sir.JAPHET
JF-Expert Member
- May 18, 2012
- 699
- 133
Jumamosi, Agosti 25, 2012 06:41 Na Bakari Kimwanga, Dar es Salaam
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willibroad Slaa, amesema kitendo cha Rais Jakaya Kikwete kusaini nyongeza ya mishahara na marupurupu ya wabunge hadi kufikia Sh milioni 11 kwa mwezi hakiwezi kukubalika.
Amesema kwamba, pamoja na kwamba lengo la Rais Kikwete ni kuwafanya wabunge wafanye kazi kwa moyo, hatua hiyo italeta manunguniko kwa kuwa wafanyakazi wengi wamekuwa wakilalamikia maslahi madogo wanayolipwa.
Dk. Slaa alitoa shutuma hizo juzi alipokuwa akihutubia mikutano ya hadhara katika vijiji vya kata mbalimbali za Jimbo la Morogoro Mashariki, Wilaya ya Morogoro.
Katika mikutano hiyo, Dk. Slaa aliwataka wafanyakazi kote nchini, kutohamishia hasira zao kwa wananchi badala yake waendelee kuikaba koo Serikali kwa kuwa ndiyo chanzo cha ugumu wa maisha yanayowakabili.
Tangu juzi nimekuwa nikisoma taarifa mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii, naona walimu wanatumiana ujumbe mfupi wa simu katika simu zao na kama kweli wataufanyia kazi, masikini watoto wetu hawa walioko shuleni na taifa lote tumekwisha.
Kama kweli ujumbe ule wa kwenye simu wanaotumiana walimu ambapo wanaelekezana kuwafundisha uongo wanafunzi ikiwa ni ishara ya kuonyesha kinyongo chao cha kupuuzwa kwa madai yao ya msingi na Serikali ya Kikwete, tunaelekea pabaya. Kama kweli wataamua kuufanyia kazi taifa hili litaangamia zaidi ya lilivyoangamia sasa.
Chonde chonde walimu wangu, naombeni hasira zenu msizihamishie kwa watoto wangu hawa wasiokuwa na kosa lolote, kila mtu mwenye akili timamu anajua madai yenu ni ya msingi sana, lakini adui yenu ni Kikwete, adui yenu ni Serikali, alisema Dk. Slaa.
Aidha, alisema hivi sasa kumekuwa na matamshi mabaya dhidi ya walimu ambapo wanaambiwa Serikali haina fedha za kuwalipa stahiki zao.
Wakati Serikali ikiwambia wananchi hakuna fedha, leo hii sekta ya ya afya haina dawa wala vitendea kazi hospitalini.
Pamoja na hali hiyo, bado Rais Kikwete anaamua kupandisha mishahara na marupurupu ya wabunge kutoka milioni 7 hadi kufikia Sh milioni 11.
Kwa hali hii, hakika Rais Kikwete pamoja na Serikali yake ya CCM haiwatendei haki wananchi wa taifa hili, kwani hivi sasa vijana wetu ambao ni maaskari polisi, mishahara yao ni kidogo.
Yaani hata posho yao wametetewa na wabunge wangu huko bungeni ndiyo imepandishwa kwa maneno kutoka 100,000 hadi 150,000.
Bado wanafanya hivyo wakati wanajua makundi mengine wakiwamo walimu, madaktari, wanajeshi na makundi mengine wana malalamiko ya msingi, sasa ni kitu gani hiki?.
Lakini, kumbukeni kwamba, mambo ya namna hii yanaweza kufanywa na uongozi mbovu usiozingatia vipaumbele katika kusukuma maendeleo na ustawi wa watu wake, alisema Dk. Slaa.
Alisema vitendo hivyo vya Serikali vimekuwa vikiwatia vishawishi baadhi ya watumishi kama walimu na kulazimika kufanya kazi zingine jambo ambalo siyo zuri wa ustawi wa taifa.
Alitolea mfano wa walimu wa kike ambao wanalazimika kupika na kuuza maandazi au vitumbua, ili kupata fedha za kujikimu na kuendesha maisha ya familia zao.
Toa Maoni yako kwa habari hii