Mishahara yapanda kwa zaidi ya 10%

Mimi niliposikia kwenye hotuba kwamba watazingatia vigezo kama kupanda gharama za maisha na mfumuko wa bei nilijua tu kwenye hizo asilimia maana ukiangalia data za uchumi mfumuko wa bei Tanzania kwa mwaka huu wanasema ni asilimia 7.2. Kwa hiyo nilijua tu watacheza maeneo hayo tu na si zaidi.

Kweni CPI ni kupanda mshahara au ni haki ya mfanyakazi kila ifikapo July ya kila mwaka? lakini pia sishangai wakisaema wamepandisha mshahara
 
Kupandishwa kwa mishahara kuzingatie kupanda kwa gharama za maisha na hapo ndipo serikali itakuwa imemsaidia mwananchi mwajiriwa na aliyejiari, kwa sababu mshahara huo utanunua unga wa mahindi, maharage, sukari, mafiuta ya taa, nauli za daladala n.k. kwa sababu endapo bei za vitu hivi itaendelea kuwa juu basi ni wazi serikali itakuwa haijampunguzia mzigo wa gharama za maisha mwananchi huyu, pia mwajiriwa wa serikali na sekta binafsi anakatwa kodi ya 14% ya mshahara wake, kwahiyo serikali ipunguze kodi na pia iangalie namna ya kupunguza gharama za vitu vinavyotumiwa nyumbani kila siku na hapo ndipo mshahara huo utakapomnufaisha mwananchi.
 
kama hizi habari ni za kweli.....basi mipango yangu
na ndoto zangu kwishney kabisa.
 
Kupandishwa kwa mishahara kuzingatie kupanda kwa gharama za maisha na hapo ndipo serikali itakuwa imemsaidia mwananchi mwajiriwa na aliyejiari, kwa sababu mshahara huo utanunua unga wa mahindi, maharage, sukari, mafiuta ya taa, nauli za daladala n.k. kwa sababu endapo bei za vitu hivi itaendelea kuwa juu basi ni wazi serikali itakuwa haijampunguzia mzigo wa gharama za maisha mwananchi huyu, pia mwajiriwa wa serikali na sekta binafsi anakatwa kodi ya 14% ya mshahara wake, kwahiyo serikali ipunguze kodi na pia iangalie namna ya kupunguza gharama za vitu vinavyotumiwa nyumbani kila siku na hapo ndipo mshahara huo utakapomnufaisha mwananchi.

Kutokana na kupanda kwa gharama za maisha makusanyo ya TRA yameongezeka? Tuisaidie Serikali yetu kupanua wigo wa makusanyo ya kodi ili tuwe na haki ya kudai stahili zetu kwa data. Au tunataka wachapishe pesa nyingi isiyo na thamani ili kulipa mishahara itakayotufurahisha?
 
Hili suala la mishahara mmmh 10% of 200,000 Serikali sikivu itamsaidiaje mfanyakazi ilhali
haijapandishwa miaka nenda.
 
Ongezeko hilo la mishahara ni kutekeleza ilani ya CCM ya kurudisha nyuma maendeleo ya nchi kwa kasi zaidi, ari zaidi na nguvcu zaidi. Mtumishi asiyeweza kumudu gharama za maisha hawezi kuleta TIJA katika kazi yake. Tujiandae kuona watoto wetu(walalahoi) wakiendelea kufeli mashuleni, madaktari wakishindwa kuhudumia wagonjwa kwa sababu wakijishughulisha na kazi binafsi ili wamudu maisha n.kCCM iondoe magamba kwa kuboresha maslahi ya watumishi wa umma........ hatimaye kuboresha huduma za jamii
 
Inamaana anayepokea laki 1 kaongezwa elfu 10 tuu! haya ndoo maisha bora kwa mtanzania kwelikweli,, safiiiiiiiiiiiii!
Wana Magamba mpoooooooo>????????????
 
Kweli wabunge wa chama changu nimeamini hawako makini,,,,waliamua kusema mshahara umepanda kwa 40% kumbe siyo
nyie wabunge wa chama changu muweni makini hata siku moja basi mbona mnawapa umaalufu hawa cdm kwa kuonyesha wako makini kuchambua mambo kuliko nyie???? Kama vile hamkwenda shule jamani

gamba limetushinda kuling'oa hata hoja kuchambua pia zitushinde!!!!!!
 
Inamaana anayepokea laki 1 kaongezwa elfu 10 tuu! haya ndoo maisha bora kwa mtanzania kwelikweli,, safiiiiiiiiiiiii!Wana Magamba mpoooooooo>????????????
Ndio maana yenyewe hiyo mkuu then kuna kukata kodi 14% kama kawaida, so hapo anaweza chukua 4500 kama ongezeko!
 
Naomba kuuliza, hivi Rais alitamka wakati wa kampeni iliyomwingiza ikulu kuwa anaongeza mishahara ya wafanyakazi kama walivyopendekeza chama cha wafanyakazi, je?? hii kauli ilitekelezwa?????????
 
Nyongeza ya mshahara kwa watumishi wa umma iliyotajwa kuwa asilimia 11 kima cha chini na 8.6 vima vingine, maana yake ni kuwa kima cha chini kimeongezwa asilimia tatu(fanya mahesabu) na asilimia 0.6(fanya mahesabu pia).
Sio kwamba nakanusha ongezeko la asilimia 11% na kuwa hesabu zinapiga chenga la hasha. mantiki hapa ni hii, ikiwa kiwango cha mfumuko wa bei hadi sasa ni asilimia 8% maana yake ni kuwa katika asilimia 11% kima cha chini ukitoa asilimia 8 kufidia mfumuko wa bei unabakiwa na asilimia 3% na kwa wale walio katika kundi la asilimia 8.6 ukitoa 8% ya mfumuko wa bei utabakiwa na 0.6%.
Hii haitaji kwenda chuo kikuu kujua kuwa hakuna lolote katika ongezeko. na kwa wabongo niwajuao mimi watapandisha bei za vitu maradufu kwa vile tu wamesikia mshahara umeongezeka.kivumbi ni kwetu wapangaji wa nyumba,naomba wenye nyumba nao wasipigie mahesabu asilimia 11%! kwani hakutakalika.
ni bora selikali ingeacha ile increment ya kawaida ambayo huingia kimya kimya.
Mungu Ibariki Tanzania, nawasilisha.
,
 
kwa taarifa yako mshahara huwa hauongezeki ila kinachofanyika ni kuendana na inflation
 
Wakuu kwa taarifa yako mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia 30 June 2011 ni 10.7%.Pitia mtandao wa taasisi ya Takwimu,bureau of statistic wametoa data.Kwa maana hiyo kima cha chini kinatarajiwa kuongezwa kwa 0.3%.Viwango vingine vimepunguzwa kwa 2.1%
 
Nalia na waalimu... Waalimuuuu! Nyie ndo mnaosimamia upigaji wa kura vituon na mnaongeka vizur tuuu mnatoa ushindi kwa wasio stahili. mna nafasi ya kuleta mabadiliko, amkeni!
 
Back
Top Bottom