharama iliyopo.
Mfano mdogo kitasa imara cha mlango mmoja tu walau sio chini Ya 60000 sasa kama unamilango 7 ni kama 420000 .
sasa bado gharama ya fundi.na gharama Ya hiyo milango.
Dirisha moja la aluminum pamoja pamoja na gril lake sio chin Ya 300000 kama hiyo nyumba ina dirisha. Kumi ni kama 3000000 bado kupiga draft za ceilin/gypsum
Bado miundo mbinu Ya maji , vigae vya sakafuni ,wiring na mengine .. mengi ..kama rangi yaani hiyo nyumba bado sana mkuu .. huko kuliko baki ndo pakubwa kulingana na UBORA wa hiyo nyumba

Ujue hapo ndio nyumba zinapotofautiana. Kitasa cha 60k ni anasa tuu. Kuna vitasa imara vya kuazia 15k mpaka 25k na viko poa tuu. Finishing inategemea budget ya mtu na nyumba haaiishi kujenga kwaiyo finishing itaendelea hata baada ya kuhamia.
 
Mkuu usiogope.......wewe anza......hata ukiishia njiani......utapandwa na mori hutakubali kuangalia nyumba ikiwa kimini.........hakunaga nyumba inayoisha......mdogomdogo utatoboa........

Mweeee!!! Nimekupenda bure jmn.ana raha yule mumeo aliyekuoa maana watoto watarithi yaliyo makuu kuanzia 'ugrit thinka',hekima,uthubutu hata upambanaji.kwa spirit hii umenikosha aiseee
 
Mkuu usiogope.......wewe anza......hata ukiishia njiani......utapandwa na mori hutakubali kuangalia nyumba ikiwa kimini.........hakunaga nyumba inayoisha......mdogomdogo utatoboa........

Kabisa dadaangu woga ni sumu ya mafanikio.
 
Dogo hilo boma tu nyumba yenyewe hujaanza bado. Rudi hapa kusimulia ukishafanya finishing.
 
Hongera but kufikia hatua hiyo ni rahisi mno hatua inayofuata ndio Ujenzi wenyewe Mziki wa nyumba upo kwenye finishing

Mkuuuu,tupe progress baada ya kuweka madirisha,miundombinu ya maji taka,safi,milango,ceiling boards n.k,huko ndio kwenye balaa,mbona kupandisha boma sio kazi,kazi finishing mkuu,hapo ndo utakapotoa macho utakapoambiwa wiring tu milioni unusu na ndipo utakapoanza kuwachukia mafundi

msimtishe....
katika hiyo hatua na wewe unaitwa baba mwenye nyumba. ulipopanga wakizingua unahamia kwako na dirishani weka mifuko ya sementi, kwani nini!!!
hzo finishingi unapiga ukiwa kwako..
 
Nyie wote mnaomtisha kwamba sasa ujenzi ndio unaanza hamfahamu mziki wa kupaua mnafahamu kwamba paa inapauliwa kwa mara moja tu na sio kidogokidogo?.Sehemu iliyobakia inakula pesa ndio lakini ni rahisi kwa sababu anao uwezo wa kutengeneza chumba kimojakimoja kila baada ya muda fulani kwa kadri atakavyokuwa anapata pesa.Mpango nilionao mimi ni kukarabati vyumba viwili kwanza sebule na chumba cha kulala na choo tu nihamie mengine nitakuwa napiga taratibu.Ila kwa sisi vijana tuliozoea kujirusha club na kuzungusha raundi ili mademu watuone tuna hela kujenga itakuwa vigumu sana na ndio wengi ninaowaona hapa wakiwakatisha tamaa wenzao ujenzi ni mgumu sana kama huna nia na pia ujenzi ni rahisi sana kama umejiwekea malengo.
 
Ni kweli, huwezi kupaua ukakaa mwaka hujaezeka, zoezi la kuezeka ni gumu kwani ni lazima liishe ndani ya muda mfupi. Nashukuru mkuu kwa kuelimisha wengine!
 
Nikusahihishe Mlango wa Mninga Dsm ni zaidi ya Laki 5, na mninga ni inferior kwa Mkongo(I work in that sector, dont argue) Mkongo ni bora zaidi ya Mninga. Na tayari ninayo milango yote 10(Didnt buy in Dar).
Hoja yangu ya msingi ni kuwa 'kidogo kidogo with determination inawezekana' tusikatishane tamaa.

Kwetu kule mbao kibao tu, ya nn kununua hapa dar? Waambie hao
 
My Opinion
Hapa Tanzania kuwa na nyumba ni suala la KIJAMII zaidi. Yaani kuna heshima fulani mtu akiwa na nyumba yake. Watu wengi huifuata hiyo heshima, hata kama hana hitajio la nyumba wakati huo.
Nakupa mfano, kuna mtu amejenga mbezi ya kimara ndani ndani huko akahamia vizuri tu. Kilichotokea ni kwamba analazimika kuamka saa 10 alfajir na hurud saa 4 usiku akawa anawaona watoto wake na kufanya mambo ya kifamilia weekend tu. Kahama kaacha nyumba karudi kupanga karibu na mjini. Sawa unakaa kwako, unajua opportunity cost ya kukaa kwako? Subiri uzeeke utaenda kukaa huko fo the rest of ur life!!!
Unawajua wahindi na waarabu wa pale katikati ya mji wa Dar? Wangapi wanamiliki nyumba? Hawana uwezo wa kujenga wale? Tena wapo nchi hii tangu Nyerere alipotaifisha baadhi ya nyumba zao, kwa hiyo wanaijua vizuri Tanzania. Jitazame, kama huna hitajio la nyumba binafsi kuishi kwa wakati huu, jenga pole pole tu. Usikurupuke eti kisa upate heshima. Hata Mungu hakuumba ulimwengu siku moja, ipo siku utahamia kwako comfortably.
Lipa kodi kwa baba mwenye nyumba, jenga polepole.
MullaX
 
Siku zote huwa namuheshimu sana mtu anaefanya kitu kama hiki......hata kama ni room moja........anastahili pongezi.......heshima kwako sana mkuu.......wenzio hiyo pesa ya kufanya hivyo wanaweka heshima bar.........

Yeah!ni wazo zuri sana.
 
My Opinion
Hapa Tanzania kuwa na nyumba ni suala la KIJAMII zaidi. Yaani kuna heshima fulani mtu akiwa na nyumba yake. Watu wengi huifuata hiyo heshima, hata kama hana hitajio la nyumba wakati huo.
Nakupa mfano, kuna mtu amejenga mbezi ya kimara ndani ndani huko akahamia vizuri tu. Kilichotokea ni kwamba analazimika kuamka saa 10 alfajir na hurud saa 4 usiku akawa anawaona watoto wake na kufanya mambo ya kifamilia weekend tu. Kahama kaacha nyumba karudi kupanga karibu na mjini. Sawa unakaa kwako, unajua opportunity cost ya kukaa kwako? Subiri uzeeke utaenda kukaa huko fo the rest of ur life!!!
Unawajua wahindi na waarabu wa pale katikati ya mji wa Dar? Wangapi wanamiliki nyumba? Hawana uwezo wa kujenga wale? Tena wapo nchi hii tangu Nyerere alipotaifisha baadhi ya nyumba zao, kwa hiyo wanaijua vizuri Tanzania. Jitazame, kama huna hitajio la nyumba binafsi kuishi kwa wakati huu, jenga pole pole tu. Usikurupuke eti kisa upate heshima. Hata Mungu hakuumba ulimwengu siku moja, ipo siku utahamia kwako comfortably.
Lipa kodi kwa baba mwenye nyumba, jenga polepole.
MullaX

Hivi tunajenga kutafuta heshima au kupata makazi ukiwa na familia yako?unaowasema bado wanaweza kuishi nyumba za msajili na wakalipa kodi,tunaojizungumzia hatuwezi hata kwenda NHC office kuulizia kama kuna vyumba,nyumba za watu katikati ya miji pia hatuziwezi na kodi zao,hatutaki pia kuhama hama na watoto kila siku unauluzwa swali na mtoto mpaka unashindwa kumjibu,hv mtoto wako akikuuliza Baba kwa nini tunahamia kwenye nyumba za watu kila siku utamjibuje?utamwambia huna pesa na anakuona kila siku unaenda vibaruani?wala yeye hajui kama pesa ni ngumu kiivyo! Anaamini baba anaweza kujenga nyumba.acha zako jombaa,we acha tujenge nje ya mji na tukimaliza tunanunua gari la kutuwahisha vibaruani bana.
 
mkuu umenisikitisha na kunishangaza sana... ....hebu wawekee paa lako Ili waige mfano........wasirudie tena kuweka paa la kizamani.......ni ombi tu........
Kama amekushangaza na kukusikitisha kwa nini unaomba akupe sample ya paa lake? Hahahahahaaa..... wabongo bana... Halafu hebu jiongelee mwenyewe, unawaombea wengine au wewe ndio unahitaji sample?

Assess mawazo na experiences za watu mbali mbali kabla ya ku rip kwamba wanashangaza kisha unaomba sample. Labda mtu kaona au kaishi sehemu ambazo hawapaui kwa staili hizo tena, anaweza kukufungua macho, unaanza ooooh anashangaza, anasikitisha... daah!

Ukitaka ufurahie ujenzi usiwe na daftari la kurekodi kila kitu.
Emotion driven decisions.
 
Back
Top Bottom