Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,199
- 1,969
Waislamu nao wameamua kujipanga ili kuhakikisha kuwa Rais, wabunge na madiwani hawachaguliwi kwa misingi ya kidini.
Ikiwa ni counter attack dhidi ya kanisa wanazuoni wa kiislamu pamoja na mashekhe 15 wameunda jopo ambalo pamoja na mambo mengine litaratibu na kusimamia mchakato mzima wa uchaguzi mkuu ujao kwa maslahi ya waislamu! Jopo hilo lilizinduliwa katika hoteli ya Starlight, Dar tarehe 21/06/2009. Mratibu wa jopo hilo, Sheikh Mohamed Idd alikemea ubaguzi wa kidini katika masuala yote ya uchaguzi.
Hata hivyo, japokuwa sababu zilizotolewa na jopo la wanazuoni hao na masheikh zinaweza kuonekana kuwa ni hofu yao dhidi ya kasi ya maandalizi ya Kanisa katika uchaguzi ujao lakini uzofu unaonyesha kuwa kama malengo ya jopo hilo yatakuwa kama yalivyo, linaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa, maana katika chaguzi zilizopita, hasa uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, misikiti mingi ilishutumiwa kwa kuwapigia debe wagombea wa chama fulani cha siasa.
Licha ya makanisa hayo kushutumiwa kuendesha kampeni kwa ajili ya wagombea mbalimbali, lakini hali ilikuwa tofauti na kampeni zilizodaiwa kufanywa misikitini, ambazo kwa asilimia kubwa, zilihusisha chama kimoja huku kanisa likishutumiwa kutumiwa na vyama mbalimbali!
Source: Nyakati, Juni 28-Julai 4, 2009.