ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,076
- 49,785
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania BoT Emmanuel Tutuba amewataka watu wanaodai maisha ni magumu wafanye kazi kwani hakuna mwaka maisha yamewahi kuwa rahisi.
Gavana Tutuba ameelezea kwamba Hali ya Uchumi wa Nchi ni nzuri na inaendelea na Ukuaji mzuri.
My Take
Ambao wamewahi kuwa na maisha Mepesi waje watuletee ushuhuda.
===
Alichokisema Gavana,
"Hali ya uchumi wa Tanzania ni nzuri, kama mnavyofahamu kwenye robo tatu zilizopita uchumi ulikua kwa wastani wa kama 5.2%. Tunatarajia takwimu rasmi zitakapotoka kwa hii robo ya mwisho, tunaamini lile lengo la 5.3% linawezekana likawa limefikiwa kabisa. Na kama mnavyojua mfumuko wa bei umeendelea kuwa wa chini wa around 3% ambayo bado ni asilimia inayoruhusu ukuaji mzuri wa uchumi. Na unaendelea kuweka mfumo wa kutunza thamani ya fedha kuwa nzuri.
Sasa kinachotakiwa ni kila mmoja kutumia fursa hiyo katika kufanya kazi. Na wengine nimewasikia wakisema maisha yamekuwa magumu. Kimsingi maisha hayajawahi kuwa rahisi. Tangu Mungu alivyoumba dunia, alivyomuumba mwanadamu alisema nenda kale kwa jasho, kwa hiyo hakuna siku maisha yalikuwa rahisi. Kinachofanyika ni serikali kuweka fursa zinazomuwezesha kila mmoja atumie fursa hizo kwa namna yake yeye mwenyewe ili aweze kufanya maisha yake yawe rahisi. Kwanza kwa kufanya kazi halali ili apate kipato halali. Kikiwa kipato kikubwa, kitamuwezesha yeye kufanya shughuli zake. Maana katika uchumi huwa tuna cartegorize watu katika yale makundi manne.
Kuna wale watu ambao kipato chao ni kidogo kuliko matumizi yao, yaani total income inakuwa ni less than total consumption. Maana yake anaishi chini ya ule mstari wa umasikini. Na ya pili ni ile total income inakuwa sawa na total consumption. Sasa yale ni makundi ambayo mapato yao ni madogo kuliko matumizi. Sasa wao pia wanatakiwa kuangalia, fursa zinazowazunguka maana sisi kama Benki Kuu kupitia sera ya fedha tunachofanya zaidi ni kuweka mfumko wa bei uwe wa chini, kuhakikisha mzunguko wa fedha uendelee kuwa mzuri. Kuhakikisha pawepo ujazi wa fedha wa kutosha kwenye uchumi, kuhakikisha kama ni mabenki na watoaji wa mikopo wengine wawe na hizo fedha ili kutoa mikopo yenyewe. Ili kuwezesha wenye nguvu na utashi wa kufanya kazi, akafanye kazi.
Lakini kuna wale ambao tunaenda kwenye level ya tatu ambao, inakuwa total income ni sawa na total consumption plus savings. Ile ni ngazi ambayo wakidhi huduma na kuwawezesha kuishi, na aweze kupata akiba yaani savings. Sasa hao wana fursa zaidi ya kuendelea kupata faida kwasababu yeye anafanya vitu hayuko kwenye pressure, anachofanya ni kuangalia fursa ili atumie ile fursa kupata faida zaidi. Na kuna wale wengine ambao total income ni sawa na total consumption plus savings plus investments/reinvestments. Hao sasa ni wale matajiri ambao hao bado kwa serikali hii ya mama Samia ya Awamu ya sita, tunaona imerahisisha mazingira ya ufanyaji biashara lakini imeweka mazingira wezeshi ya kila fursa ya kiuchumi...."