kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 268
SERIKALI imetangaza kuwalipa watumishi wa umma mishahara yao kupitia madirishani kwa muda wa miezi miwili.
Katika kipindi hicho, itachukua hadhari zote ikiwamo ya kuhakikisha hakutokei uporaji mishahara hiyo ili kuwagundua watumishi hewa wanaotafuna fedha za umma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Hawa Ghasia, alisema hayo juzi mjini hapa kwenye mafunzo ya maboresho ya utumishi wa umma awamu ya pili.
Utaratibu wa kuwalipa watumishi madirishani utakuwa wa muda tu, angalau miezi miwili tu. Nia ni tuwatambue, tusiowaona, tutawaondoa kabisa, alisema Ghasia.
Alisema, ulipaji huo wa mishahara utawezesha kugundua watumishi hewa na kutolea mfano wa uhakiki uliofanywa katika shule za sekondari, ambako moja ilielezwa kuwa ina walimu 17, lakini ikakutwa na walimu wawili na nyingine walimu 70, lakini ukweli ilikuwa na walimu 20.
Kuhusu uboreshaji wa maslahi ya watumishi ikiwamo mishahara, alisema Serikali itaendelea kuiboresha kadri uwezo wa kifedha utakavyoruhusu.
Akiwa kwenye mafunzo hayo, Ghasia aliwataka watendaji wa halmashauri kusimamia vema fedha ili kuondoa mawazo kuwa halmashauri zimejaa wezi.
Kuhusu ajira, alisema kuanzia sasa mtu atakayefaulu usaili wa kazi katika utumishi wa umma na kupangiwa kituo cha kazi, hataitwa tena katika usaili wa kazi yoyote serikalini.
Alisema hiyo ina nia ya kukabiliana na watu ambao wanapewa kazi, lakini wanakwenda kuripoti vituoni na kuchukua fedha za kujikimu, kisha kutoweka.
Waziri Ghasia yuko katika ziara ya mafunzo kuhusu mabadiliko ya utumishi wa umma awamu ya pili na jana alitarajiwa kuwa Misenyi.