Mishahara ya madaktari wetu; wanastahili nini?

Kama wanadai nchi ni maskini, sasa kwa nini umaskini usiwe kwa wote?!!!!!!! Inasikitisha sana tena sana
 
Kwa vile wafanyakazi Benki Kuu wanastahili maisha ya juu kama ya wale wa Benki za nchi zilizoendelea na wabunge wetu nao wanastahili maisha kama ya wabunge wa nchi zilizoendelea; na kwa vile wapo watu wanaostahili katika utumishi wa umma maisha ya kimagharibi.. naomba kuuliza je madaktari wetu wanalipwa mishahara inayolingana na madaktari kama wa nchi za US na UK?

Je itakuwa vibaya kama na wao wakiamua kudai "mastahili" yao kutoka kwa watawala?

au hawastahili nyumba nzuri zenye mabwawa nje na magari na posho kubwa zaidi? Labda niulize tu kwa wastani daktari wa Tanzania analipwa kiasi gani na kiasi kinalinganishwa vipi na daktari wa US.

Muhimu ni kuwa mwangalifu katika maelezo yako. Si kweli kwamba mishahara ya madaktari wa UK au US ndiyo mikubwa kuliko yote Duniani na si kweli kwamba wafanyakazi wa BOT wanapata salaries kubwa sana kihivyo. Kuna nchi nyingi sana zinawalipa wafanyakazi wao, wakiwemo doctors hela nzuri sana. Kumbuka pia kwa BOT hapa bongo, issue ni ufisadi. Mishahara yao ni mdogo sana ukifananisha na financial institutions zingine nyingi tu nchini. Mfano mwngine ni kwamba Rais wa Cameroun anapokea mshahara mkubwa kuliko yoyote Duniani. Maana yake kuwa hata maafisa wake wa ngazi za juu wako karibu yake kimshahara pia. Usisahu kubwa wabunge wa Kenya wanapokea mishahara ya juu sana kuliko nchi nyingi sana Duniani.

Turudi kwenye point. Suala siyo madakari kupokea mshahara sawa na wale wa UK au US. Suala ni kuwawezesha waweze ishi modest life. Lakini madaktari ni sehemu ndogo sana ya wataalamu wengine muhimu wa sector mbali mbali nchini. Hakuna aliye muhimu kuliko mwenzake. Tuongelee kuhusu mishahara ya Watanzania kuimarishwa kulingana na uwezo wa kiuchumi wa nchi.
 
Thanks Saitama, umesahau, hata hiyo 650000 ni basic, take home yake ni laki nne. Miaka sita ya shule chuo cha udaktari na internship. Si bora kwenda China kusomea udaktari huohuo miaka mitatu kama kina nanii?

Leka
 
Turudi kwenye point. Suala siyo madakari kupokea mshahara sawa na wale wa UK au US. Suala ni kuwawezesha waweze ishi modest life. Lakini madaktari ni sehemu ndogo sana ya wataalamu wengine muhimu wa sector mbali mbali nchini. Hakuna aliye muhimu kuliko mwenzake. Tuongelee kuhusu mishahara ya Watanzania kuimarishwa kulingana na uwezo wa kiuchumi wa nchi.

Hivi unajua Waziri Mkuu wa Tanzania akistaafu au akiondoka (hata kwa kujiuzulu kwa kashfa kama Lowassa) analipwa pensheni (hata kama amekaa siku moja ofisini?). Unajua hesabu ya pensheni yake hupimwaje? Ukiangalia utaona kuwa mishahara ya Watanzania imeshaboreshwa... tatizo ni kuwa Watanzania hao ni wanasiasa na watawala wanaotokana nao!
 
mie sioni niseme nini tena katika hili...ila ni busara kila mtu awe mwizi wa mali ya umma., ale rushwa kadri ya uwezo wake....watokee warloads wakamate himaya zao watu wakipita wawalipe road tolls na kila aina ya uchavu hata tufikie level ya somalia....nitafurahi sanaaaaa...we millions got nothin to lose...nchi ikiwa haikaliki ndipo kila mtu atatia akili kichwani na kumheshimu kila tom,harry and dickens aliyemzunguka
God forbid. Lakini hii ndio inatakiwa maana punda hendi bila mjeledi.

ni tatizo kubwa sana, madaktari,walimu na watumishi wengi wa umma...mpaka mapolisi wanalipwa kidogo sana, ndio maana hata rushwa haitisha maana wanataka kujikimu, na hili pia linashusha ufanisi katika taaluma zao sana....
Ukiondoa madaktarihao walimu napolisi ni stahili yao. Ona polisi walivyofunga ndoa na CCM. Ukipita pale Osterbay kwenye kambi yao kule wamejenga vibanda vya maboksi utafikiri vya kufugia kuku halafu wameweka na antena za TV. Hapo hapo wakiambiwa kwenda kwenye maandamano ya KAFU utaona wanavyonyasa raia. Walimu nao ndio hao hao wasimamizi wa vituo vya kura akija mtu hajui kusoma utawaona wanamweleza chagua CCM. Kama hawawezi kujisaidia wenyewe sasa nani awasaidie?
 
Muhimu ni kuwa mwangalifu katika maelezo yako. Si kweli kwamba mishahara ya madaktari wa UK au US ndiyo mikubwa kuliko yote Duniani na si kweli kwamba wafanyakazi wa BOT wanapata salaries kubwa sana kihivyo. Kuna nchi nyingi sana zinawalipa wafanyakazi wao, wakiwemo doctors hela nzuri sana. Kumbuka pia kwa BOT hapa bongo, issue ni ufisadi. Mishahara yao ni mdogo sana ukifananisha na financial institutions zingine nyingi tu nchini. Mfano mwngine ni kwamba Rais wa Cameroun anapokea mshahara mkubwa kuliko yoyote Duniani. Maana yake kuwa hata maafisa wake wa ngazi za juu wako karibu yake kimshahara pia. Usisahu kubwa wabunge wa Kenya wanapokea mishahara ya juu sana kuliko nchi nyingi sana Duniani.

Turudi kwenye point. Suala siyo madakari kupokea mshahara sawa na wale wa UK au US. Suala ni kuwawezesha waweze ishi modest life. Lakini madaktari ni sehemu ndogo sana ya wataalamu wengine muhimu wa sector mbali mbali nchini. Hakuna aliye muhimu kuliko mwenzake. Tuongelee kuhusu mishahara ya Watanzania kuimarishwa kulingana na uwezo wa kiuchumi wa nchi.

Ni kweli mishahara ya watanzania wote iimarishwe hata wa kada ya chini kabisa na siyo ya madaktari peke yao maana kila mtu ana umuhimu wake kazini. Mtu amefanya kazi ya kudeki mahali kwa miaka 10 na bado analipwa 150,000, its not fair...
 
MM Nashukuru sana kwa kuleta hii hoja kwenye uwanja wa majadiliano. Mimi ni daktari na kutokana na huo mshaara ushuzi ulioonyeshwa hapo juu nimejiamulia kubwaga manyanga nafanya vitu vingine kabisa. kwa nini nipate dhambi za bure? Kama unashindwa kutimiza wajibu wako hiyo ni dhambi na mimi sikuwa tayari kufanya hivyo.

Kuna neno uzalendo limeimbwa hapo juu but sijui huyo mdau anaanisha uzalendo gani? Kama keki ya taifa ni yetu tugawane wote. Wewe huwezi kusema mbunge wa darasa la nne posho kwa siku laki moja kwa vile maisha magumu halafu daktari unampa laki sita na nusu kwa siku 30! Jamani tumuogope Mungu. Hana vikao, hana posho, hana mafuta hata gloves za kupiga PR na PV hamna pia, mazingira ya kazi magumu, vitendea kazi hamna yeye ni nani haswa hadi akae hapo...

Hawa viongozi wetu wataendelea kufa vifo vya mende. Wanaweza kwenda India kwa Check up na elective procedures lakini akipata heart attack au emergency nyingine hawezi fika hata airport kutoka Kimara achilia mbali India! Kama hakutakuwa na mwamko wa kuimarisha huduma za afya hali itaendelea kuwa mbaya. Wadanganyika nawasikitikia sana.

Kinachotokea sasa kutokana na utandawazi na fursa mbali mbali vijana madaktari wazuri wanaacha kutibu na kufanya mambo mengine yenye kipato. Mnachotakiwa kujua ni kuwa madaktari wengi ni watu wernye akili kuliko watu wa kawaida na akijitune kidogo tu anafanya kazi nyingine vizuri sana kwa hiyo wanaondoka kimya kimya.

Hesabu zinaonyesha kuna kama madaktari 2400 Tanzania lakini wanaotibu najua hawafiki 800. Wapo hapo hapo mjini wanapambana na MKUKUBI wao(Mkakati wa Kupambana na Umaskini Binafsi).

Sintosahau mwaka 2005 wakati tukiwa na mgomo kutaka mshahara uongezwe kutoka laki na nusu(150,000) kwenda milioni moja (1,000,000) Usicheke ukweli ndo huo nilikutana na afisa mwajiri wa Wizara ya afya jina lake nalihifadhi, Tukawa tunamwambia kama Wizara haiongezi hela tunaacha kutibu na kumwambia kuwa tupo adimu, akasema kuwa Nani kakwambia hata mkiondoka Watanzania watatibiwa kwa dharau ya hali ya juu. Niliinua macho juu nikamwambia Mungu niepushe na hawa vihiyo, nikaangalia mbele na sijarudi tena kudai milioni moja baada ya kusoma kwa jumla ya miaka 20! Give me a break.

Tatizo kubwa Tanzania kila mtu anayevaa koti jeupe anaitwa daktari. Hata akiwa mchinja nyama. Mtu akienda hospitali kuanzia karani, mfagiaji, nurse assistance, binzari wote wanaitwa madaktari. Serikali imetumia huu mwaya kuwakanya madaktari sana lakini kwa anayejua kitu ambacho Daktari anachoweza kufanya in relation to Medical Assistant, AMO na kada nyingine anajua namaanisha nini.

Nisijekuwachosha kusoma ila kwa mwendo huu wa serikali yetu kwa kuwa na double standards kwa wafanyakazi wake sioni mwanga. Nilishang'atuka kazi kwenu mliopo kwenye fani. Njaa na maendeleo havipikiki kwenye chungu kimoja.

Naomba kuwakilisha

Dr. Mchapakazi unatisha! Yaani ingawa sipendi kusoma maelezo marefu lakini nikajikuta nafuatilia story yako hadi mwisho. Kweli madaktari wanaweza mambo mengi,hata uandishi dr. uko juu: usicheke,give me a break,etc..hahahahaha
 
Yes, we have to be creative but we also have to hold our government responsible to meet its obligations. That is all I am asking for. Daktari aliyesomeshwa kwa mkopo hata kabla hajaulipa mkopo huo aende benki kukopa tena ili aanzishe private practice? Does it really make sense?

Ni zipi obligations bora za serikali? Watu wengine wanaweza kua na mawazo tofauti sana na yako lakini ukichunguza bado utaona it makes sense hata kwa aliyesoma kwa mkopo kupewa mkopo mwingine, ila hamna atayekuambia ni rahisi kupata matokeo mazuri ya huo mkopo kwa mhusika baada ya kupewa.

Kama serikali inakopesha kusomesha, pia inaweza kopesha ama kudhamini mikopo toka mabenki kwa wahitimu ili waweze kuwekeza. Elimu ni kuwawezesha raia kua na mwangaza mpana lakini baada ya kupata elimu mkopo utawawezesha raia kutumia elimu yao kuzalisha mali zaidi. Kwa kua nia ya serikali ni kuinua hali ya maisha ya watu basi ni nia nzuri tu na kuwakopesha mitaji kwa kuunda utaratibu tu unaofaa kuwawajibisha wakopaji. Utaratibu wa sasa wa kuachia mzigo wote kwa mabenki si mzuri kwa kua watu wetu vipato bado ni kidogo sana na hawana chochote cha rehani.

Mfano: Serikali inaweza kwa kupitia REAL ESTATES na Banks jenga na kumorgage kwa muda mrefu nyumba, na nyumba hizo hizo wanunuaji wakazitumia kama rehani kwenye mabenki. Chukulia mnunuaji analipia 10% tu malipo ya mwanzo na anapewa doc zote za nyumba.
 
Kwa sababu kila kitu sisi tunalaumu serikali tu. Kwani serikali inapanga hata mishahara ya sekta binafsi?

Kwa nini madaktari wengi wasianzishe practice zao wenyewe....kwa nini makanisa yasianzishe hospitali zao yenyewe. Mimi majuu sijawahi kwenda hospitali ya serikali. Kwanza sijui hata kama kuna hospitali za serikali....[/QU

Hongera yako wewe unae kwenda kwenye private Hospital huko majuu kwako.!! Hivi unategemea kweli kila Daktari ataweza kuanzisha practice yake mwenyewe hapa Tanzania ? Makanisa mengi yana Hospital nyingi tu hapa watanzania.

Na kama una kumbuka Baada ya TRA kuona njia pekee ya kukusanya mapato ni kuwanyima msamaha wa kodi hawa wenye Hospital za Kidini kutokana na kwamba Mahospitali ya kidini ni mengi na yana pata msamaha mkubwa wa Kodi .

Kwahiyo nataka tu kukufahamisha kwamba hospital za kidini zipo, Kwa wale ambao wamezaliwa Majuu na ambao hawajawahi fika Tanzania au walishafika na kuishia kwenye viti vilefu hawawezi kuyatambua matatizo ya nchi hii.

Hii nchi haina system nzuri kwa wafanyakazi wake hata kidogo. ogopa kabisa kufanya kazi serikalini.

Inabidi ifike wakati serikali ikae chini ipange mfumo mzuri kwa wafanyakazi..Hili swala la marupu rupu ni mtego mbaya kwani walio juu ndio wanalitumia kama njia ya kujineemesha.

Marupurupu ni makubwa kuliko mshahara wenyewe. na marupu rupu ni kwa walio juu. Mwalimu au nurse au Medical Assistant kule kijijini atayapata wapi marupu rupu wakati hata hiyo elimu kwa ajili ya kujiendeleza anaisikia redioni kama ana betri.

HII NI DHAMBI !!! ACHENI KABISA WATU WANAISHI KWA SHIDA SANA TANZANIA..!!

Kuchangia mada au post sio tu kuweza kuandika , bali kuwakirisha mawazo yanayoendana na hali halisi ya mada au post iliyotolewa.
 
Kwani na wao ni "The best trained people and individuals with highest intergrity in the society" kama wale wa BOT?

Kama sio hawastahili zaidi ya wanachopata

Mtu mzima mmoja alipata kuniambia kuwa vitu vyote muhimu duniani havina thamani. Drogba na wenzake walipokuwa hapa walifanyiwa dhifa ya kitaifa na mkuu wa nchi pale golden tulip. Haitatokea hali kama hiyo ikiwa atakuja kutembelea Tanzania daktari bingwa wa magonjwa ya moyo toka India au Ufaransa
 
Kwa vile wafanyakazi Benki Kuu wanastahili maisha ya juu kama ya wale wa Benki za nchi zilizoendelea na wabunge wetu nao wanastahili maisha kama ya wabunge wa nchi zilizoendelea; na kwa vile wapo watu wanaostahili katika utumishi wa umma maisha ya kimagharibi.. naomba kuuliza je madaktari wetu wanalipwa mishahara inayolingana na madaktari kama wa nchi za US na UK?

Je itakuwa vibaya kama na wao wakiamua kudai "mastahili" yao kutoka kwa watawala?

au hawastahili nyumba nzuri zenye mabwawa nje na magari na posho kubwa zaidi? Labda niulize tu kwa wastani daktari wa Tanzania analipwa kiasi gani na kiasi kinalinganishwa vipi na daktari wa US.

Hakuna serikali inayopeda watumishi wake wapate tabu hata siku moja suala ni mapato ya nchi yanatosha kukidhi haja hizo.Kada nyingi za utumishi wa umma zina mishahara midgo si tu kwa madaktari ,angalia polisi, walimu n.k

Kama bajeti yetu bado haitokani na mapato yetu ya kwa 100% unategemea mtumishi wa umma awe na mshahara mzuri? pia tukumbuke kuwa kuna taalumu zingine ni wito kama unurse,udaktari na ualimu
 
Nimekupata.. unaonaje kama wabunge, mawaziri, na wakurugenzi wote wa mashirika ya umma wapate 20% pay cut, wajipangishie nyumba wenyewe, na wakati huo huo, serikali iongeze mishahara ya watumishi wote kwa viwango tofauti kutokana na ajira zao kati ya asilimia 20 na 30?

Unaonaje kama wastaafu wote wa serikali waanze kulipwa asilimia 70 ya watumishi walio na nafasi zao sasa (hii inawahusu Marais Wastaafu, Mawaziri Wakuu, wabunge n.k pia)?
 
unajua tanzania kwa sasa hakuna tunachokijali zaidi ya siasa na UANASIASA!kwasababu huko ndiko kuna ''mianya ya fedha''!

TAALUMA KAMA UALIMU na UDAKTARI hazithaminiwi kabisa...!

mianya ya fedha= ?

Geoff hebu tufafanulie.
 
Tatizo ni kwamba Tanzania hatuna scales, natural or artificial, zilizo equitable au reasonable. Hatuna scales, hatuna uchumi rasmi unaoeleweka, hatuna bajeti, hatuna watchdogs, hatuna pressure groups, hatuna civil society, hatuna wa kusema mbunge na gavana si muhimu zaidi ya daktari (zaidi ya sauti chache za hapa na magazeti machache sana).

Hatuna, hatuna hata sensa ya kujua tuna wafanyakazi wangapi wa serikali na wangapi ni madaktari, walimu etc.

Hatuna.

Nikaogopa kwamba tusije kukosa hata mtu wa kusema hatuna, nikasema hatuna.

Mkuu haya ndiyo maneno. Ukitazama kwa harakaharaka kinachojionyesha wazi ni kuwa uongozi wetu umejikita katika kujenga tabaka la wateule (ELITES) wenye maisha tofauti kabisa na wananchi wengi bila mantiki inayoeleweka. Hata ulinganisho tunaojaribu kuutoa ili ku-justify stahili za kada mbalimbali za taaluma, utendaji na uongozi wa kisiasa hauna misingi iliyo wazi. Mwelekeo wa majibu mengi hapa ni kama kupapasa gizani, kufuata utashi binafsi au hata ubabaishaji wa kifisadi tu (kwa wanaotetea status quo).

Kwamba tofauti ya kati ya stahili za baadhi ya wakuu kama Gavana, Spika, Mbunge vis a vis waalimu, madaktari, mainjinia, n.k. inatisha si hoja tena; ni jambo lililo wazi kabisa. Lakini nani anastahili nini Tanzania? Hilo ndilo swali lenyewe.

Nafikiri MMKJJ ameanzisha thread ngumu sana kuijadili na kuitolea hitimisho la uhakika labda kama anataka kuwapa wana-JF ufa wa kupenyezea hasira zao zote kwa mwelekeo wa ELITISM unaozidi kujengwa na watawala wetu. :cool:
 
JAMA JAMA JAMA,
Kuna hizi kazi za kufagia mabarabarani na kuzoa uchafu, hakuna kazi ngumu kama hiyo,
utakuta kwenye uchafu kuna Condom* zilizotumiwa, Mavi*, miozo ya kila namna lakini ukikuta mishahara yao wanavyolipwa kweli Lazima utakubaliana na mimi kuwa sisi Tuna roho mbaya mbaya mbaya sana.

Ukienda Norway utashangaa mwenyewe hao wasafisha jiji/mitaa mshahara wanaopata hao watu wanao safisha miji/mitaa ni mkubwa kuliko wafanyakazi wa maofisi yaani ni kazi inayolipa na wala hauwezi kukuta wakuja kapewa hiyo kazi maana ni HOT CAKE.

Ila huku kwetu tuna wadharau sana wafagiaji kwa jinsi walivyo jichokea.
 
kuna wengi wenu mmeongelea private practise,kwanini daktari asifungue ka jiwe kake,sasa kila mtu akianza kufubgua ka private clinic kake,hizi hospitali za serikali zote zitakufa kutoa huduma,kwa sababu tutakuwa tunakimbia kazini mapema ili ku run ma clinic zetu ili tupate zaidi,kuna mfano live tu,madaktari ambao wamebahatika kupata private zao,muda mwingi wanatoroka mapema kazini,na wakati mwingine pia humwambia mgonjwa njoaa private kwangu,utapata huduma ya haraka.sasa hii ikitokea watanzania maskini wanaotegemea hosp za serikali watafanya nini?hapa ni bora angalau tupate mshahara wa kuridhisha ,tu ta perform with utmost ethics,ama sivyo kila kitu kitakuwa kijiweni.kwa kweli sisi tuna hali ngumu.mimi wakati nilipoanza kazi,na mshahara wa kama 450 laki,hali ilikuwa mbaya sana,unakodi nyumba,laki 250,huja kula,huja vaa,usafiri hamna.mimi mpaka kwa aibu nilikuwa baada ya kazi natafuta njia za mchochoroni,ili wagonjwa wanaonipita wasiniangale na kata mbuga kwa mguu.sometimes wanakucheka daktari mzima huna usafiri.sasa na huu mshahara usafiri utaupata wapi,daladala kila siku kama 1000,sasa kweli utaishi?hapo nimeamua tu kuji stoaway.tanzania basi.unakula zamu masaa 24,hela ya zamu una ambiwa hamna,hospitali haina fungu kwa sasa,na zamu za hosp za mkoa ni za kutesa mno,daktari mmoja unakula zamu masaa 24 hospitali nzima, bila malipo.kweli unasthaili.hosp incentives kwa madaktari hamna,kwa wezetu hapa majuu,kila wiki angalau mnapelekwa dinner na kujiburudisha,anagalu una ji feel kidogo,lakina hapo kwetu wewe ni punda ambaye ulitenda dhambi ya ku soma medicine na kutumikia watanzania.i swear,madaktari wa kitanzania tuna dharau liwa sana.tukumbuke daktari anaokoa maisha,yaani within seconds usipopata medical attention,na uwe tajiri kiasi gani,huna maisha,kama umepata ka acute condition,so why dont respect these important people who saves lives,be poor or rich.na badfo najiuliza zile kamati za ku review mishahara zimepotelea wapi?mbona hakuna majibu,au ziliundwa kwa kujipatia per diem zao na wametoweka.siku nzima mbunge anakaa tu,anakula 100,000,lakina in the same day,daktari anaokoa masiha ya watu zaidi ya kumi in tht same day,so who the hell is important?than why neglect us?
god bless tz doctors and may u find a green pasture even if uhave to deny ur nationality.amen.
 
Kunani Pale TGA umenena vizuri na hiyo ni changamoto kubwa kwetu wote kama Watanzania.

Jana nilikuwa hospitali ya Amana hali niliyoikuta si nzuri hata kidogo. Kuna wodi moja ya kina mama wamejazana na kwa ukubwa wake huitaji zaidi ya shilingi milioni saba kuijenga kikamilifu wodi mpya ya namna hiyo. Tukumbuke mshahara ya marupurupu ya mbunge mmoja kwa mwezi ni hizo shilingi milioni saba. Hii maana yake nini? Kwa kutumia mishahara na marupurupu ya wabunge wetu kila mwezi tuna uwezo wa kujenga wodi za namna hiyo 323.

Binafsi sioni kwa nini mshahara wa daktari usianzie shilingi milioni 1.5 kwa mwezi.
 
Naona pia madaktari na wauguzi wa tanzania wana lugha chafu sana na matusi hawathamini wagonjwa, so hata mimi mtawala nachelea kumpa hela kwani adabu zao ni ndogo sana walio wengi!!? uhusiano si mzuri basi tu yatubidi tuhudhurie hospitals
 
Back
Top Bottom