Misingi ya Imani ya Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG)

tamsana

JF-Expert Member
Jan 13, 2012
3,245
7,116
Ni ukweli usiopingika kuwa kila imani (kanisa/dhehebu) lina misingi ya kuanzishwa kwake ambayo ndiyo inaisimamia.

Misingi ya Imani ya Tanzania Assemblies of God inasimamia misingi kumi na sita (16) ambayo kila muumini anatakiwa kuiishi. Misingi hiyo ipo kwa mujibu wa Biblia Takatifu ambayo ni Neno la Mungu.

Kwa kifupi mingisi hiyo ya Imani ya TAG imejipambanua na ndiyo inayotofautisha Kanisa la TAG na makanisa mengine ya Kipentekoste na hivyo kulifanya Kanisa la TAG kuwa na utulivu wa hali ya juu huku tukishuhudia utendaji wa Mungu Roho Mtakatifu kila mahali.

Misingi hiyo ni kama ifuatavyo:

1. Biblia ni Neno la Mungu.
2. Mungu mmoja tu wa kweli.
3. Yesu ni Mwana wa Mungu.
4. Anguko la mwanadamu.
5. Wokovu wa mwanadamu.
6. Ubatizo wa maji mengi na ushirika.
7. Ujazo wa Roho Mtakatifu.
8. Kunena kwa lugha mpya.
9. Utakaso.
10. Kanisa ni mwili wa Kristo.
11. Makusudi matano ya kanisa.
12. Mungu ndiye mponyaji.
13. Kufufuka na kunyakuliwa.
14. Utawala wa Yesu Kristo kwa miaka elfu.
15. Hukumu kuu ya mwisho.
16. Mbingu mpya na nchi mpya.

Nawatakia baraka za Bwana!
 
Attachments

  • T.A.G NATIONAL PRAISE TEAM - MISINGI YA IMANI (Official Video) (64 kbps).mp3
    4.1 MB

Vp msimamo kuhusu NDOA huko TAG manake TAG wa zamani walikua wanawacheka wakatoliki,waanglikana na walutheri kwa kufungisha ndoa wanandoa waliozaa tayari au wenye mimba lakini sikuhizi TAG nao wanafungisha ndoa unakuta mwanamke ana mimba kubwa tu.
 
Wanaofanya hivyo sio kwa kanisa la TAG. Tunasimamia misingi ya imani yetu.
 
Wadada wa TAG ni watamu balaa wakifuatia wa SDA
mdada TAG: kama unanipenda mchungaji kasema twende ukamuone tuombewe na uamie kanisani kwetu.
Mimi: Nihamie kwa nini?
Mdada TAG: Huku ndio yupo Mungu wa kweli anatenda miujiza.
Mimi: kwahiyo sisi wa madhehebu mengine Mungu wetu ni wa uongo?
Mdada TAG: Kama hutaki kumsikiliza mchungaji wangu basi tuachane.
Mimi: Poa

Haka katabia sikapendi, ivi haiwezekani kuamini walipo bila kuona imani za wengine si kitu?
 
Sema unaiishi wewe usiwasemee wengine kwenye mambo ya Mungu kila mtu anasimama yeye kama yeye.

,
Ndio maana msingi wa 15 unasema Hukumu Kuu ya Mwisho. Wote tunaishi na kuisimamia hii misingi tukiamini kuwa ambaye haiishi na kuisimamia atahukumiwa kwa matendo yake mema au mabaya.
 
Ndio maana msingi wa 15 unasema Hukumu Kuu ya Mwisho. Wote tunaishi na kuisimamia hii misingi tukiamini kuwa ambaye haiishi na kuisimamia atahukumiwa kwa matendo yake mema au mabaya.
Siku hizi katiba nzuri, msingi mzuri ya makanisa imebaki kwenye vitabu kuna upagani wa kutosha makanisani wengine wameahirisha kabisa kwenda mbinguni kwa hiyo kusifia dhehebu fulani kwa ujumla wake kwamba hakuna mawaa ni uchanga wa kiroho.
 
Tumieni mitandao ya kijamii kuhubiri injili ya ufalme( Methew 24:14) kuliko kusifia madhehebu yenye madhaifu mengi ya wazi. Sifa za injili ya ufalme hainui dhehebu Wala mhuburi flani bali humwinua Kristo peke yake
 
mdada TAG: kama unanipenda mchungaji kasema twende ukamuone tuombewe na uamie kanisani kwetu.
Mimi: Nihamie kwa nini?
Mdada TAG: Huku ndio yupo Mungu wa kweli anatenda miujiza.
Mimi: kwahiyo sisi wa madhehebu mengine Mungu wetu ni wa uongo?
Mdada TAG: Kama hutaki kumsikiliza mchungaji wangu basi tuachane.
Mimi: Poa

Haka katabia sikapendi, ivi haiwezekani kuamini walipo bila kuona imani za wengine si kitu?
Ni mfumo wa mafundisho yao, siwalaumu
 
Back
Top Bottom