Tetesi: RC Chalamila kuhamishwa Dar

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Chalamila anaondoka DSM kutokana na kushindwa kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto za jiji hilo kubwa. Mahitaji ya wananchi na maono ya RC Chalamila vimeshindwa kuendana na hivyo mapendekezo yametolewa aondolewe hasa kipindi hiki cha kuomba uungwaji mkono.

Hayo yametokea baada ya Kitila Mkumbo kujaribu kufanya mikutano wananchi wakamkataa, Jerry Slaa amekataliwa adharani mbele ya Mawaziri wenzake huko Gwajima akizurura bila kutatua wala kuonyesha watu wa kawe atafanya nini.

Katika mikutano muhimu ya kupanga mipango ya jiji ambayo RC Chalamila ni MWENYEKITI ameshindwa kabisa kuwashawishi wajumbe kuimarisha miundombinu na kusimamia huduma.

RC Chalamila anaongoza jiji ambalo bikwazo vya biashara vinavyochangiwa na watumishi wa umma vimeongezeka na hakuna udhibiti. Mfano rushwa barabarani imekuwa kama huduma kwa wananchi na siyo jambo la kuogopa kama ukoma.

Huduma ya afya imeyoyoma, elimu hakuna mwelekeo jambo linalopelekea watoto kurandaranda mitaani hadi usiku na unifomu. Hakuna kiongozi wa serikali ikiwemo local Government anayewajibika.

Kwa analysis hii tayari exit yake ipo mkononi for implementation, anarudi ofisini kama Naibu Katibu Mkuu wizara ya Sanaa.

Pamoja na kwamba hoja zote za kumwondoa zina mashiko ila kidogo tusimshtukize. Kwa mantiki hiyo nimeandika uzi huu makusudi kuchelewesha uhamisho wa huyu mlevi mwenzetu asitumbuliwe usiku huu. Naamini kwa uzi huu Mdogo wetu Chalamila utapata muda wa kujiandaa unapohamishwa usiwe na mshtuko sana.

Umofia Kwenyuuuu.......Igweeeeeww
 
Chalamila anaondoka DSM kutokana na kushindwa kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto za jiji ilo kubwa. Mahitaji ya wananchi na maono ya RC Chalamila vimeshindwa kuendana na hivyo mapendekezo yametolewa aondolewe hasa kipindi hiki cha kuomba uungwaji mkono...
Tuna katiba ya hovyo sana mkuu wa mkoa anapoka majukumu ya Mayor??

Mkuu wa mkoa hana kazi yoyote ni cheo Cha uchawa tu
 
Back
Top Bottom