Mishahara ya mwezi Februari itatoka lini?serikali mbona inatudhalilisha watumishi wake?

bushman

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,411
743
Jana jioni mwenye dhamana ya mishahara udom, katoa barua ya kusema hajapokea fedha yoyote kutoka hazina kwa hiyo hakuna mshahara mpaka atakapo pata fedha, sio kosa lake kasema ukweli mimi nalia na mkuu wa kaya j.k.

Mbona mnatudhalilisha mjini hapa? Sijui tasisi nyingine za serikali kama wamelipwa ila hapa matangazo yameshatoka kuwa mpunga haujaingia kutoka serikalini.

Tunaishije mjini hapa?spika makinda anna anajua vizuri ugumu wa maisha dodoma ndio maana anakomalia posho,sasa tusiokuwa na posho na tunaishi dodoma miaka yote tunafanyeje?hali mbaya!!!!!!!!
 
Nchi imefilisika, wanabembeleza mabenki wawakopeshe, subiri tu utalipwa.
 
Jana jioni mwenye dhamana ya mishahara udom, katoa barua ya kusema hajapokea fedha yoyote kutoka hazina kwa hiyo hakuna mshahara mpaka atakapo pata fedha,sio kosa lake kasema ukweli mimi nalia na mkuu wa kaya j.k mbona mnatudhalilisha mjini hapa?sijui tasisi nyingine za serikali kama wamelipwa ila hapa matangazo yameshatoka kuwa mpunga haujaingia kutoka serikalini,tunaishije mjini hapa?spika makinda anna anajua vizuri ugumu wa maisha dodoma ndio maana anakomalia posho,sasa tusiokuwa na posho na tunaishi dodoma miaka yote tunafanyeje?hali mbaya!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Mjomba bandiko lako limenisikitisha sana!:embarassed2:
Poleni sana kama hamjashikishwa hadi leo...wakiendelea hadi mwisho wa wiki dawa mgomo tu kama madaktari!
 
Mzeee home hapaingiliki,hali mbaya kibaya zaidi taarifa haijaweka time frame imesema zitalipwa zikiletwa kutoka serikalini,lini hiyo?kama sio kutuletea matatizo kwenye familia zetu?
 
Nilishawahi andika humu 'hazina ya serikali imekauka' watu wakanikebehi hapa! Nasahivi serikali haiwezi kufanya jambo mpaka upige kelele.
 
watumishi wa umma wanataabika sana bongo, mshahara tarehe 36 dah,
 
mwezi huu wamejitahidi kuwalipa madaktari kwanza nyie wengine mtasubiri kwanza hadi zipatikane, c umeona hata wabunge wamegomewa nyongeza? tuvumilie hali serikali nimbaya kifedha
 
mliambiwa mapema mtajuta kumchagua ****** sasa matokeo ndio hayo
 
Hazina imekauka ilhali maparty ya wizara bado yanaendelea! MaV8 yanatembea na viyoyozi juu!!
 
Nchi imefilisika, wanabembeleza mabenki wawakopeshe, subiri tu utalipwa.

Mabenki nayo yako hoi mkuu...Rostam kahamisha ngawira zake zote toka kwenye mabenki ya hapa...Kahamishia nchini Malysia
 
Mzeee home hapaingiliki,hali mbaya kibaya zaidi taarifa haijaweka time frame imesema zitalipwa zikiletwa kutoka serikalini,lini hiyo?kama sio kutuletea matatizo kwenye familia zetu?

Ina maana we unaishi kwa kutegemea mshahara tu? imeandikwa mtu hataishi kwa mkate tu mkuu!
 
Jana jioni mwenye dhamana ya mishahara udom, katoa barua ya kusema hajapokea fedha yoyote kutoka hazina kwa hiyo hakuna mshahara mpaka atakapo pata fedha,sio kosa lake kasema ukweli mimi nalia na mkuu wa kaya j.k mbona mnatudhalilisha mjini hapa?sijui tasisi nyingine za serikali kama wamelipwa ila hapa matangazo yameshatoka kuwa mpunga haujaingia kutoka serikalini,tunaishije mjini hapa?spika makinda anna anajua vizuri ugumu wa maisha dodoma ndio maana anakomalia posho,sasa tusiokuwa na posho na tunaishi dodoma miaka yote tunafanyeje?hali mbaya!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

SIo UDOM tu mkuu hata DUCE nako bado hawajacheka
 
Poleni wote Dodoma na wale walio kosa mishahara hadi leo.

Yapasa tumshauri Mkuu wa kaya akakope kwa wale matajiri aw TZ walio kwenye list aliyopewa Davos.

Mbona hela iko nyingi tu TZ !!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom