Mishahara yapanda kwa zaidi ya 10%

Kila mfanyakazi sio hao tu.
Sio kweli kwamba kila mfanyakazi anatakiwa kuuona ukikutwa nao kama huhusiki itakula kwako. Ndio maana utakuta waraka husika ukeelekezwa kwa Wakuu wa Idara zinazojitegemea, Wakurugenzi wa Halmashauri, Majiji, Manispaa, Makatibu Wakuu wa Wizara na Wakuu wa wakala wa serikali. Narudia tena sio kila mtu ndio maana huyo Afisa Utumishi hajakuruhusu ukae nao muda mrefu otherwise ungekuja na full information
 
Kama ni kweli, hiyo ni dhihaka kwa wafanyakazi. Pesa ya posho ya vikao kwa wakubwa ipo, lakini ya kulipa mishahara inakuwa tabu, why?????
 
hako ka inremenent ni kama kulambiha mtu asali na ncha ya sindano mana aaskia utamu kidogo na kuanza kuugulia maumivu ya kuchomwa na hio sindano. kuna faida gani kusema mishahara imepanda wakati katika mwaka mpya wa fdha uliopita unga ulikuwa 600 sasa 900, petrol 1640 sasa 2200 mbali ya baadhi ya tozo za mafuta hayo kuondolewa? mafuta ya taa sasa ni 1800/= toka 1350/= sasa hiyo 10% ni nini kama sio utani? ada za watoto
 
dah! wafanyakaz wa uuma kwisha kabisa, matokeo yake serikali ijiandae kuyaona siku za karibuni
 
jaman hapo mwalimu wa sekondari alikua anapata 287,000 sasa ukiongeza 10% na ukicheki mfumuko wa bei mm naona hamna kitu hali itabaki vile vile.
Hii sirikali bana imezidi kuwaona watumishi wajinga!

Atafikia kima cha chini cha CDM cha TShs. 315,000
 
we unakinga hyo.... uongezwe nin??????? mwalimu anapata laki mbili....... upuuz wa nchi hiiiiii..........

We umejuaje kama yeye hiyo ndio salary yake mkubwa acha hizo bwana usiharibu uzi we mwenzio he was trying to share some info wit u
 
inflation ni more that 12 percent i guess lakini increment ni around the said percent.anyaway tumezoea hivi hivi ...
 
Normally kama mtu anayepokea TShs. 1,000,000 akipata nyongeza ya 10%; yule wa chini yaani wa TShs 135,000 nyongeza yake inaweza kupanda hata 20%. Kwa maani nyingine mshahara mdogo hupandishwa kwa %age kubwa kuliko mshahara wa juu
 
Hakuna ongezeko la mshahara serikali wewe, hiyo ni increment ya kawaida ambayo hufanyika kila mwaka; huyu naye sijui anafanya nini kwenye osifi za serikali, kila anachoona yeye anaona ni habari! serikali ya Kikwete haina watu kabisa sijui anawaokota wapi? huyo ni mtu yupo kwenye ofisi ya Umma? akiona forgery ya wizi wanaofanya yeye na Bosi wake haleti hapa akisoma barua za ofisi ndio anatuambia hapa.
 
Wana JF,

Nimeona waraka wa msajili wa hazina wa mishahara itakayolipwa mwezi huu mwishoni inaonekana mishahara imepanda kwa zaidi kidogo wa asilimia 10. Waraka wenyewe alikuwa nao Ofisa utumishi akanionesha kidogo na scale niliyoiona inaonesha asilimia hizo. Ndugu wakuu nawasilisha.

Hakuna ongezeko la mshahara serikali wewe, hiyo ni increment ya kawaida ambayo hufanyika kila mwaka; huyu naye sijui anafanya nini kwenye osifi za serikali, kila anachoona yeye anaona ni habari! serikali ya Kikwete haina watu kabisa sijui anawaokota wapi? huyo ni mtu yupo kwenye ofisi ya Umma? akiona forgery ya wizi wanaofanya yeye na Bosi wake haleti hapa akisoma barua za ofisi ndio anatuambia hapa.
Arafat umemaliza
 
Sio kweli kwamba kila mfanyakazi anatakiwa kuuona ukikutwa nao kama huhusiki itakula kwako. Ndio maana utakuta waraka husika ukeelekezwa kwa Wakuu wa Idara zinazojitegemea, Wakurugenzi wa Halmashauri, Majiji, Manispaa, Makatibu Wakuu wa Wizara na Wakuu wa wakala wa serikali. Narudia tena sio kila mtu ndio maana huyo Afisa Utumishi hajakuruhusu ukae nao muda mrefu otherwise ungekuja na full information

Ndugu ninachosema ni kuuona na kuangalia mshahara wako, lakini viongozi wa vyama vya wafanyakazi huwa wanapewa nakala ili kila mfanyakazi aweze kuuona kama maofisa utumishi watamwekea ukiritimba. Unajua mambo mengi viongozi wanafanya kwa sababu ya woga tu. Hebu fikiria mshahara ni haki ya mfanyakazi inawezekanaje usema document inayoonesha haki za mtu ni siri? Ndio maana kuna wafanyakazi wengine waliwahi kulipwa mishahara midogo tofauti na waraka unavyoelekeza kwa hiyo nasisitiza kila mfanyakazi ni muhimu kuuona ili ajue kwamba kile anacholipwa ndicho chenyewe.
Halafu wakati mwingine ni uzembe tu au kutojua kwa wafanyakazi kwani ukiwaambia utumishi wakupe uangalie mshahara wako hawawezi kukataa eti ni siri wanakupa na unaweza kukaa nao kwa muda fulani. Hii ya leo jamaa hajanipa muda mrefu kwa sababu ndio wanaandaa schedule za mabadiliko ya mishahara ili kuipeleka hazina mishahara ya Julai iweze kulipwa mipya na sio kweli kwamba hajanicha nao kwa sababu ni siri
 
Hakuna ongezeko la mshahara serikali wewe, hiyo ni increment ya kawaida ambayo hufanyika kila mwaka; huyu naye sijui anafanya nini kwenye osifi za serikali, kila anachoona yeye anaona ni habari! serikali ya Kikwete haina watu kabisa sijui anawaokota wapi? huyo ni mtu yupo kwenye ofisi ya Umma? akiona forgery ya wizi wanaofanya yeye na Bosi wake haleti hapa akisoma barua za ofisi ndio anatuambia hapa.

Nimeishasema na narudia tena waraka wa msajili wa hazina sio barua ni document iliyobeba haki za watu. na kwa taarifa yako unaweza kupatikana hata ofisi za TUCTA, RAAWU, CHODAWU, TRAWU na vyama vingine vya wafanyakazi.

Mpaka sasa hakuna annual increment inayofikia laki moja kwa taarifa yako, nimeangalia scale nyingi za watumishi wa umma kama PGSS, PTSS, PHTS, TGS, TGHS, TGOS, TUJ, PUTS na nyingine hata wanaopata mishahara ya kufiki milioni mbili hakuna annual increment inayofikia hapo. Kwa hiyo, naomba uelewe nafahamu ninachokisema
 
Jamani pigeni kazi tu hiyo mishahara itawaumiza vichwa kichwa, stress na hatimaye muugue migonjwa ya ajabu ajabu. Mishahara haisaidii, kama unataka pesa kuwa mbunifu bila kuvunja sheria za nchi.
 
To be exact ni kama 10.7% au waliosoma hesabu watusaidie kucalculate kutoka 1,023,100 mpaka 1,133,400/=. Ni asilimia ngapi? hiyo ndiyo scale niliyoiona

yes you are right, to be more exactly it is 10.780959827973804%
 
Back
Top Bottom